Madiwani wa CHADEMA Arusha waibua gumzo

Madiwani wa CHADEMA Arusha waibua gumzo

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
by JOHN BUKUKU | Jambo Leo | NOVEMBER 18, 2012


​
MADIWANI wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(Chadema) wilayani Arusha waliogoma kumtambua Meya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo sasa wanadaiwa kuanza kumtambua kwa kupitia ‘mlango wa nyuma'.

Tangu ufanyike uchaguzi wa meya wa Jiji la Arusha, kumeibuka mvutano wa kisiasa uliosababisha Chadema wawatangazie wananchi kutomtambua Meya huyo.


Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Omari Mkombole akizungumzia matumizi ya fedha zilizotumika katika uzinduzi wa Jiji hilo hivi karibuni alisema kwamba

madiwani wa vyama vyote walishiriki vikao muhimu vya kufanikisha sherehe hizo.

Lakini itakumbukwa ya kwamba msimamo wa madiwani wa Chadema kutomtambua meya huyo ulikuwa ni kutoshiriki vikao vyote vya jiji hilo kama ishara ya kusimamia msimamo wao.


Tayari baadhi ya makada wa Chadema jijini hapa wametoa msimamo wao kwa nyakati tofauti wakati wakihojiwa kuhusiana na hali hiyo ambapo baadhi ya wamelaani kitendo hicho huku wakienda mbali zaidi na kusema kwamba kitendo hicho ni unafiki mkubwa.


"Taarifa zilizonukuliwa nje kama ni siri zilikuwa ni makisio ya bajeti ambayo baada ya kupitiwa ilibadilishwa na kupata bajeti halisi ya sherehe, hili si siri nyaraka madiwani waliohudhuria wanazo vikao vyote hivi vilifanyika kwa ushirikiano wa madiwani wa Tlp, Chadema wasiokuwa na mivutano na chama chao na CCM chini ya Meya wa Jiji la Arusha," alisema Mkombole


Mkombole, akichanganua fedha hizo alisema, zilikuwa ni Sh. 123,689,550 milioni ambapo Mamlaka ya Maji Safi na Taka Arusha (AUWSA) walichangia Sh. 18,156,500 fedha zilizokarabati mnara wa Azimio la Arusha.

Alisema mdau mwingine Kampuni ya Jiangxi- Geo –Engeneering (Group) Corporation inayojenga barabara za Jiji la Arusha ilichangia Sh, 12 milioni , kampuni ya China Railway Seventh Group Co Ltd ilichangia Sh , 4 milioni na kufanya jumla ya Sh Milioni 35 kuchangwa na wadau.


"Halmashauri ya Jiji la Arusha yenyewe imetumia Sh,89,533,050 milioni kugharamia sherehe hizo kwa shughuli mbalimbali zilizobakia mbali na kuwalipa wasanii mbalimbali walioalikwa, fedha hizo pia zilitumika kugharamia chakula cha Rais Kikwete, msafara wake na wageni waalikwa Hoteli ya Mt. Meru," alifafanua kaimu mkurugenzi huyo


Akifafanua kuhusu chakula hicho Mkombole alibainisha kwamba kamati iliyokuwa inasimamia chakula cha Rais Kikwete ilikuwa ikiongozwa na Efatha Nanyaro ambaye ni diwani wa Kata ya Levolosi (Chadema) akishirikiana na Paul Mathysen Diwani wa Moshono kupitia CCM.


Alisema ushiriki wa viongozi hao ambao ni wawakilishi wa wananchi jijini Arusha ulionyesha kwamba suala hilo lilifanyika kwa ridhaa ya Baraza la Madiwani kwa niaba ya wananchi.


Alipotafutwa mwenyekiti wa madiwani wa Chadema jijini hapa,Isaya Doita ambaye ni diwani wa kata ya Ngarenaro alikiri wao kushiriki hatua zote katika maandalizi ya uzinduzi wa jiji hilo na kudai kuwa walipokea posho kwa kuwa ni haki yao na wana njia mbalimbali za kutomtambua meya wa jiji la Arusha.

 
Sh 89,533,050 Jiji la Arusha LILICHANGIA FURAHA ZA CCM KUIITA ARUSHA - JIJI
Na Wachina Walichangia pesa kidogo...

Hizo barabara Wachina Wanazozijenga ni kwa MKOPO lakini kila siku tunapoteza TEMBO WETU... SHAME; SHAME

Madiwani wa CHADEMA hapo wana WALAKINI...

Na SERIKALI ya CCM inayajua HAYO...
 
Cdm hapo arusha kazi wanayo kama ni fukuza fukuza nadhani labda itabidi iendelee! Tatizo njaa! Kweli umasikini ni janga!!
 
Njaaa tu, watafuna nchii kama mchwa, wapiga kura tumekwisha , kumbe nchi hii Dk slaa pekee ndiyo mzalendo
 
Kila mtu anatafuta kula si ccm,CDM cuf ,tlp wajinga Ndio waliwao
 
Jambo leo jambo leo hivi hili gazeti si ni la chama hili, maana lina undugu wa damu na Uhuru. Mie napita tuuuu!!
 
katika siasa usafi ni wa mtu binafsi wala si wa chama chake!!
 
Nadhani Jamboleo hawana mawasiliano sawasawa na wana Arusha,walio ibua ufisadi huwo ni madiwani wa chadema na kama ukikumbuka vizuri Nanyaro aliondoka kwenye kikao kilichopitisha maamuzi, sasa huyu muandishi kama anaoa kuna aufisadi anafurahia chadema kushiriki au anapashwa kuyalipoti kwa vyombo husika amabavyo vinaongozwa na mafisadi wa ccm.Wanatafuta pakutokea.
 
Mkuu wangu nngu007 nakuheshimu sana............................ lakini kwa kupost hii thread kutoka gazeti la Jambo leo umetudharau mkuu. Unaposema Jambo leo manake ni sawa na kusema Gaudence Lyimo, au Kikwete au CCM
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu nngu007 nakuheshimu sana............................ lakini kwa kupost hii thread kutoka gazeti la Jambo leo umetudharau mkuu. Unaposema Jambo leo manake ni sawa na kusema Gaudence Lyimo, au Kikwete au CCM

Gazeti gani kwako linaandika ukweli?!mwananchi sikulikiandika mnavyotaka mnalisifia likiandika msivyotaka mnaliponda....msiyumbishwe na mapenzi hamna binadamu mkamilifu
 
Last edited by a moderator:
Jambo leo nalo ni gazeti la kinafiki, silitofautishi na yale magazeti pendwa.
 
Gazeti gani kwako linaandika ukweli?!mwananchi sikulikiandika mnavyotaka mnalisifia likiandika msivyotaka mnaliponda....msiyumbishwe na mapenzi hamna binadamu mkamilifu

Sipendi media inayoegemea upande moja, either kwa serikali au kwa upinzani, that's obvious, ndo maana naiamini Jf kuliko media nyingine yoyote, kwa sababu habari zake zinapostiwa kama zilivyo.
Siyo jambo leo wala Tanzania daima. Siku zote nasoma habari ambazo ziko sawa.
Jana nilikuwa na Madiwani wawili wa Arusha, na niliwauliza kama ile habari ina ukweli, na wao walishangaa hawajui chochote. what the news is this?
Ficha Upumbavu wako! Usifiche hekima yako! by Invisible
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu nngu007 nakuheshimu sana............................ lakini kwa kupost hii thread kutoka gazeti la Jambo leo umetudharau mkuu. Unaposema Jambo leo manake ni sawa na kusema Gaudence Lyimo, au Kikwete au CCM


Ni kundi gani nimelidharau, Ndugu? Ninaamini UHURU wa JAMII FORUMS kwanini tusijadili chochote?

Mwandishi kaandika na Kwanini HOJA yake ISIJADILIWE? Sababu ya DHARAU??? Na Unajua Mimi ninaishi NJE ya NCHI ninasoma kila kitu kilicho kwenye INTERNET kinachohusu HABARI za TANGANYIKA... Na Habari ninazoziona saa nyingine nzuri; saa nyingine zina utata; saa nyingie sizielewi nawajumuisha WANA JAMII FORUMS nione wao wanaionaje hiyo HABARI na Naishukuru JAMII FORUMS na Members wanaichangia hiyo habari na Ninapata USULUHISHO wangu kutokana na Sababu nilizozieleza...

Sasa SIJUI DHARAU YANGU IKO WAPI !!! But what I believe is all things must be examined, debated, investigated without exception and without regard for anyone's feelings...
 
Sipendi media inayoegemea upande moja, either kwa serikali au kwa upinzani, that's obvious, ndo maana naiamini Jf kuliko media nyingine yoyote, kwa sababu habari zake zinapostiwa kama zilivyo.
Siyo jambo leo wala Tanzania daima. Siku zote nasoma habari ambazo ziko sawa.
Jana nilikuwa na Madiwani wawili wa Arusha, na niliwauliza kama ile habari ina ukweli, na wao walishangaa hawajui chochote. what the news is this?
Ficha Upumbavu wako! Usifiche hekima yako! by Invisible
Mambo mangapi ya uwongo yanaletwa hapa JF ........wewe Ndio ufiche uwo upumbavu wako kwa kuamini kuwa Kila kinacholetwa JF ni ukweli nakila unaloambiwa ni ukweli....ukweli ni ule uliouthibitisha wewe sio kwa kuambiwa .
 
Last edited by a moderator:
magazeti yaliyo kwenye harakati dhidi ya CDM ..sasa unategemea yaandikeje?.. la msingi ni kuyafungia vioo... shit!!
 
Back
Top Bottom