Madiwani Kigamboni wamshukia Ndugulile

Madiwani Kigamboni wamshukia Ndugulile

Mkuu FUSO alisema mwenyewe akiwa bungeni akimlaumu mama Tibaijuka kwa kumlipa fidia yeye kwa lengo la kumziba mdomo,na alipotishiwa kuichwa kwenye chama kwa usaliti moto wote ukazima"
mkuu una uhakika alishalipwa fidia? maana tunavyojua sisi familia yao wana nyumba kigamboni tangu miaka hiyo na ndiyo hiyo inayoongelewa na hakuna mkazi yoyote wa kigamboni aliyelipwa as of now.
 
madiwani wengi wa kigamboni hawajui wanataka nini...... Wengine wana magari ya wizi, wengine wanahongwa vigori, wengine walipanda gari kwenda dodoma hotel nk

daktari is too advanced kwao, sijui kwanini alijiigiza kwenye hao wapuuzi, his vision doesnt match madiwani na chama alichopo

Hapo kwenye red,hasa diwani dotto
 
Madiwani wanakataa nn nani hajui kama wanatumika?
 
Madiwani hawa wana chekesha. Mnadai mbunge ana wachonganisha na wananchi wenu sasa badala ya kwenda kwenye kata zao kujieleza wana panda pantoni kwenda kutoa press conference.
 
MADIWANI wa mji wa Kigamboni wamemtaka mbunge wa jimbo hilo, Faustine Ndugulile, kuomba radhi kutokana na kauli yake kuwa hawajui kitu kinachoendelea katika uanzishaji wa mji mpya wa Kigamboni (KDA).

Faustine aliwatuhumu madiwani hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mji Mwema Februari 23 mwaka huu kuwa ni mbumbumbu juu ya suala hilo na kwamba walisafiri kwenda mkoani Dodoma kufanya kikao cha kujadili uundwaji wa KDA bila mbunge huyo kufahamu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Madiwani wa Kigamboni, Selemain Methew, alisema kuwa mbunge wao amekiuka taratibu za uongozi kutokana na kuwachonganisha na wananchi katika mradi huo.

Alisema mbunge amekuwa kigeugeu kwa kuwazunguka madiwani katika mipango mbalimbali ambayo mwisho wa siku anajitoa na kwenda kuzungumza na wananchi.

Methew alibainisha kuwa safari ya madiwani wa Kigamboni kwenda Dodoma, mbunge wao ndiye aliyependekeza, lakini sasa anarudi nyuma na kusema hatambui uwepo wa kikao hicho.

Kwa upande wake, mlezi wa kamati, Diwani wa Tungi, Kanali mstaafu, Abel Luambano, alisema Ndugulile anakiuka taratibu za utawala bora na maazimio ya kikao walichofanya Dodoma na kwamba mgongano uliopo ni kiongozi kutokujua mipaka ya madaraka yake.

Jitihada za Tanzania Daima kumtafuta Ndugulile kupitia simu yake ya kiganjani kuzungumzia madai hayo hazikufanikiwa.

Source: Tanzania Daima | na Chalila Kibuda

Njaa ni ulemavu mbaya sana. Mama Tiba anajua kutumia pesa kupata sapoti ya madiwani bila ridhaa ya wananchi. Anaelewa fika Mbunge ni tishio kwenye mkakati wake wa kifisadi. Kama kutatokea umwagaji damu (Mungu aepushe) itakuwa juu ya Anna Tibaijuka.
 
MADIWANI wa mji wa Kigamboni wamemtaka mbunge wa jimbo hilo, Faustine Ndugulile, kuomba radhi kutokana na kauli yake kuwa hawajui kitu kinachoendelea katika uanzishaji wa mji mpya wa Kigamboni (KDA).

Faustine aliwatuhumu madiwani hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mji Mwema Februari 23 mwaka huu kuwa ni mbumbumbu juu ya suala hilo na kwamba walisafiri kwenda mkoani Dodoma kufanya kikao cha kujadili uundwaji wa KDA bila mbunge huyo kufahamu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Madiwani wa Kigamboni, Selemain Methew, alisema kuwa mbunge wao amekiuka taratibu za uongozi kutokana na kuwachonganisha na wananchi katika mradi huo.

Alisema mbunge amekuwa kigeugeu kwa kuwazunguka madiwani katika mipango mbalimbali ambayo mwisho wa siku anajitoa na kwenda kuzungumza na wananchi.

Methew alibainisha kuwa safari ya madiwani wa Kigamboni kwenda Dodoma, mbunge wao ndiye aliyependekeza, lakini sasa anarudi nyuma na kusema hatambui uwepo wa kikao hicho.

Kwa upande wake, mlezi wa kamati, Diwani wa Tungi, Kanali mstaafu, Abel Luambano, alisema Ndugulile anakiuka taratibu za utawala bora na maazimio ya kikao walichofanya Dodoma na kwamba mgongano uliopo ni kiongozi kutokujua mipaka ya madaraka yake.

Jitihada za Tanzania Daima kumtafuta Ndugulile kupitia simu yake ya kiganjani kuzungumzia madai hayo hazikufanikiwa.

Source: Tanzania Daima | na Chalila Kibuda

Kama hawa madiwani wanaufahamu vizuri huu mradi wa Kigamboni, Tibaijuka alifikiaje hatua hii bila wao kujua?

[h=2]Tibaijuka azua tafrani Kigamboni[/h]

Na Moshi Lusonzo

26th January 2013

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

headline_bullet.jpg
Madiwani kuitisha kikao kumpinga

TibaijukaNHC1%283%29.jpg

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka

Tangazo la Serikali kulichukua eneo lote la Kigamboni na kuliondoa chini ya mamlaka ya Manispaa ya Temeke, limezua tafrani baada ya madiwani kutaka kuitisha kikao maalum cha kupinga hatua hiyo.

Katika kutimiza azma yao hiyo, wameanza kukusanya saini za madiwani wanaofikia nusu na robo ili kiitishwe kikao walichokiita kuinusuru Temeke.

Hivi karibuni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alitangaza kulitwaa eneo la Kigamboni na kuongeza ukubwa wa eneo kwa kuchukua kata zingine kwa ajili ya uanzishwaji wa jiji la kisasa la Kigamboni.

Katika hatua hiyo, Profesa Tibaijuka alitangaza kuanzishwa kwa chombo cha Wakala wa Kuendeleza Mji wa Kigamboni (KDA) ambapo hatua hiyo inaiondoa kutoka Manispaa ya Temeke kiutawala.

Madiwani hasa kutoka Kigamboni wameliambia gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao kuwa kuondolewa kwa kata zao kuwa chini ya Manispaa ya Temeke imewafanya kutojua hatma yao pamoja na wananchi kukosa sehemu ya kukimbilia.

Walisema kitendo cha Serikali kuwaondoa kibabe bila kuwashirikisha kimezidisha hofu kwa wananchi wa eneo hilo ambao tangu mradi huo uanze kuandaliwa, wamerudishwa nyuma kimaendeleo.

Mmoja wa madiwani hao alisema wameanzisha zoezi maalum la kukusanya saini za madiwani kwa ajili ya kuomba kuitishwe kikao cha dharura cha madiwani kwa ajili ya kujadili kauli ya Waziri huyo.

"Tumeshtushwa sana na kauli ya waziri Profesa Tibaijuka, ni hatua ya kibabe iliyochukuliwa bila kutushirikisha sisi madiwani, haiwezekani kutuondoa manispaa ya Temeke bila kufuata utaratibu wa kisheria," alisema diwani huyo.

Alisema kitu cha kushangaza, Serikali imeongeza kata zingine nne na kuziingiza kwenye mradi bila kutoa taarifa kwa wananchi ili waweze kujadili na kutoa maoni yao.

Kata zilizoingizwa kwenye mradi huo ni Kisarawe 11, Kimbiji, Somangila na Pembamnazi, ambapo kata zilizokuwa awali ni Kigamboni, Tungi, Kibada, Mjimwema na Vijibweni.

"Tutalazimika kukutana haraka kuona jinsi gani tutaijibu serikali kwa maamuzi yake haya ya ukandamizaji, sisi ni wawakilishi wa wananchi kwa nini wanafanya mambo yao kwa usiri mkubwa na kisha kutupa taarifa kama vile huku hakuna mamlaka inayokubalika," aliongeza kusema Diwani mwingine.

Imeelezwa mpaka jana tayari saini za madiwani zilikuwa zimepita nusu ya idadi inayotakiwa na hivyo wakati wowote kuna uwezekano wa kuitishwa kwa kikao hicho.
Madiwani hao wamepingana na kauli ya Waziri huyo kwamba wataingia katika Baraza la Ushauri la KDA kwa sababu mpaka jana hakukuwa na taarifa zozote za kikao.

Awali Profesa Tibaijuka alisema kutokana na kuanzishwa kwa KDA, kata zote za Kigamboni, zitaungana na madiwani wake na mbunge wao watakuwa wakikutana katika Baraza la Ushauri la KDA.

Alisema wananchi wa Kigamboni ambao wako kwenye maeneo ambayo yatahitajika kwa ajili ya ujenzi huo watashirikishwa ipasavyo katika mchakato mzima ikiwa ni pamoja na kulipwa fidia zao kwa wakati.
 
Na kama Mbunge aliwapangia wakakutane na Tibaijuka Bungeni ikawaje Mbunge katolewa nje bungeni kwa kuhoji madiwani hao kuitwa na Tibaijuka bungeni? Soma hapa Hadubini - My-o-scope: Mbunge wa Kigamboni Atolewa Bungeni kwa Kuwatetea Wananchi Wake

Kwa ujumla madiwani hawa wana akili finyu sana na wanadhani wananchi wanakubaliana na hiyo njaa yao. Tibaijuka anaonekana kutumia mbinu za kitapeli na kifisadi kulazimisha uhalali wa mradi wa mji wa Kigamboni
 
Mh. Ndugulile ana ugonjwa unaitwa "Obsession" ya kupinga mradi uliondani ya Ilani ya chama chake. Ibara 60 (b)(iv). Anatushangaza wengi.

Hana jipya. Kimsingi Jimbo halina mbunge litasota mpaka 2015. Nakubaliana na mnaosema ukichagua vibaya unaishi vibaya.
 
Hawa madiwani wameingizwa mjini na mama tibaijuka.
Safi dr.ndungulile, endelea kuwachapa madiwani njaa kali wamewauza wakazi wa kigamboni kwa vipande thelathini vya pesa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Duhh" hao madiwani kasheshe mmoja Dalali pale wizara ya Ardhi, Mwingine Mfanyamaigizo katika kupoteza magari ya watu na huyo mwingine ni kamanda mstaafu aliyepoteza uelekeo wakati mathew anajiandaa kugombea ubunge huko Lindi kwa kupeleka unga katika jimbo mmoja waache wakusanye hela za maandalizi
 
Halima Mdee is the biggest disappointment kwa Vijana wanaopenda mageuzi
hakuna kitu pale na anajua hawezi kurudi

Anajipa moyo kuwa hata hasiporudi atapata 'viti maalum'...ndio inayomfanya hasijali!
 
Mh. Ndugulile ana ugonjwa unaitwa "Obsession" ya kupinga mradi uliondani ya Ilani ya chama chake. Ibara 60 (b)(iv). Anatushangaza wengi.

Hana jipya. Kimsingi Jimbo halina mbunge litasota mpaka 2015. Nakubaliana na mnaosema ukichagua vibaya unaishi vibaya.
madai ya ngugulile huyajui mkuu..sisi wakazi wa kigamboni tunaona atleast yeye anatetea wananchi sio hawa wapuuzi madiwani
 
Nchi hii kweli ni ya sarakasi. Waziri ni wa CCM, madiwani wengi ni wa CCM, mbunge ni wa CCM ila bado wenyewe kwa wenyewe hawaelewani.

Bora tufanye mabadiliko tu
 
Na kama Mbunge aliwapangia wakakutane na Tibaijuka Bungeni ikawaje Mbunge katolewa nje bungeni kwa kuhoji madiwani hao kuitwa na Tibaijuka bungeni? Soma hapa Hadubini - My-o-scope: Mbunge wa Kigamboni Atolewa Bungeni kwa Kuwatetea Wananchi Wake

Kwa ujumla madiwani hawa wana akili finyu sana na wanadhani wananchi wanakubaliana na hiyo njaa yao. Tibaijuka anaonekana kutumia mbinu za kitapeli na kifisadi kulazimisha uhalali wa mradi wa mji wa Kigamboni

1. Diwani wa Somangila - CCM (mama Mpanjila) - kuna tetesi kwamba hatogombea tena udiwani mwaka 2015 baada ya kuupata kwa mbinde, chakachusm, na mizengwe mingi mwaka 2010 (kuna watu wanashikana mashati sasa hv kuwania hii nafasi), hivyo hajishughulishi sana na kuwatetea wananchi wala kuwaelimisha kuhusu hatima yao ndani ya huu mradi

2. Diwani wa Tungi - CCM (mzee Luambano) - alipenyea kwenye tundu la sindano mwaka 2010 (ingawa tetesi ni kuwa uchakachuzi ulifanyika), ni mwanajeshi mstaafu ambaye alishapigika sana kimaisha, angalau sasa udiwani umemtoa kidogo na hata kale ka-pub kake pale tungi ameweza kukafufua tena. Haonyeshi matumaini na hana jitihada zozote za kuwatetea wananchi zaidi ya kuangukia kwenye kundi la wachumia tumbo na mwenzie wa vijibweni. Yuko busy kwenye mtandao wa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa 2015, ingawa kwa sasa hakubaliki

3. Diwani wa Vijibweni - CCM (Selemani Mathew) - huyu jamaa ni very deceptive ... ana siasa za ghilba na maslahi binafsi kwake ni mbele. Anajipanga zaidi kwa 2015 katika mtandao wao walioutengeneza na wenzie. Ana mwaga pesa kama njugu kwa akina mama na vijana katika kata yake na baadhi ya matukio anayoalikwa. Anatumia fursa zozote za mkusanyiko kutengeza publicity. Ana malengo yake binafsi ya kupanda kisiasa kupitia mtandao wa wanasiasa wa serikalini hivyo utetezi wa kero za wananchi katika mradi wa kigamboni hauna tija kwake na hajishughulishi kabisa; anatumia sana manipulative tactics katika kuficha haiba ya siasa yake ingawa wananchi wengi wameshamjua na wanakula tu hela yake.

3. Diwani wa Kigamboni - CCM (Dotto Msawani) - Habari zake nyingi ziko humu JF ... ndio wale wale!

Kifupi, .... hatma ya maslahi ya wananchi wa kigamboni its still a nightmare!
 
kwa hiyo mkuu REMSA una maana hizi statement zake zote ni usaliti kwa kwananchi wa kigamboni?

Dk. Ndugulile: Chama changu kinaniunga mkono katika hili. Tulishazungumza ndani ya chama na kama itatokea nikaitwa na kuambiwa nisipingane na serikali itabidi kwanza watambue kuwa mimi nimechaguliwa na wananchi, nitasema kwa masilahi ya wananchi, naomba wana CCM wanielewe juu ya hili la wananchi wangu.

Swali: Inasemekana kutolewa kwako bungeni, kumekufanya urudi nyuma katika harakati za kuwapigania wananchi kudai masilahi yao. Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Dk. Ndugulile: Siwezi kuwasaliti wananchi,labda wao wafanye hivyo kwangu, nami msimamo wangu ni ule ule. Serikali irudi kwa wananchi ikawaambie mradi huo utaanza lini, haki ya msingi ya Wana Kigamboni ni ipi katika mradi huu? Mradi utaanzia wapi?

Wana Kigamboni wanataabika tangu wameingia kifungoni Oktoba mwaka 2008 na hawana matumaini ya kutoka kifungoni. Hawajui tarehe ambayo serikali itawatoa kifungoni, serikali imekuwa kimya mno na majibu ambayo yamekuwa yakitolewa ikiwa pamoja na yale ambayo yametolewa katika hotuba mbalimbali za viongozi, hayaashirii kwamba serikali inawatakia neema Wana Kigamboni.

Mbunge atueleze ukweli mradi huu utakuwa chini ya nani, na kwa maslahi ya nani?
je ni wawekezaji au serikali? kwenye ramani kuna shule zinaonyeshwa "for whites only"
hiki ni nini na ni kwa nini? Na kwa sasa nini kinachoendelea? hizo fidia zinazosemwa 70,000
na 35,000 kwa sq meter je sio siasa? Mwambie mbunge ajibu haya atakuwa siyo mnafiki"

Chezea ccm weye"
 
Back
Top Bottom