Madiwani Kigamboni wamshukia Ndugulile

Madiwani Kigamboni wamshukia Ndugulile

mimi ni miongoni mwa wahanga ambao tumo ndani ya sakata hili na serikali, ki ukweli mh. Ndugulile anatutetea sana, hawa madiwani wanataka kutuzunguka, wanaenda kuongea na waziri bila hata kukusanya maoni yetu. ndiyo maana ki-ujumla huu mradi umejaa usiri mkubwa.

Hawa madiwani hawajatimiza wajibu wao wa kukusanya maoni ya wananchi na kinachokubaliwa kwenda kukiwakilisha kwa mbunge ili wote kwa pamoja (Mbunge, madiwani) waende kwa waziri kumpa kitu kamili ambacho kinatoka kwa wananchi. sasa wao wanachofanya ni kumzunguka mbunge, kutuzunguka sisi wananchi wamiliki wa eneo hili then wanaenda moja kwa moja kwa waziri kusema mambo ambayo sisi hatujaafikiana nao.

Natoa pongezi zangu za dhati kwa mbunge wetu Ndugulile, anatutetea sana kuhusu mradi huu na anajaribu kila kiwezekanalo ili uwe na haki, uwazi na ukweli.
 
kwa kigamboni picha ndo kwaanza inaanza tena ni ya kihindi, huo mzunguko wake sasa mbona kazi sana. si hayo tu subirini hao madiwani wenu wajifanye kichwa ngumu mda si mrefu mtajutia maamuzi yenu, tunaw3asubirini na second episode.:-*😛layball:😛layball:😛layball:😛layball: 😛layball:pamoja tuijenge tzania yetu hii nzuri
 
Hiyo ya Kawe hapo unampa 'promo' tu Halima Mdee...mimi ni pro-Chadema supporter lakini sijawahi kuona mBunge dhahifu kushughulikia kero za wananchi wa jimboni kwake kama Halima Mdee. Nakubali ni mBunge mahiri kwa kushughulikia mambo ya kiTaifa, lakini Mdee hujachaguliwa na Taifa, umechaguliwa nasi wanaKawe...na hutujali, tuna kero kibao, tunatengeneza vikamati vya kujitolea na task-forces kufuatilia kero zetu pasi wewe kushiriki hata kidogo!

Bwana Riwa naungana na wewe kwa asilimia chache walau ambazo binafsi ni practical kwangu. Mimi kama mmoja kati ya wakazi wa jimbo lake tuliwahi pamoja na wenzangu kumuuliza kuhusu suala la maji akaishia kujibu general tu wala hakuwa na majibu thabiti. Kama mbunge ambaye anatakiwa kuwalink wananchi wake na serikali alipaswa kuwa na majibu thabiti yaliyosheheni. Am disappointed. Wakazi wengi wa Makongo Juu na vitongoji vingine wanalalamika sana ishu ya maji haijatolewa suluhu mpaka leo ila hamna hata kuona kuna hatua kadha wa kadha zimechukuliwa. Very disappointing
 
huyu mbunge hana ushauri mzuri na kuna hisia kuwa ana agenda ya siri naye kwenye mradi wa kigamboni, kwa mfano amekuwa akituhumiwa kushindwa kuipa kamati ya wanakigamboni ushirkiano na utaalamu
 
Mnaweza kukesha kumlaumua mbunge au madiwani lakini ukweli unabaki palepale kuwa iwapo sheria ya nchi ya ardhi inaipa nguvu kubwa wizara kuliko local governments wawakilishi hawa hawataweza kumsimamisha mama Tibaijuka kuendekea na mikakati ya wizara ya jiji jipya la Kigamboni.
yes, hizi sheria ndizo zinaibuka migogoro ya ardhi kila sehemu katika nchi yetu.
 
huyu mbunge hana ushauri mzuri na kuna hisia kuwa ana agenda ya siri naye kwenye mradi wa kigamboni, kwa mfano amekuwa akituhumiwa kushindwa kuipa kamati ya wanakigamboni ushirkiano na utaalamu
hiyo kamati umeiunda lini na mlipitia mchakato upi? wananachi wa kigamboni hawaitambui. haya ndiyo mapungufu tunayoyaongelea.
 
JUMATATU, FEBRUARI 25, 2013 20:49 NA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

MADIWANI wa Kigamboni wamemtaka Mbunge wa Jimbo hilo, Dk. Faustine Ndungulile, kuwaomba radhi kutokana na kauli yake chafu dhidi yao. Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, madiwani hao walisema mbunge huyo amewadhalilisha kwa kuwaita mbumbumbu wasiokuwa na elimu ya mipango miji.

Akisoma tamko hilo kwa niaba ya wenzake, Diwani wa Kata ya Vijibweni, Suleiman Mathew, alisema kauli ya mbunge huyo haikuwa na maana nyingine zaidi ya kuwadhalilisha madiwani.

Katika tamko hilo, madiwani hao walimtaka Dk. Ndungulile kuheshimu mipaka yake ya kazi na kwamba madiwani wa Kigamboni si mbumbumbu kama alivyodai mbunge huyo.

“Kutokana na maneno yaliyotamkwa na mbunge wa Kigamboni, tunakanusha kwa nguvu zetu kuwa aliyoyasema si ya kweli, bali yana lengo la kutuchonganisha na wananchi.

“Sisi sote ni viongozi, kila mmoja ni mwakilishi wa wananchi kwa ngazi yake, tunaomba tuheshimiane, kitendo cha mbunge kusema madiwani wa Kigamboni ni mbumbumbu kimetukera sana.

“Tunamtaka mbunge atuombe radhi kutokana na maneno yake machafu dhidi yetu, kwani ametudhalilisha kwa kiasi kikubwa mbele ya wananchi,” alisema Mathew.

Madiwani wengine waliokuwa wameandamana na Mathew ni pamoja na Diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa, Diwani wa Mji Mwema, Halima Kisenga na Diwani wa Tungi, Abel Luambano.

“Sisi madiwani tunapenda kuwahakikishia wananchi wa kata zetu kwamba tupo makini juu ya mpango mzima wa mji mpya Kigamboni, ili kuhakikisha maslahi ya wananchi wa Kigamboni yanapatikana.

“Suala la mbunge la kuwazuia madiwani kutofanya mikutano kwenye kata zao mpaka wapewe kibali na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, inaonyesha kwamba haelewi mipaka ya madaraka yake.

“Sisi madiwani tunamtaka mbunge awe mkweli juu ya suala la Mji Mpya wa Kigamboni, kwani kauli za uchochezi ambazo anazitamka kwenye mkutano zitasababisha uvunjifu wa amani,” alisema Luambano.

“Kutokana na mbunge kutotambua mipaka, kanuni na taratibu za uongozi na utawala bora kwa bahati mbaya au kwa makusudi, aelewe kuwa sisi ni viongozi wa kuchaguliwa na tuna mipaka yetu.

Suala la kutueleza sisi madiwani, wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji kuwa ni mambumbumbu na hatuna elimu ni kutudhalilisha,” alisema diwani mwingine

Uh Kigamboni kubaya hakumrudishi Mbunge wake Mara ya pile... kila wakati ni MPYA
 
Hapa hakuna hata mwenye nafuu,mbunge haweki wazi juu nini kinachoendelea kuhusu Kigamboni,
na hii ni kwa sababu yeye alishalipwa fedha ya fidia na Tibaijuka kama rushwa ili kumfunga mdomo
maana isingekuwa rushwa wakazi wa Kigamboni wote wangelipwa kwa nini peke yake? Na ukweli
halisi wa nini kinaendelea kuhusu Kigamboni Dr.Ndungulile anaujua kwa nini asiweke wazi?

Madiwani wako kisiasa zaidi kwenye suala nyeti kama hili wao wanajazwa ujinga na mawziri na kuubeba
ujinga huo kuuleta kwa wananchi kuupigia debe bila kujua ukweli haswa wa KDA"

Watanzania wa Kigamboni wataendelea kufanywa wajinga kwa sababu ktk hili hakuna kiongozi aliye tayari
kusema ukweli halisi wa kilichojificha juu ya ujenzi wa mji mpya."But time will tell"
 
MAdiwani wa Kigamboni sio mbumbumbu hata kidogo bali wanajua wanawasaliti wananchi waliowachangua kwa makusudi ya matumbo yao maana mungu wao ni Tumbo!!
 
mimi ni miongoni mwa wahanga ambao tumo ndani ya sakata hili na serikali, ki ukweli mh. Ndugulile anatutetea sana, hawa madiwani wanataka kutuzunguka, wanaenda kuongea na waziri bila hata kukusanya maoni yetu. ndiyo maana ki-ujumla huu mradi umejaa usiri mkubwa.

Hawa madiwani hawajatimiza wajibu wao wa kukusanya maoni ya wananchi na kinachokubaliwa kwenda kukiwakilisha kwa mbunge ili wote kwa pamoja (Mbunge, madiwani) waende kwa waziri kumpa kitu kamili ambacho kinatoka kwa wananchi. sasa wao wanachofanya ni kumzunguka mbunge, kutuzunguka sisi wananchi wamiliki wa eneo hili then wanaenda moja kwa moja kwa waziri kusema mambo ambayo sisi hatujaafikiana nao.

Natoa pongezi zangu za dhati kwa mbunge wetu Ndugulile, anatutetea sana kuhusu mradi huu na anajaribu kila kiwezekanalo ili uwe na haki, uwazi na ukweli.

Mbona hakukutetea na wewe ukalipwa fidia kama yeye alivyoplipwa,kwa nini alipotishiwa kupelekwa
kamti ya chama akaufyata?
 
all in all wananchi wa jimbo lote la kigamboni hawana umoja.....hata kwenye kuchagua wanachagua kutokana na ushabiki na si utendaji...madiwani wengi wamepita kutokana na uzawa uwenzetu (angalau hii uwenzetu kidogo ilikosa nguvu uchaguzi wa '10) na majungu plus elfu mbîli mbili zao na hayo ndo matokeo yake..... maana mwisho wa siku wanajua watapata viwanja vyao kadhaa maisha yao mstari
 
Mbona hakukutetea na wewe ukalipwa fidia kama yeye alivyoplipwa,kwa nini alipotishiwa kupelekwa
kamti ya chama akaufyata?
kaka hapo pekundu mimi sijui chochote kama mbunge wangu alishalipwa fidia, na sidhani anaweza kuwasaliti wana kigamboni kiasi hiki. kwa kuwa na yeye mi member basi tusuburi aje atoe ufafanuzi zaidi.
 
Wenzake wakina Mnyika wanafanya Mikutano kukusanya Kero za wananchi ndio maana yangu kumuona. Sasa nije mjini kufanya nini? Kumuona Ndungulile? Wakati wakati wa kura nilipigia mjini? Hebu peleka ujinga huko! Kwahiyo anawakilisha watu wa mjini wakati sisi wapiga kura wake tuna Kero ambazo anatakiwa aziwakilishe serikalini au atakuja tena 2015?

2015 huwezi kumtoa mwenyewe inabidi ushirikiane na wananchi wenzako wa mbagala ,,,, je unawatayarisha vipi wananchi wenzako kuyatafuta mabadiliko 2015 mkuu?
 
[Hiyo ya Kawe hapo unampa 'promo' tu Halima Mdee...mimi ni pro-Chadema supporter lakini sijawahi kuona mBunge dhahifu kushughulikia kero za wananchi wa jimboni kwake kama Halima Mdee. Nakubali ni mBunge mahiri kwa kushughulikia mambo ya kiTaifa, lakini Mdee hujachaguliwa na Taifa, umechaguliwa nasi wanaKawe...na hutujali, tuna kero kibao, tunatengeneza vikamati vya kujitolea na task-forces kufuatilia kero zetu pasi wewe kushiriki hata kidogo!]

NAUNGA HOJA MKONO HATA HUKU SALASALA KWA BABU MDEE TUNAMSIKIA TU:lying:
 
kaka hapo pekundu mimi sijui chochote kama mbunge wangu alishalipwa fidia, na sidhani anaweza kuwasaliti wana kigamboni kiasi hiki. kwa kuwa na yeye mi member basi tusuburi aje atoe ufafanuzi zaidi.

Mkuu FUSO alisema mwenyewe akiwa bungeni akimlaumu mama Tibaijuka kwa kumlipa fidia yeye kwa
lengo la kumziba mdomo,na alipotishiwa kuichwa kwenye chama kwa usaliti moto wote ukazima"
 
kwa hiyo mkuu REMSA una maana hizi statement zake zote ni usaliti kwa kwananchi wa kigamboni?

Dk. Ndugulile: Chama changu kinaniunga mkono katika hili. Tulishazungumza ndani ya chama na kama itatokea nikaitwa na kuambiwa nisipingane na serikali itabidi kwanza watambue kuwa mimi nimechaguliwa na wananchi, nitasema kwa masilahi ya wananchi, naomba wana CCM wanielewe juu ya hili la wananchi wangu.

Swali: Inasemekana kutolewa kwako bungeni, kumekufanya urudi nyuma katika harakati za kuwapigania wananchi kudai masilahi yao. Je, kuna ukweli wowote kuhusu hili?

Dk. Ndugulile: Siwezi kuwasaliti wananchi,labda wao wafanye hivyo kwangu, nami msimamo wangu ni ule ule. Serikali irudi kwa wananchi ikawaambie mradi huo utaanza lini, haki ya msingi ya Wana Kigamboni ni ipi katika mradi huu? Mradi utaanzia wapi?

Wana Kigamboni wanataabika tangu wameingia kifungoni Oktoba mwaka 2008 na hawana matumaini ya kutoka kifungoni. Hawajui tarehe ambayo serikali itawatoa kifungoni, serikali imekuwa kimya mno na majibu ambayo yamekuwa yakitolewa ikiwa pamoja na yale ambayo yametolewa katika hotuba mbalimbali za viongozi, hayaashirii kwamba serikali inawatakia neema Wana Kigamboni.
 
Back
Top Bottom