Jangakuu
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 513
- 221
MADIWANI wa mji wa Kigamboni wamemtaka mbunge wa jimbo hilo, Faustine Ndugulile, kuomba radhi kutokana na kauli yake kuwa hawajui kitu kinachoendelea katika uanzishaji wa mji mpya wa Kigamboni (KDA).
Faustine aliwatuhumu madiwani hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mji Mwema Februari 23 mwaka huu kuwa ni mbumbumbu juu ya suala hilo na kwamba walisafiri kwenda mkoani Dodoma kufanya kikao cha kujadili uundwaji wa KDA bila mbunge huyo kufahamu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Madiwani wa Kigamboni, Selemain Methew, alisema kuwa mbunge wao amekiuka taratibu za uongozi kutokana na kuwachonganisha na wananchi katika mradi huo.
Alisema mbunge amekuwa kigeugeu kwa kuwazunguka madiwani katika mipango mbalimbali ambayo mwisho wa siku anajitoa na kwenda kuzungumza na wananchi.
Methew alibainisha kuwa safari ya madiwani wa Kigamboni kwenda Dodoma, mbunge wao ndiye aliyependekeza, lakini sasa anarudi nyuma na kusema hatambui uwepo wa kikao hicho.
Kwa upande wake, mlezi wa kamati, Diwani wa Tungi, Kanali mstaafu, Abel Luambano, alisema Ndugulile anakiuka taratibu za utawala bora na maazimio ya kikao walichofanya Dodoma na kwamba mgongano uliopo ni kiongozi kutokujua mipaka ya madaraka yake.
Jitihada za Tanzania Daima kumtafuta Ndugulile kupitia simu yake ya kiganjani kuzungumzia madai hayo hazikufanikiwa.
Source: Tanzania Daima | na Chalila Kibuda