Madiwani hawa hawafai hata kidogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani hawa hawafai hata kidogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JERUSALEMU, Oct 25, 2012.

 1. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,804
  Trophy Points: 280
  Halmashauri ya Morogoro vijijini imekuwa haiishiwi vituko, baada ya uchunguzi wangu wa muda mrefu nimegundua kuwa tatizo lipo kwa madiwani wao.Wamekuwa wakikiuka taratibu za utumishi bila kujali athari za kiutendaji na tija ya mfanyakazi kwa ujumla.

  Mathalani katika kipindi cha miaka miwili madiwani hawa wamemshinikiza AFISA ELIMU SEKONDARI kuwa demote wakuu wa shule 15 bila sababu za msingi na mbaya zaidi wanaachwa katika vituo vyao vilevile vya zamani, Je,wanategemea walimu hawa watafanyakazi yenye tija kweli? kama kuna makosa serious wamefanya ni bora wafukuzwe kazi kuliko kuwapa mateso ya kisaikolojia.

  Lakini pili hawa walimu kimsingi hawata kuwa na tija tena darasani,kama siyo kuwakomoa na visasi vya kisiasa ni nini?? HUYU AFISA ELIMU SEKONDARI NAE AMULIKWE kwani wila yake imekuwa na matokeo mabaya ya kidato cha nne kila mwaka sababu kila kukicha anawaza namna ya ku implement fitna za wana siasa badala ya kufanyakazi.

  USHAURI WANGU

  Madiwani wajengewe uwezo wa namna ya kusimamia maendeleo katika maeneo yao lakini wazingatie sheri,kanuni na taratibu za utumishi wa umma,pia watambue kuwa mahali pasipo na utulivu na amani hakuna maendeleo.
   
 2. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hivi mdiwani wanajua kweli hata jinsi shughuli za elimu zinavyoendeshwa au wanakurupuka tu?
   
 3. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,804
  Trophy Points: 280
  wapo wachache wanajua ila walio wengi hawana ufahamu wa kutosha. Ni wajibu wa serikali kuwajengea uwezo ili ku balance mambo. ninavyoona mimi baadhi ya watendaji serikalini hasa wanao karibia kustaafu wanapokea kila kitu kutoka kwa madiwani bila kupembua mambo kwa faida ya serikali na umma wa atanzania kwa ujumla.HAIWEZEKANI UKUBALI KUM DEMOTE MKUU WA SHULE HALAFU UNAMWACHA KITUO KILEKILE,HUMTAKII MEMA MKUU MPYA.VILEVILE UNA MWATHIRI KISAIKOLOJIA HUYU ULIYE M DEMOTE,JE ANGEKUWA YEYE ANGEJISIKIAJE?
   
 4. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakulaumiwa ni hao maafisa elimu kutojua wajibu wao, kama wataalamu hawapaswi kufanya kazi kwa kukurupuka. Wanatakiwa kuwaeleza ukweli hao madiwani. Mara nyingi siku hizi maafisaelimu wanateuliwa kwa fadhila na si uwezo wao wa kazi! Kawaida siasa inatakiwa itumikie utaalamu na si utaalamu kuitumikia siasa!
   
Loading...