Madiwani CHADEMA wafichua ufisadi wa Bilioni 11 unaohusisha viongozi wa CCM, TAMISEMI na Hazina

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Madiwani wa CHADEMA wa Halmashauri ya Geita wamefichua nyaraka za ufisadi kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika july 14 2013, zinazoonesha wilaya hiyo kupokea Ths Bilioni 11.1 kwa ajili ya ununuzi wa madawati lakini zikaibwa na wajanja.

Katika kile kinachoaminika kuwa ni ufisadi wa fedha za umma, imeabainika kuwa Halmashauri hiyo mwaka 2012 ilipokea Tsh 11,131,035,000/= kwa ajili ya ununuzi wa madawati kwa shule zote 271 za msingi lakini fedha hizo hazikufika kwenye shule husika.

Nyaraka hizo zinaonesha fedha hizo zilipangiwa matumizi na kuinigizwa ktk akaunti za shule zote husika za NMB Tawi la Geita.

Madiwani hao Peter Donald (kalangalala) Fabian Mahenge (Kasamwa) na Marceline Simbasana (viti maalum) wote kutoka CHADEMA wamesema; Tumepata nyaraka hizi , pesa zililetwa kutoka serikali kuu lakini wamepanga matumizi wakaita walimu wakuu, wakasaini, zikaenda mifukoni mwa wajanja wachache.

Uchunguzi wa mwandishi wa Jamhuri umebaini kwamba hakuna shule yo yote iliyopokea fedha hizo kwenye akaunti ya shule hizo mwaka 2012 kwa ajili ya unununuzi wa madawati kama mgawo unavyoonesha kwenye nyaraka hizo.

Taarifa hizo zinakuja mwezi mmoja baada ya mkuu wa mkoa wa Geita, Magallula Said Magallula kuagiza wananchi wote wachangie fedha kupitia kwa watendaji wa mitaa na vijiji ili kumaliza tatizo la madawati ktkt shule za misingi mkoani humo.

Uchunguzi umebaini pia kuwa, nyaraka hiyo inayoonesha mgawa huo wa Bil 11.1 kwenda akaunti za shule hizo inafanana na akaunti nyingine kwa kila kitu na nyaraka nyingine zilizopo ktk halmashauri hiyo zilizotumika kupanga migawo mbali mabali ya fedha za shule ya msingi/. Tofauti iliyopopo ni kiwanog cha pesa lakini vitu vingi vinafanana.

Hadi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukuta wa jengo la ofisi za idara ya Elimu ya Msingi wilayani Geita, kulikuwa na tangazo linaloonesha mgawa wa fedha kwa shule za msingi ambao umepangwa kwa mfanano ule ule kama nyaraka hii ya Bil 11.1

Chanzo chetu cha habari ktk halmashauri hiyo idara ya uhasibu kimedai; Kuna madudu mengi sana yanafanywa na ni mtandao mrefu unaohusisha watu Fulani wa TAMISEMI, Hazina na viongozi fulani wa ccm, hata wewe angalia yawezekana ukifuatilia hili utapambana na matatizo makubwa sana.

Baadhi ya waalimu wa wakuu wa shule za msingi zilizopo Geita Mjini wameiambia jamhuri kuwa kuna wakati wanaitwa na maafisa na kulazimishwa kusaini fomu za kukiri kupokea fedha kwenye akaunti za shule, lakini fedha hizo huwa haziingizwi kwenye akaunti za shule zetu, wakiuliza, wanaambiwa pesa zimepangiwa kazi nyingine.

Kuna wakati walimu wakuu wote wilaya nzima tuliitwa na kukalazimishwa kusaini fomu fulani za kukiri kupokea fedha za kuendesha shule kwa makubaliano kuwa pesa zitaingizwa kwenye akaunti za shule zetu, lakini hadi leo mwaka unaisha fedha hizo hazijaingizwa, sasa huu kama siyo ufisadi ni wakati tulisha saini kukiri kupokea? Amesemwa mmoja wa walimu hao.

Afisa mipango wa Halmashauri hiyo, ambaye pia ni mkurugenzi wa wilaya hiyo amesema sisi hatukupokea kiasi hicho mwaka 2012 ila tulipokea milioni 11( yaani siyo Bilioni 11)

Alipoulizwa nyaraka ziliandaliwa kwa malengo gani na kuwapo ofisini kwake zinaonesha kupokea Bil 11. 1 za madawati na zinaonesha namba zote za akaunti za shule, idadi ya wanafunzi na kiasi cha pesa kwa kila shule? Mkurugenzi bado alikana akidai mimi nakumbuka mil 11, labda afisa elimu atuambie.

Diwani wa CHADEMA Peter Donald alisema bado ninakusanya ushahidi mwingine wa ufisadi, tatizo ni hata madiwani wenzetu nao wana mtandao mwingine wa ufisadi.

Halmashauri ya Geita ina histori ya kupata hati chafu, na Juni 2013 kuna watendaji walipandishwa kizimbani na Takukuru.

My take;
Je, kitendo cha mkuu wa mkoa kuhamasisha watu kuchangia fedha za madawati ina maanisha kwamba yeye hajui fedha hizo au yeye ni mmoa wa waliogawana?

Ujasiri wa kuwaita walimu wa kuu wote na kuwasainisha nyaraka kama hii ina maana kwamba ufisaidi ndani ya CCM ni wa kimfumo na anayefichwa ni wapinzani na siyo Waziri au TAKUKURU.

Kwa masikitiko mengi sana, naomba kuwasilisha

Big up Deo Balile na Jackton Manyerere..
Source; Gazeti la Jamhuri.

NB; Ukitaka kujua wizi NA ufisadi uliofanyika serikali wakati wa mkutano wa smart partnership soma gazeti hilo. Mamilioni yameteketezwa kifisadi mpaka katibu mkuu kiongozi anataka kuruka kimanga.
 
Mzee Sijaona uhusiano wa ulichoandika na habari iloyoletwa jamvini! M4C haina madiwani wala mkurugenzi wala afisa elimu wala account za shule....! Kwahiyo unataka kutuambia kwamba kama michango ya m4c haiko accounted for basi ni justification kwa halmashauri kufisadi hela ya walipa kodi, tena ya madawati ya shule kwa watoto wetu?
 
Last edited by a moderator:
Watuonyeshe na ufisadi wa pesa za M4C + pesa za ruzuku.

Wewe ni Mburula sana, acha kuwadhihaki Wana wa Geita ambao Wilaya yao imefanywa kama Shamba la Bibi, unajua kama Geita kila Mtendaji wa Serikali anayekuja masikini anaondoka akiwa tajiri? Unaelewa kwamba Madiwani wa CCM Geita ndiyo wenye Tender za Halmashauri za ujenzi na zabuni za manunuzi?

Mfano ni Diwani wa Kata ya Bungw`angoko (CCM) ambaye pia ndiye Meya wa Mji wa Geita anaitwa Kwilasa.
 
ukiona akina njiwa,zemaporomoko, tume ya katiba n.k wanasimama upande wa CCM kwa nguvu zote ndo mujuwe kuwa manufaa yao yoooote ni unyonyaji wa makusudi kama huu wa Geita. wana mirija ya wizi wa kutisha miaka mingi!!
 
Wewe ni Mburula sana, acha kuwadhihaki Wana wa Geita ambao Wilaya yao imefanywa kama Shamba la Bibi, unajua kama Geita kila Mtendaji wa Serikali anayekuja masikini anaondoka akiwa tajiri? Unaelewa kwamba Madiwani wa ccm Geita ndiyo wenye Tender za Halmashauri za ujenzi na zabuni za manunuzi?

Mfano ni Diwani wa Kata ya Bungw`angoko (ccm) ambaye pia ndiye Meya wa Mji wa Geita anaitwa Kwilasa.

Nyamigota hii ni habari nzuri uliyoiweka hapa, hata hivyo, naona umechelewa kutujuza kwamba mkiti wa Halmashauri ndo mzabuni wa Halmashauri yake.
 
Watuonyeshe na ufisadi wa pesa za M4C + pesa za ruzuku.

Duh! Wewe kweli huna uchungu na jasho la walipa kodi. Ushabiki mwingine hauna tofauti na ulevi. Ndugu yangu, hii ni fedha ya serikali inaliwa na wachache na wanafunzi wanakaa chini. Hakika hili jukwaa wakati mwingine wachangiaji wanatia aibu. Wako watu ambao literally are using their toes to think. Yaani wewe umeamua kukifanya kichwa chako pambo. Mlata uzi angesema CCM imetafuna pesa pengine ungeweza ku-argue hivyo. Duh! Shule za saint kayumba zinaabisha.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mzee; Bila shaka ile methali ya kichwa cha kuku hakibebi mzigo inakuhusu!
 
Last edited by a moderator:
Mzee Sijaona uhusiano wa ulichoandika na habari iloyoletwa jamvini! M4C haina madiwani wala mkurugenzi wala afisa elimu wala account za shule....! Kwahiyo unataka kutuambia kwamba kama michango ya m4c haiko accounted for basi ni justification kwa halmashauri kufisadi hela ya walipa kodi, tena ya madawati ya shule kwa watoto wetu?

Mijtu isiyo jielewa yakuachana nayo
 
Last edited by a moderator:
ndo maana akina Ritz @rejeo Mzee.... hawabanduki hapa wanalipwa perdiem kwa ajili ya kutetea ouvu wa ccm.huu ndio mwisho wenu na mtatapika mlivyokula nanina zenu
 
Last edited by a moderator:
Watuonyeshe na ufisadi wa pesa za M4C + pesa za ruzuku.

mzee kam jina lako lilivyo jarib kuhoji kuchangia mada iliyopo ili kuwaondoa manguruwe wote na kama unamashaka na izo pesa za ruzuku na M4C nadhan ukileta thread mpya na vithibitisho itakuwa poa sana, nawasilisha mkuu..
 
Gazeti la jamhuri limeona nyaraka, wewe kama unaushahidi unaohusu M4C siyo vibaya ukatujuza na sisi. Nijuavyo mimi, m4c hakuna wizi.

unayasema hayo kwasababu unataka tuamini hivyo acha unafiki wizi ni wizi kama najua huna courage ya kusema wizi na ufisadi ndani ya CHADEMA wewe ni mmoja wa wale waganga njaa hilo huwezi kulisema hata siku moja!
 
unayasema hayo kwasababu unataka tuamini hivyo acha unafiki wizi ni wizi kama najua huna courage ya kusema wizi na ufisadi ndani ya Chadema wewe ni mmoja wa wale waganga njaa hilo huwezi kulisema hata siku moja!

Waganga njaa mpo lumumba tu
 
Asante sana kwa aliyetuletea uzi huu. Jana kwenye taarifa ya habari ya ITV nilimwona mwenyekiti wa ccm Mkoa wa geita aking'aka sana kuhusu ubadhirifu, kwa kweli sikuelewa chanzo cha habari ile vizuri lakini aliongea mambo yale yale wanayoongea viongozi wa CHADEMA, kwamba watendaji wakiwemo wakurugenzi ndio wanaosababisha CCM na viongozi wake kuzomewa barabarani na wananchi. Kwa kweli Mwigulu Nchemba, Nape, Wasira na Kinana wangelijua hili, CHADEMA isingekuwa na hoja majukwaani na zaidi ya hayo kusingekuwepo na haja ya vyama vingi.
 
Kwenye halmashauri za wilaya kuna ifujaji mwingi sana wa Fedha za miradi na hakuna hatua zinazochuliwa.Kuna mitandao mikubwa ya uwizi ambayo ukojaribu kuifuatilia lazima ukumbane na mabalaa na hata kupoteza maisha katika mazingira ya utata.
Nawapongeza sana madiwani wa chadema kwa ujasiri na wengine waige mfano huo.

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom