Madiwani Chadema Moshi wachachamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani Chadema Moshi wachachamaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by issenye, Jun 2, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,146
  Likes Received: 988
  Trophy Points: 280
  :peace::peace:

  Na Salome Kitomary
  1st June 2011

  [​IMG]
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

  Madiwani 23 wa Manispaa ya Moshi,wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),wamewasilisha maombi Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi wakiomba kuunganishwa katika kesi namba 6 ya mwaka 2011,inayomkabili Mkurugenzi wa Manispaa hiyo dhidi ya viwanja viwili vinavyokaliwa na Chama Cha Mapinduzi.

  Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa Mahakamani hapo na Wadhamini wa (CCM) na Umoja wa Vijana (UVCCM) wakimshtaki Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kwa kushindwa kuwapa hati za viwanja viwili ambavyo wanavikalia kwa sasa.

  Viwanja vyevye mgogoro ni majengo yanayokaliwa na UVCCM Mkoa na ofisi za CCM Moshi mjini.

  Wakili wa madiwani hao, Albert Msando, aliwasilisha maombi hayo mbele ya Msajili wa Mahakama hiyo,Aron Lyamuya ,ambapo katika maombi hayo amedai kuwa walalamikaji hao wamemshtaki Mkurugenzi huyo bila kuwajumuisha madiwani hao ambao ndio wawakilishi wa wananchi.

  Alidai kuwa,mali zinazodaiwa kuwa ni za CCM ni kiwanja namba 54 na 19/2 vilivyopo katika Manispaa hiyo,wakidai kuwa mali hizo na zao kihalali na kumtaka Mkurugenzi kuwapa hati miliki na madiwani hawana maslahi katika mali hizo na wasiingilie na kwamba zilitolewa kwa chama hicho zamani kikiitwa Tanu kwa matumizi ya ofisi tangu Machi 1 mwaka 1976.

  "Tumewasilisha maombi ya kuunganishwa kwenye kesi hii kwa kuwa madiwani ndio wawakilishi wa wananchi waliopewa jukumu la kusimamia na kulinda mali za umma na hivyo tunamaslahi nazo"alidai.

  Wakili Msando alidai kuwa walalamikaji hao kwa kushirikiana na mshtakiwa ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,wamejaribu kuhamisha umiliki wa mali hizo na kuwa katika jina la CCM na hivyo ni wazi kuwa Mkurugenzi huyo hataweza kutetea mali hizo mahakamani.

  Aliwadai kuwa madiwani hao wameona kuwa upo uwezekano wa Mkurugenzi kuridhia mali hizo kumilikishwa kwa chama hicho na hivyo kuona umuhimu wa kuunganishwa katika kesi hii ili waweze kutetema mali za umma zisichukuliwe na kwamba ushiriki wa madiwani katika kesi hiyo utasaidia mahakama kupata ushahidi wa pande zote na kutoa haki.

  Alidai kuwa kwa mujibu wa barua ya Aprili 10 mwaka huu,kwenda kwa Meya wa Manispaa hiyo,Mkurugenzi wa Manispaa,Bernadetta Kinabo inaonyesha kuwa hawezi kutetea mali hizo,kwani alidai kuwa mali hizo zimekuwa zikizungumzwa kwenye vikao mbalimbali vya Halmashauri kuanzia mwaka 1995 na kupitishwa maamuzi mbalimbali.

  CHANZO:
  NIPASHE
   
 2. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Teteeni mali za wananchi kwa nguvu zote tena kwa nguvu,ila msisahau na huyo Mkurugenzi ni fisadi namba moja,haiwezekani mkausahau ule uwanja wa Memorial ambao hivi sasa umegeuzwa soko niwaulizeni nyie madiwani wa CHADEMA mlishiriki katika maamuzi haya?

  Kama ndiyo mjue hakuna dhambi kubwa mliyotufanyia kama hiyo ya kugeuza matumizi tunautaka uwanja wetu uwe wazi tuanzishe timu za mpira wa miguu wakimbiaji na sisi tuingie katika ramani ya michezo siyo kutafuta fedha pekee.

  Hamuoni aibu kudhalilisha michezo kiasi hicho nasikia kuna mpango wa mchungaji fulani wa kanisa la kilokole amepewa ajenge kanisa huko ndani,angalieni sana msituone wajinga iko siku patachimbika hapo Moshi. Pia pale juu ya kanisa la KKKT Moshi mjini sijui ni kitu gani kinajengwa pale kwa miaka mingi sasa mbona wanatufugia wezi wale halafu wamezuia eneo la wazi Puplic area,hivi watu wa Moshi wanapopumzika wanakwenda kuvinjari katika baa za pombe tu?

  Pale kulikuwa na upepo mzuri sana hebu fikirieni pabaki wazi pale siyo kufuata mali chache hizo,labda niwaulize pale stendi katika jengo la mjerumani nasikia ni jengo la wadhamini wa CCM mbona hilo hamfuatilii,ukipita pale huwezi amini eti ile ndiyo katikati ya mji wa moshi ule unaosifika kuwa ukitupa kichungi cha sigara unakamatwa! uchafu na mimoshi mabanda yaliyoezekwa kwa maturubai machafu na mbona hamfuatilii ile chuma ya winchi ya kunyongea inaonekana historia mbaya ya wazee wetu kunyongewa pale.

  Lakini sasa mbona hakuna usafi pale CCM wanalea uchafu?hivi hamuoni hayo mazingira yalivyo machafu yanaharibu kabisa mandhari ya mji,lakini CCM wanatafuta nini8 pale kwanini msiwatimue hivi lile jengo ni lao,hiyo CCM ilikuwepo enzi za mjerumani? na mjerumani alipoondoka akawarithisha.

  Kwa ujumla Manispaa ya Moshi inaendeshwa sivyo kabisa na nawaasa nyie madiwani wa Moshi muwe wa CHADEMA au wa CCM ZINDUKA MTETEE MJI WA MOSHI KABLA HAUJAANGUKA iko siku tutaachiwa magofu,hakuna watendaji wenye uchungu na mji mambo yanayofanyika Moshi naweza kusema kwa asilimia100(100%) hayawezi kufanyika katika miji ya Mwanza,Morogoro,Daresalaam hata Ujiji Kigoma na mingineyo :frusty::frusty:haiwezekani,
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Homosapien
  Sijakaa Moshi kwa muda sasa tangu 2000, nasikia soko la Kiborloni lilihamishiwa Memorial ni kwenye ule uwanja wa michezo au ni lile neo la wazi chini ya Shule ya Msingi Karanga? Nachelea kuamini kama soko limehamishiwa ndani ya uwanja wa michezo kwani endapo ikitokea sikukuu ya kitaifa ikafanyika Moshi sijui watakodisha uwanja wa Chuo cha Ushirika au wapi?

  Pili umeeleza mengi yanayohitaji kufuatiliwa, labda wewe muda mwingi uko Moshi, Hivi ile Shule ya Sekondari pale uwanja wa Mashujaa haikujengwa kwenye eneo la wazi?
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  VA ulichosikia ni sahihi kabisa, soko la Kiborloni limehamishiwa ndani ya Memorial ila lipo ule upande usio wa uwanja wa michezo (na jukwaa pia). Ingawa bado kuna eneo la kutosha tu limebaki pale, siku hizi ukiacha mikutano ya Injili sikukuu za kitaifa, kimkoa na nyinginezo (kama Kili Marathoni) zinafanyikia MUCCoBS. Sekondari iliyopo uwanja wa Mashujaa ni ipi hiyo? Labda unazungumzia Muungano, ile pale nyuma ya RC office?
   
 5. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Uwanja wa Mashujaa shule iliyopo jirani ni Northern Highland Sekondari.
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,453
  Likes Received: 12,710
  Trophy Points: 280
  Sure sure!
   
Loading...