Madiwani Buchosa wakubali kuhamia Geita ili kutoa fursa kuanzishwa mkoa mpya wa Chato

Ukitumia barabara, Buchosa kwenda Mwanza ni mbali kuliko Buchosa kwenda Geita. Kumbuka kutoka Buchosa kwenda Geita haupiti Sengerema bali kuna njia ya mkato kwenda Geita kupitia Kamhanga.
Hiyo njia ya Kamhanga inapitika? Kuna usafiri wa uhakika? Kwa sababu wote wanaotoka Buchosa kwenda Geita hupitia Sengerema tu. Huko unakosema ni njia zisizopitika
 
Kutoka kikunde - kilindi hadi Tanga Mjini zilipo ofisi za RC ni zaidi 350km alafu mnatuletea habari za 100km wapuuzi kabisa nyinyi
Bure kabisa, tunaongelea Buchosa wewe unaleta habari za Kilindi. Fungua uzi wako wa Kilindi.
 
Eneo la Chato unalijua? Au unafikiri ni kaeneo kadogo kama Tandale?
Wameaminishwa na wanasiasa wa twitter kwamba Chato ni kijiji hawajui mkoa mpya wa Chato utakuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni moja na nusu kutoka kwenye wilaya za Chato, Ngara, Biharamulo, Kakonko na Bukombe. Hii ni idadi kubwa sana ya watu inatakiwa huduma za kijamii ziwe karibu ndiyo maana mkoa mpya unapendekezwa.
 
Inapitika kaka. Na wakishahamia huko inaimarishwa zaidi maana huwa inakutana na barabara inayotoka Nzera kwenda Geita
Hiyo njia ya Kamhanga inapitika? Kuna usafiri wa uhakika? Kwa sababu wote wanaotoka Buchosa kwenda Geita hupitia Sengerema tu. Huko unakosema ni njia zisizopitika
 
Kikao cha dharula cha madiwani wa halimashauri ya Buchosa kimekubali kumegwa na kuhamia mkoa wa Geita ili kutoa fursa kwa mkoa mpya wa Chato kuanzishwa haraka iwezekanavyo.
===

Madiwani wa halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza wameridhia kuhamia Mkoa wa Geita kwa sharti la halmashauri hiyo kupandishwa hadhi kuwa wilaya sambamba na kuongezwa tarafa, kata na vijiji.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuitishwa baraza maalumu la madiwani la halmashauri hiyo kwa lengo la kujadili agenda ya maombi ya kuanzishwa nkoa mpya wa Chato kwa kumegwa jimbo la Buchosa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Buchosa, Paul Malala ametaja faida za kuhamia Mkoa wa Geita kuwa ni pamoja na kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi sambamba na kupunguza umbali kutoka Buchosa hadi Mwanza (kilomita 10) huku kwenda Geita ni kilomita 58, itasaidia huduma za wananchi kupatikana kwa urahisi.

Malala ametaja faida nyingine halmashauri hiyo itapata fursa ya kuwa wilaya itaongeza huduma za kijamii kama mahakama, kituo cha polisi, Magereza ,ofisi ya mkuu wa wilaya Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma nyingi za kijamii ambazo hazikuwepo hapo awali katika eneo hilo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema, Barnabas Nyerembe amepongeza hatua ya baraza maalumu la madiwani kukubali kwa kauli moja halmashauri ya Buchosa kuhamia Mkoa wa Geita kwa sharti la kuwa wilaya yenye mamlaka kamili.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa, Idama Kibanzi amesema maoni ya kamati ya fedha utawala na mipango baada ya kujadili faida na athari za halmashauri kuhamia Geita Ili kuwezesha kuanzishwa mkoa mpya wa Chato iliridhia kumegwa kwa jimbo la Buchosa kuwa sehemu ya Mkoa wa Geita endapo halmashauri hiyo itapewa hadhi ya kuwa wilaya yenye mamlaka kamili.

Diwani wa kata ya Bupandwa, Masumbuko Bupamba na Dotto Bulunda (Kafunzo) waliunga mkono hoja kwa kuridhia kuhamia Mkoa wa Geita.

Wameseme hata awali Buchosa na Sengerema zilimegwa kutoa Geita hivyo hawaoni tatizo lolote juu ya halmashauri hiyo kuhamia Mkoa wa Geita ila inatakiwa kupewa mamlaka kamili kama Wilaya.

MWANANCHI

Tafuteni uwekezaji wa kibiashara badala ya kusubiri huruma na upendeleo. Mambo ya upendeleo ni ya muda kama sasa tumeona Hayati hayupo tena. Chato haina vigezo vyovyote vya kuwa mkoa. Kama Chato itakuwa mkoa basi kila sehemu watataka kuanzisha mikoa mingine.

Mfano mkoa wa Tanga ni mkubwa sana kutoka bararini mpaka Kilimanjaro ungetakiwa kuwa mikoa miwili mwingine uwe pale koregwe, mombo na lushoto
 
Hao Tanga wamepeleka mapendekezo serikalini wakakataliwa ? Au unalopoka tu ?
Tafuteni uwekezaji wa kibiashara badala ya kusubiri huruma na upendeleo. Mambo ya upendeleo ni ya muda kama sasa tumeona Hayati hayupo tena. Chato haina vigezo vyovyote vya kuwa mkoa. Kama Chato itakuwa mkoa basi kila sehemu watataka kuanzisha mikoa mingine.

Mfano mkoa wa Tanga ni mkubwa sana kutoka bararini mpaka Kilimanjaro ungetakiwa kuwa mikoa miwili mwingine uwe pale koregwe, mombo na lushoto
 
SHIDA YAKO KUBWA NINI ACHA CHUKI KIONGOZI LAZIMA TUMUKUMBUKE KIONGOZI WETU MAANA AMEFANYA TUWE HIVYO

MAANA NCHI HII ALICHOFANYA MAKUBWA NYIE MULIO INULIWA NA KIKWETE SHIDA YENU MUNABEZA KILA KITU CHA JEMEDARI KWANI ANNA TIBAIJUKA NINA KWAKO WEWE
Tukimaliza Butiama na Lupaso ziwe mikoa pia.
 
Kwanini serikali inawaonea aibu waaambie ukweli hakuna Mkoa wa chato hapa utakaotokea.
 
Bure kabisa, tunaongelea Buchosa wewe unaleta habari za Kilindi. Fungua uzi wako wa Kilindi.
sijawahi kuona ukabila mkubwa katika nchi hii kama ulioonyeshwa na wasukuma wakati na baada ya utawala wa magufuli
 
Kikao cha dharula cha madiwani wa halimashauri ya Buchosa kimekubali kumegwa na kuhamia mkoa wa Geita ili kutoa fursa kwa mkoa mpya wa Chato kuanzishwa haraka iwezekanavyo.
===

Madiwani wa halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza wameridhia kuhamia Mkoa wa Geita kwa sharti la halmashauri hiyo kupandishwa hadhi kuwa wilaya sambamba na kuongezwa tarafa, kata na vijiji.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuitishwa baraza maalumu la madiwani la halmashauri hiyo kwa lengo la kujadili agenda ya maombi ya kuanzishwa nkoa mpya wa Chato kwa kumegwa jimbo la Buchosa.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Buchosa, Paul Malala ametaja faida za kuhamia Mkoa wa Geita kuwa ni pamoja na kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi sambamba na kupunguza umbali kutoka Buchosa hadi Mwanza (kilomita 10) huku kwenda Geita ni kilomita 58, itasaidia huduma za wananchi kupatikana kwa urahisi.

Malala ametaja faida nyingine halmashauri hiyo itapata fursa ya kuwa wilaya itaongeza huduma za kijamii kama mahakama, kituo cha polisi, Magereza ,ofisi ya mkuu wa wilaya Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma nyingi za kijamii ambazo hazikuwepo hapo awali katika eneo hilo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Sengerema, Barnabas Nyerembe amepongeza hatua ya baraza maalumu la madiwani kukubali kwa kauli moja halmashauri ya Buchosa kuhamia Mkoa wa Geita kwa sharti la kuwa wilaya yenye mamlaka kamili.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa, Idama Kibanzi amesema maoni ya kamati ya fedha utawala na mipango baada ya kujadili faida na athari za halmashauri kuhamia Geita Ili kuwezesha kuanzishwa mkoa mpya wa Chato iliridhia kumegwa kwa jimbo la Buchosa kuwa sehemu ya Mkoa wa Geita endapo halmashauri hiyo itapewa hadhi ya kuwa wilaya yenye mamlaka kamili.

Diwani wa kata ya Bupandwa, Masumbuko Bupamba na Dotto Bulunda (Kafunzo) waliunga mkono hoja kwa kuridhia kuhamia Mkoa wa Geita.

Wameseme hata awali Buchosa na Sengerema zilimegwa kutoa Geita hivyo hawaoni tatizo lolote juu ya halmashauri hiyo kuhamia Mkoa wa Geita ila inatakiwa kupewa mamlaka kamili kama Wilaya.

MWANANCHI
Wapeleke huko upuuzi wao. Mkoa wa chato ili umfaidishe nani? Watu wanawaza kubuni nafasi za vyeo badala ya namna ya kuleta maendeleo kwa watu. Nchi hii kama ni kuanzisha mae eo mapya ya utawala chato haipo kabisa kwenye kipao mbele.
 
Wameaminishwa na wanasiasa wa twitter kwamba Chato ni kijiji hawajui mkoa mpya wa Chato utakuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni moja na nusu kutoka kwenye wilaya za Chato, Ngara, Biharamulo, Kakonko na Bukombe. Hii ni idadi kubwa sana ya watu inatakiwa huduma za kijamii ziwe karibu ndiyo maana mkoa mpya unapendekezwa.
Yaani ni kama mliingiwa na pepo au kaulevi fulani!!. Ubinafi wa kiwango cha lami..
 
Back
Top Bottom