Madiwani 10 wa CCM na UDP wajiunga na CHADEMA

Wakati zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za ubunge na udiwani kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka huu likiwa limepamba moto katika vyama mbalimbali vya siasa hapa nchini,waliokuwa madiwani wapatao 10 kutoka katika vyama vya CCM na UDP wilayani Bariadi mkoani simiyu wamevihama vyao vyao na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.

Wametangaza uamuzi wa kuvihama vyama vyao katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika kijiji cha Dutwa.

Katibu mwenezi wa chama hicho wilaya ya Bariadi, Martin Moga amesema kujiunga kwa madiwani hao kutakiongezea nguvu chama hicho hasa ukizingatia kwamba sasa hivi wanaelekea katika uchaguzi mkuu.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho Wilson Mshuda amesema chama hicho kimechukizwa na mbinu chafu zilizofanywa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Andrea Chenge la kuzuia jimbo hilo lisikatwe wakati kuna wilaya hapa nchini zina wakazi wachache majimbo yao yamekatwa na kwamba kufanya hivyo ni kuwanyima wananchi kupata huduma za msingi huku mwenyekiti wa baraza la vijana mkoa huo mark malulu akiwataka vijana wa mkoa huo kutojenga uoga katika kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

naona umeweka jamvin ukiwa na haraka wakati issue yenyewe siyo ya leo hujataja hata majina yao lakin pia hao madiwan hawafiki kumi
 
hao walishajua watakatwa kama lowasa wameamua kukimbia mapema kuepuka aibu
 
Wanatanga tanaga tu hao wanasiasa wenu,,,,tufanyekazi tubadili maisha maana hao noa wako kazini kubadili maisha yao ndo maana wanahamahama kusaka uongozi ndani ya vyama kama taasisi za Ajira
 
Wanatangatanga tu hao kutafuta maisha , tufanye kazi tubadili mfumo wa maisha yetu na familia zetu kuliko kuamini katka hawa wanasiasa kwa 100% . maana hao nao wanatafuta maisha mazuri kupitia taasisi za kisiasa kwa kutaka nafasi za juu za uongozi ili wapige hela. that why wanasema wamechoshwa na uongozi wa vyama fulani. Mfano ni WENJE,aliyenifundisha thaqaafa si yule wa leo ambaye amehama na mwanza na maisha yake yako dar na biashara zake zote anafanyia huko..mwanza anakuja kuwazunga tu eti mtoto wa mama ntilie , huyo mama yake anauzia wapi hicho chakula?
 
Huko ndio kukuwa kwa uhuru wa siasa nchini lakini mimi nashangaa wakiama wa CCM kwenda vyama vingine vya siasa inakuwa poa tu yani doho tabu lakini wakiama wa vyama vingine especially wa chadema unaitwa usariti au inakuwa ni bifu lakini em samahani nisaidieni maana ya neno msariti?

"Msariti" halipo popote, wewe umelipata wapi dogo?? Labda kama ni la kilugha, lakin sio kiswahili!!
 
Ila Pamoja na Kuvuna Wanachama kutoka CCM na UDP mie bado nina mashaka na dhamira ya ndugu Yangu Seni silanga mtia ni ya Ubunge kwa tiketi ya Chadema maana ni kaka yake mtia nia wa ccm Njalu Silanga,Seni toka kuanze vyama vingi kishakuwa diwani wa UDP,akawa Diwani wa ccm,then Akahamia NCCR now yupo chadema duu
 
Masikini yule Mzee kuwadi wa magamba washamkata sehemu nyeti,amekwisha!
 
Karibuni tukomboe nchi kutoka kwenye makucha ya unyanyasaji na dhulma!
 
Hongera mzee mkapa najua rohoni ulikuwa unafurahii tu kijana wako anavyopenya kwenye mawimbi ya rushwaa, visasi na vyeo ila alikuwa anaitwa askari wa mwamvuli wakt wako na nina imani ulikuwa haujawahi kumfukuza kwa simu hata maramoja ila kijana wako wako mulize ndani ya miaka 10 hii ya uongozi wake amefukuzwa Mara ngapi kwa simu na usishangae atakuambia na alishakuambia naamini kuwa inaqeza hata kuwa alikuwa anafukuzwa Mara 4 ndani ya mwezi sasa urfk wake na huyu kaka unatoka wapi hata bodyguard aliongolewa acha kabisa SIASA TAMU
 
Back
Top Bottom