Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,431
- 73,078
Sijasema nani ni dikteta ila napenda tujiulize hao madikteta wanazaliwaje (sio biological) na wanakufaje (wanavyoishia).
Mwaka 1971 Idd Amin alipo mpindua Obote utawala wake uliookelewa kwa shangwe na matumaini makubwa. Alipoamua kuwanyanganya waasia mali zao na kuwafukuza wananchi wakawa na matumaini makubwa kwake hivyo kila alilosema likaonekana kina nia njema kwa nchi yake.
Lakini Amin alikosa vision ya mwekekeo wa kiuchumi wa kuinua nchi na nchi ikaanza kuporomoka. Wanasiasa walipoanza kulisemea hilo akaona litampunguzia unaarufu, akawakamata na kuwafunga mwisho akaona isiwe tabu akaanza kuwaua. Hapo ndio Udijteta wake ukipozaliwa. Viongozi wa dini walipoona hayo wakakemea nao wakapandishwa vyeo kuwa marehemu.
Nchi ikagwaya, wataalamu na wanaharakati wakosoaji eitha wakanyamaza, wakakimbia nchi na waliojifanya mdomo unawasha yakawakuta makubwa. Maisha yakawa magumu, uchumi uka angamia kabisa na nachafuko juu. Ikawa hakuna njia nyingine zaidi ya kumtoa Amin kwa nguvu na hicho ndio kikawa kifo chake katika utawala.
Alijifia kwa aibu akiwa mafichoni Saudia. Ingekuwa ni zama hizi basi angeenda kuibuliwa huko Saudia na angefia jela.
Nani anachangia kuzaliwa na kufa kwa madikteta? Obviously ni wananchi wenyewe kugawanyika katika kusifu na kukosoa mienendo ya utawala wa binadamu huyo.
Sauti za kusifia zikiwa na nguvu na kuonekana zile za kukosoa zinatenda dhambi kuna jenga tabia ya huyo binadamu kuchukia ukosoaji.
Sasa kimbembe kitakuja pale hata wale wasifiaji watakapo anza kupungua kutokana binadamu huyo kushindwa kutumia ushauri mbadala na hali ya uchumi kuwa mbaya.
Ili ku maintain stutas binadamu huyo huanza kutumia njia mbalimbali kuzuia idadi ya wakosoaji kuongezeka na ndio MWISHO MBAYA humtokea mfano wa huyo Amin aliye ingia kwa shangwe na madikteta wengine.
Wananchi wanawezaje kujizuia kuzalisha hao madikteta? Nazungunzia hasa hapa Afrika.