Ripoti: Mustakabali wa Madikteta unazidi kufifua kutokana na Watu kudai Demokrasia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mustakabali wa madikteta unazidi kufifia hata hivyo viongozi wa kidemokrasia wanapaswa kuchukua hatua bora zaidi ili kuzikabili changamoto za dunia amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kutetea Haki za Binadamu, HRW.

Mkurugenzi huyo amesema katika ripoti ya mwaka huu wa 2022 kwamba watu katika nchi zinazotawaliwa na madikteta wameendesha harakati za kuwania demokrasia kuanzia Cuba hadi Hong Kong.

Amesema watu wamejitokeza mabarabarani kudai demokrasia hata katika hatari ya kutiwa ndani au kupigwa risasi.

Roth ameongeza kusema kwa vile madikteta hawawezi tena kutegemea chaguzi zinazoendeshwa kwa hila ili kudumisha mamlaka yao, wengi wao sasa wanatumia njama dhahiri ambazo zinahakikisha matokeo wanayotaka lakini matokeo hayo hayatoi uhalali wa uchaguzi.

Bwana Kenneth Roth amesema madikteta wanaweka mbele maslahi yao binafsi kabla yale ya wananchi wao. Hata hivyo ameshauri kwamba viongozi wa nchi za kidemokrasia wanapaswa kutekeleza sera bora zaidi ili kuzikabili changamoto za dunia. Ameeleza kwamba viongozi wengi kwenye nchi za kidemokrasia wametingwa na maslahi ya muda mfupi kwa ajili ya kujipatia mitaji ya kisiasa badala ya kuweka mkazo juu ya maswala muhimu, kama vile ya mabadiliko ya tabia nchi, janga la maambukizi ya virusi vya corona, ubaguzi wa rangi na umasikini. Amewataka viongozi waliochaguliwa kwa njia halali kufanya kazi nzuri ili kuyashughulikia masuala hayo.

Katika dibaji ya ripoti ya mwaka huu ya asasi hiyo ya haki za binadamu mkurugenzi, Kenneth Roth ameyapinga maoni kwamba nchi za madikteta zinastawi wakati zile za kidemokrasia zinafifia. Amesema madikteta wengi wanadai kwamba wanawatumukia watu wao vizuri kuliko viongozi waliochaguliwa kwa njia za kidemokrasia.
 
Demokrasia ina gharama sana kwa raia wenye elimu ndogo, ... kwa mfano hili la kutoa elimu, HAFIFU, bure, kwa kisingizio cha kuwajali wanyonge linafanya wizara ya elimu isibebeke na kutoa huduma chini ya kiwango sana!
TATIZO NI KUFANYA KILA KERO YA WANANCHI MTAJI WA KISIASA!
NB: INABIDI TUME, HURU, YA UCHAGUZI IZIPITIE AJENDA ZA WAGOMBEA NA KUWAWEKEA MIPAKA YA 'UONGO' WAO, KAMA INAWEZEKANA!
 
CCM serikali ya kidikteta
Ccm si wema ni laana ya nchi!iv askari wanafaidika nini kutumikishwa na wakuu wao kulaghai haki zao ambazo wenyew zinawahusu!mfano uwizi wa kura ,unaluta igp anawatumqa waibe kura kwa manufaa yake igp ,hao askari wanaotumwa wanafaidika vip mfano anawazuia wasitoe Siri za rushwa hao wanafaidika nini?da
 
Back
Top Bottom