Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,247
- 33,765
Wadadisi wengi wa masuala ya kiimani wanaelezea namna ambavyo HATIMA ya kila safari ya maisha kwa kiumbe binadamu. Maandiko Matakatifu yanaelekeza kuwa moto ni hitimisho pia adhabu kwa kila anayekiuka kwa makusudi au bahati mbaya maagizo ya Mola.
Hapa duniani tunaelewa namna moto unavyoteketeza na kuharibu kitu chochote unachokipitia. Tumeona nyumba zinapoungua na bila juhudi za kudhibiti moto usiendee huleta madhara makubwa na hatima yake ni jengo kuteketea lote bila huruma.
Wananchi wengi wanaojitwalia sheria mkononi dhidi ya vibaka, huwa wanahitimisha shughuli yao kwa kumchoma moto mwivi ili kuhakikisha hawi hai tena.
Lakini moto pia, ni ubatizo wa kubadilisha hali moja kwenda nyingine. Dhahabu husafishwa kwa moto ili kuifanya bidhaa mpya yenye thamani. Ukilinganisha mfano huu ni wazi Samia ameonesha kwa vitendo HATAKI kukosolewa kwa sababu amewashughulikia wakosoaji wake kwa kuwapoteza, kuwafungulia kesi ama kuwaua kama ilivyofanyika kwa marehemu Ally Kibao na wengine.
Kitendo cha BAWACHA kuamua kuchoma moto vitenge walibyozawadia na Samia alipohutubia Baraza kuu la Wanawake wa CHADEMA ni dalili mbaya sana kwake. BAWACHA walifafanua sababu za kuteketeza vitenge hivyo na kuwataka wanawake nchi nzima kuchoma vitenge vyenye taswira ya Samia.
Tumeona namna Samia alivyomshughulikia kijana Shadrack Chaula aliyechora picha yake na kuamua kuichoma. Alieleza sababu za kuchoma picha hiyo lakini Samia kupitia jeshi la polisi walimkamata na akaamuru afungwe ambapo wananchi walichanga fedha ya kumlipia faini. Kitendo cha wanasheria wa Chaula kusajili rufani ya adhabu aliyopewa Chaula, kijana alikwapuliwa na maafisa waliojitambulisha ni polisi na mpaka leo hajapatikana. Lengo la passage hii ni kuonesha laana inayogubikwa na moto. Tangu picha ichomwe na Chaula tumeona mambo mengi yamebadilika kwenye safari ya kisiasa ya Samia ikiwemo kuporomoka kwa umaarufu na kukubalika kwake kwenye jamii.
Tunaona humu, machawa na waungaji mkono wa utawala huu dhalimu wakigeuka vituko kwa kuanzisha mada zisizo na kichwa wala miguu huku.
BAWACHA wametia dosari kubwa kwenye safari ya kisiasa ya Samia. Kukubalika kwake ndani ya CCM kumeporomoka kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba chawa wake Lucas Mwashambwa badala ya kububujikwa machozi ya furaha, sasa amekuwa akiomboleza na kusaga meno.