Madhehebu yanachangia umasikini Afrika

Madhehebu yanachangia umasikini Afrika

NJALI

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
1,534
Reaction score
1,092
Kuabudu ni jambo la heri sana, Maana linakuunganisha na Mola wako au Allah, Jaa n.k.

Pia mtu anaemjua Mungu kupitia ibada, huwa mstaarabu, mwenye hekima. Ki ufupi hana MAKUU.

Pia dini inapunguza magonvi, uzinzi, ulevi na watoto wasiyo na makazi.

Pia taifa la watu wenye dini walioshika sana ibaada linatawarika kirahisi Kwani washika dini wanamioyo iliyopondeka, kupitia mafundisho yao ya MTU akikupiga kofi shavu la kushoto mtegee na la kulia.

HOJA
Licha ya manufaa KADHAA niliyo yataja, ngoja tutizame jinsi gani dini ina uhusiano na kustawi kwa ufukara Africa.

1.Michango imekuwa mingi sana makanisani, misikitini sijui Kwani huwa siendi. Utakuta siku ya saba ya Juma waumini wanapangiwa vikapu Kama vitano vikihitaji waumini kutoa michango Kila kikapu.

Mfano, kuchangia safari ya wainjisti kwenda mkoa X

Kuchangia pesa ya umeme WA kanisa na nyumba ya baba MCHUNGAJI n.k

2.Siku za kusali zimekuwa nyingi sana
Mfano Jumapili ni siku ya Ibaada kuu. Juma tano utakuta waumini wanaambiwa waende kanisani kuombea yatima, wagonjwa, wajane, tasa, wagane.

Ijumaa kwenda pia kwenye maombi, na maombezi
Jumanne kwenda kwenye kwaya kufanya mazoezi ya kuimba.

Alhamis kuhudhuria mikusanyiko ya kuwatembelea watu mbali mbali hasa wapendwa wenye matatizo anwai.

3.Baadhi ya dini zinawaaminisha waumini wao kuwa. utajiri ni dhambi. Wakinukuu kile kifungu kuwa "Ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye Tundu la sindano kuliko Tajiri kuingia ufalme wa mbinguni".

Baadhi ya mambo niliyo yataja Hapo juu yana uhusiano na umasikini Kwani waumini wanatoa kuliko kipato chao. Wanakosa muda wa kutosha kufanya kazi, Mfano wengine Siku nzima ya Juma mosi hawafanyi kazi yoyote.

Japo imani inanguvu sana kwa wanadamu hembu tuangalie waliotuletea hizi dini na wao wanasali kama sisi muda WOTE? Vijana wanashindia kanisani almost five days per week? China wakoje? UK vipi?, Ujerumani vipi?, Ufaransa vipi?
 
Kiasi fulani kuna kaukweli hasa kwenye Makanisa binafsi, lakini angalia usijekuwa una-kapepo ka kutopenda kutoa sadaka.
 
Mimi nilishaacha kwenda kanisani zaidi ya miaka 15 nafuata dini ya asili ya mwafrika ya mila na desturi. Ukiweza nawe utakuwa huru
 
Baadhi ya mambo niliyo yataja Hapo juu yana uhusiano na umasikini Kwani waumini wanatoa kuliko kipato chao. Wanakosa muda wa kutosha kufanya kazi, Mfano wengine Siku nzima ya Juma mosi hawafanyi kazi yoyote.

Mkuu kama kweli waumini wanatoa kuliko kipato chao....nadhani basi watakuwa wamelimbikiza madeni kibao nyuma yao na hawatokuwa matajiri kamwe.....Utajiri ni heshima!.
 
Bora uliyotaja, mimi kinachonikera hua ni ujinga uliowajaa kichwani, kila kitu wao utasikia tumuachie Mungu, hawataki hata kujituma kutafuta solution, najua sio wote ila wananifanya hadi nione aibu kusema na mimi nina dini.

Mfano kuna picha imefanyiwa editing mtandaoni maji kama uso wa yule jamaa aliyeact movie ya Yesu, watu tayari wanaanza mara ohh siku za mwisho zimefika dalili zimeanza kuonekana, wengine wanasema aliyeedit ile picha kaingiliwa na roho sijui wa wapi, theory kibao za kipuuzi tu. Ukiingia deep kwenye haya mambo bila kuchanganya na zako unageuka zezeta.
 
Mpaka maombezi yanalipiwa siku hizi.

Unapanga mstari kwenda kuombewa, pembeni ya mstari kuna kikapu cha gharama ya maombi.

Habari ya pesa weka mbali kabisa.
 
Na sasa wanauza:
Mafuta.
Chumvi.
Maji.
Vitambaa.
Bangili.

Vyote hivyo ni upako.
 
MAKANISA NI BIASHARA KUBWA....

OVAA
 
zamani makanisa ilikuwa kimbilio la maskini lakini sasa makanisa ni kimbilio la wenye nacho utakuta mtu anayetoa mchango mkubwa anapewa kipaumbele sana wanasahau kuhusu Bwana Yesu alipokuwa akiwaeleza wanafunzi wake juu ya sadaka ya mwanamke maskini.Michango na mahubiri mengi ni juu ya michango na sadaka ndio maana idadi ya waumini inapungua siku hadi siku
 
Mbaya zaidi ni kuwa waumini hawa maskini ndiyo chanzo cha sadaka zinazowafanya wachungaji wao waishi maisha ya 'peponi'.
 
Nilikaa chini nikatafakari weeeeeeeeeeeeeeeee nikaona hakuna tofauti ya makanisa ya kiroho na Uganga Wa jadi
 
Kuabudu ni jambo la heri sana, Maana linakuunganisha na Mola wako au Allah, Jaa n.k.

Pia mtu anaemjua Mungu kupitia ibada, huwa mstaarabu, mwenye hekima. Ki ufupi hana MAKUU.

Pia dini inapunguza magonvi, uzinzi, ulevi na watoto wasiyo na makazi.

Pia taifa la watu wenye dini walioshika sana ibaada linatawarika kirahisi Kwani washika dini wanamioyo iliyopondeka, kupitia mafundisho yao ya MTU akikupiga kofi shavu la kushoto mtegee na la kulia.

HOJA
Licha ya manufaa KADHAA niliyo yataja, ngoja tutizame jinsi gani dini ina uhusiano na kustawi kwa ufukara Africa.

1.Michango imekuwa mingi sana makanisani, misikitini sijui Kwani huwa siendi. Utakuta siku ya saba ya Juma waumini wanapangiwa vikapu Kama vitano vikihitaji waumini kutoa michango Kila kikapu.

Mfano, kuchangia safari ya wainjisti kwenda mkoa X

Kuchangia pesa ya umeme WA kanisa na nyumba ya baba MCHUNGAJI n.k

2.Siku za kusali zimekuwa nyingi sana
Mfano Jumapili ni siku ya Ibaada kuu. Juma tano utakuta waumini wanaambiwa waende kanisani kuombea yatima, wagonjwa, wajane, tasa, wagane.

Ijumaa kwenda pia kwenye maombi, na maombezi
Jumanne kwenda kwenye kwaya kufanya mazoezi ya kuimba.

Alhamis kuhudhuria mikusanyiko ya kuwatembelea watu mbali mbali hasa wapendwa wenye matatizo anwai.

3.Baadhi ya dini zinawaaminisha waumini wao kuwa. utajiri ni dhambi. Wakinukuu kile kifungu kuwa "Ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye Tundu la sindano kuliko Tajiri kuingia ufalme wa mbinguni".

Baadhi ya mambo niliyo yataja Hapo juu yana uhusiano na umasikini Kwani waumini wanatoa kuliko kipato chao. Wanakosa muda wa kutosha kufanya kazi, Mfano wengine Siku nzima ya Juma mosi hawafanyi kazi yoyote.

Japo imani inanguvu sana kwa wanadamu hembu tuangalie waliotuletea hizi dini na wao wanasali kama sisi muda WOTE? Vijana wanashindia kanisani almost five days per week? China wakoje? UK vipi?, Ujerumani vipi?, Ufaransa vipi?

Sidhani kama uko sahihi. Kwanza utoaji si kanisani au msikitini tu; hata utoaji mitaani, kwa mayatima, kwa wajane pia ni utoaji.

Nitaongelea upande wangu katika imani ya kikristo.

Angalia sehemu zenye maendeleo makubwa nchini ni zile ambazo kanisa liliingia zamani - Kilimanjaro, Arusha, Rungwe, Kagera n.k. Na maeneo hayohayo yanasifika kwa utoaji makanisani (kama Arusha na Kilimanjaro). Kanisa lilileta dini na elimu na pia ajira - ni maendeleo. Vyote hivyo viko connected na utoaji.

Lakini pia hebu fikiria, miaka hiyo kabla makanisa na misikiti haijaingia Afrika, kulikuwa na kitu gani? Miji gani iliyostaarabika? Barabara za lami? Unadhani kanisa (na misikiti) lisingeingia leo kungekuwa na hali gani leo?

Hivi unaweza nitajia sehemu, au mtu binafsi asiye mtoaji ambaye kafanikiwa? Kama nilivyosema utoaji si kanisani au msikitini tu, hebu fikiria kuna watu kama Bill Gates wanajitoa hadi basi na Mungu anazidi kuwabarikia.

Kusanya pesa zako na usitoe hata senti uone kama utabarikiwa.
 
Back
Top Bottom