Madhara yaletwayo na Michepuko ktk ndoa

Madhara yaletwayo na Michepuko ktk ndoa

Satuuuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2015
Posts
1,849
Reaction score
1,994
Mume alirejea nyumbani na kukuta ujumbe juu ya meza umeandikwa "NIMEONDOKA" ilikuwa jioni, alienda jikoni na kukuta kukavu, aliwaita watoto na kuwauliza wakasema walimuona Mama akiondoka na begi lakini hakuwaambia anaenda wapi. Mume alichanganyikiwa, alijaribu kuchukua simu kumpigia lakini ilikuwa haipatikani, kabla hajafanya chochote mtoto wao wa mwaka mmoja alikuja akilia na kusema ana njaaa.

Ilibidi kuingia jikono na kutaka kupika huku akitukana matusi yote, kila kitu kilikuwa hakuna, hapo ndipo alipokumbuka kua asubuhi mkewe alimuomba pesa ya kununua chakula akamuambia hana afanye maarifa. "Ataondokaje ghafla namna hii, huyu mwanamke mshenzi kabisa.." Aliwaza lakini alikumbuka kuwa asubuhi hiyo hiyo baada ya kumnyima mkewe pesa ya chakula mke alilalamika kua amechoka maisha yale na yeye akamjibu "Kama umkechoka si uondoke, wanawake wako wengi ukiondoa kitu na weka kitu..."

Akili yake iliwaza sana akakumbuka mchepuko wake, aliupigia simu uje nyumbani, lakini ulistuka kuhusu Mama watoto, akamuambia ameondoka na kamuachia watoto wote wa nne. Mchepuko ulijifanya hausikii vizuri na baada ya muda ukazima simu. Sasa alikuwa amechanganyikiwa, alitaka kupiga simu Kijijini ndipo alikumbuka kuwa hata namba ya Mama mkwe wake alikuwa hana, hakuwa na kawaida ya kuongea nao na mara chache alipoongea ni pale ambapo mkewe alipiga simu na kumuambia kuwa aongea na familia.

Alikumbuka ana namba ya rafiki wa mke wake, akampigia kumuuliza mkewe yuko wapi akasema hajui lakini mara ya mwisho alipompigia alimuambia kuwa "ANAENDA KUPUMZIKA". Alizidi tena kutukana, alitoka jikoni nakuwachukua watoto kwenda kwenye mgahawa alizunguka nao mpaka kupata sehmu ya kula, watoto walifurahi sana siku hiyo kutoka na Baba yao, waliongea na kucheka kula nnje ya nyumbani, kidogo alipata faraja na kutabasmau lakini bado alikuwa akiwaza kuhusu mkewe.

Baada ya kumaliza chakula aliwarudisha watoto nyumbani alitaka kwenda kuwalaza lakini walikataa na kutaka kuogeshwa. Kimbembe kilianza katika kuwaogesha wale wadogo. walihtaji kuoga kwa maji ya moto, alienda moja kwa moja kuwasha jiko la umeme akakuta haliwaki. Akaanza kutukana ndipo alipokumbuka miezi mitatu iliyopita liliharibika na mkewe alipomuambia alisema watumie mkaa, akaenda kwenye jiko la gesi, hata hakuwasha kwani alikumbuka kuwa siku tatu zilizopita mkewe alimuomba hela ya gesi akamtukana mwanamke gani mvivu kuwasha mkaa, anatumia tu hela wakati hana chakufanya.

Alichanganyikiwa zaidi, akaenda kuwalaza watoto kwa lazima lakini ile na yeye anapanda kitandani mtoto mdogo akaanza kulia kwa sauti ya juu, joto, alitaka kuoga, ilibidi kunyanyuka kutaka kuwasha mkaa, atauwashaje hata mafuta ya taa hajui yako wapi labda angeweka ili uwake. Ilibidi kunyanyuka kuwasha TV watoto waliangalia mpaka walipopitiwa na usingizi, hata hakuwanyanyua yeye na watoto walilala, pale pale kwenye kochi mpaka asubuhi. Wote walipitiwa, asubuhi alistuka ameichelewa kazini na watoto walitakiwa kuandaliwa kwaajili ya shule.

********
Kichwa kilizidi kumuuma, hakujua aanzie wapi aishie wapi, akanunue vitafunwa au apike chai lakini atapika na nini? Akawaambia siku hiyo hakuna kwenda shule, akawasha gari kwenda kununua gesi na vitu vya nyumbani. Bado mkewe alikuwa hapatikani. alinunua jiko na kuja kupika chai akawapa watoto, akaanza kumtumia meseji mkewe za kumuomba msamaha, kumuomba arejee nyumbani kwani peke yake asingeweza kuwale watoto lakini meseji hasikupokelewa.

Simu ilianza kuita, ilikuwa namba ya bosi wake, alikuwa akimhitaji kupeleka taarifa ofisini, aliamua kumtafuta mdogo wake aje akae na wanae lakini naye alikuwa bize na kazi zake. Ili bidi kuwaacha watoto nyumbani na kwenda ofisini hivyo hivyo. Alifika ofisini na kukabidhi taarifa, baada ya muda meseji simu ilipiga kelele kuashiria kuwa meseji alizomtumia mkewe ziliingia, simu ilikuwa imewashwa.

Harakaharaka alinyanyua simu na kupiga, ilipopokelewa alianza kuomba msamaha aliongea maneno mengi ya kujilaumu na kumtaka mkewe kurejea nyumbani. "Wewe ndiyo mume wake?" Upande wapili uliuliza. "Ndiyo! Ndiyo Mimi! Kuna nini kimetokea! Mke wangu kafanya nini?" Aliuliza maswali mengi mfululizo. Ndipo aliposikia sauti ikimwambia tunapenda kukupa taarifa kuwa mkeo ame.......

Hakusubiri wamalizie iloneno ghafla akaishiwa nguvu na kuanza kupiga kelele akilia kwa sauti akisema "mke wangu kafariki" ndipo wafanyakazi wenzake walipo mnyanyua na kumkalisha katika viti na kuanza kumfariji. Rafiki yake mmoja aliamua kuichukua ile simu na kuamua kuongea na yule mtu ili ajue nini kilichotokea,akiwa pale chini ameishiwa nguvu ndipo alipoiskia sauti ya rafiki yake ikimuambia "unalia nini wakati mkeo amejifungua Salama".

Ooooh ndipo alipokumbuka kuwa mke wake nikweli alikuwa mjamzito na siku sinyingi alimpa taarifa juu ya siku za kujifungua zimekaribia Ila kwa sababu akili yake ilikua imetawaliwa na mchepuko hakuwa na ufwatiliaji juu ya afya ya mke wake,alijutia nakuomba radhi kwa wafanyakazi wenzake na akaomba kupelekwa Hospitali alipo mke wake.

Alipofika hospitali alienda moja kwa moja kwa mke wake na kupiga magoti japo lililowashangaza wengi kwakuwa wote walikua wakitokwa na machozi ndipo alipo omba msamaha na kukiri ni kweli alimtesa na kutomjali mke wake kwa sababu ya mchepuko aliokua nao uliiteka akili yake,iliskika sauti toka kwa mke yule 'mme wangu nilisha kusamehe siku nyingi ndio maana nipo nawe mpaka Leo' alijawa na furaha moyoni mwake na kukiri amejufunza juu ya upendo wa dhati na uaminifu katika ndoa na kuahidi kumpenda mke wake na familia nzima katika upendo wa kweli.

--------------MWISHO---------------
 
Haya bana wenye kuelewa watakuelewa na wenye kukaza shingo waendelee kukaza.

Ipelekwe MMU.
 
Ok. Kwa ambao ni mara ya kwanza kuiona burudikeni. Ilishaletwa hapa kitambo
 
Back
Top Bottom