Madhara ya Shisha

Dr. Sajjad Fazel

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
435
421
Shisha ni uvutaji wa tumbaku uliochanganywa na ladha za matunda mbali mbali kwa kutumia hookah. Hookah ni chombo kinachohifadhi maji na huwa ina mirija kuanzia eneo lakuchoma tumbaku kupitia maji mpaka mirija yakuvutia moshi mdomoni.

Shisha ni kitendo cha burudani iliyoenea nafasi nyingi hapa Tanzania mpaka imekua kitu cha kawaida. Burudani hii siyo tabia ya waafrika ki asili bali ni tabia ya warabu. Warabu huvuta shisha kwasababu ipo ndani ya mila yao. Watu wengi Tanzania wameiga tabia hiyo bila kujua madhara yake.

Uvutaji wa shisha inamadhara mengi kuliko uvutaji wa sigara. Hii ni kwasababu ya muda na idadi ya moshi unaovutwa. Mtu anayevuta sigara huwa anavuta mililita 30 ya moshi mara ishirini. Lakini mtu anayevuta shisha kwa saa moja, huwa anavuta mililita 500 ya moshi mara 200. Kwa ujumla anayevuta sigara anavuta takriban mililita 600 ya moshi wakati anayevuta shisha anavuta mililita 100,000 ya moshi kwa ujumla. Hivyo, mvutaji wa shisha huvuta moshi wa idadi ya sigara 100.

Madhara ya shisha hutokana na madhara yanayosababishwa na tumbaku. Tumbaku husababisha saratani aina 20, ikiwemo saratani ya mapafu, mdomo, koo, figo, kongosho, ini, tumbo na kadhalika. Tumbaku inayo chemikali sumu zinazosababisha saratani. Pamoja na hilo Chemikali sumu ndani ya tumbaku husababisha tatizo la moyo, tatizo la ufizi wa meno, kupunguza nguvu zakiume na tatizo la mapafu kwa ujumla.

Watu wengi wakivuta shisha, huwa wanatumia hookah moja. Tatizo lakutumia hookah moja ni mambukizi ya magonjwa. Kwa mfano; kama mtu moja anayo tatizo la kifua kikuu au kisamayu, kwa kutumia hookah ule ule anaweza kuwaambukiza wenzie.

Wakina dada pia wanapenda kujihusisha na mambo ya shisha. Ni muhimu kwa wale waliokuwa wajawazito waelewe kwamba uvutaji wa shisha huleta madhara kwa mtoto tumboni. Watoto wanaozaliwa kwa wale wanaotumia shisha huwa wanatatizo la mapafu pamoja na uzito mdogo sana.

Tumbaku pia huwa inayo nikotini. Nikotini inasababisha mazoea kwa wavutaji sigara na shisha. Nikotini ndicho kinachofanya mwili ipate mvutio na tumbaku (addiction). Ni vizuri watu waelewe tatizo la kuzoea shisha na ugumu wakuiacha baada yakutengeneza mazoea.

Kuna fikra moja la uwongo kwamba moshi ya shisha Ikipita ndani ya maji, huwa yanatoa chemikali sumu zinazosababisha saratani na nikotini. Huo si kweli. Utafiti zinaonyesha maji hayaondoi chemikali sumu inayopatikana ndani ya tumbaku.

Mbali na wavutaji shisha, wale watu waliokuwa pamoja na wavutaji wanaathirika kwa kuvuta hiyo moshi kwa ina moja au nyingine. Hivyo, wavutaji shisha hawaharibu afya zao tu lakini pia za wengine waliopo karibu nao.

Hizi ni baadhi ya chemikali sumu zinazopatikana ndani ya tumbaku yanaosababisha saratani (Acetaldehyde, Aromatic amines, Arsenic, Benzene, Beryllium, Cadmium, Chromium, Cumene, Ethylene oxide, Formaldehyde, Nickel, Polonium-210, Polycyclic aromatic hydrocarbons, Vinyl chloride)

Kama mtu yeyote anayo maswali kuhusu madhara ya shisha, anaweza kuniuliza hapa.

Asante.

13618152_10157176726785038_1490248848_n.jpg
 

Attachments

  • 13618152_10157176726785038_1490248848_n.jpg
    13618152_10157176726785038_1490248848_n.jpg
    67.1 KB · Views: 187
"Watakaokufa kwa Kuvuta Sigara ni Wachache kuliko Wakulima wa Tumbaku watakaokufa Tabora kwa kukosa soko la zao lao la Tumbaku, kupanga ni kuchagua Serikali ichague inataka Raia gani wafe"- Mbunge wa Zamani wa Sikonge Mh.Said Mkumba
 
"Watakaokufa kwa Kuvuta Sigara ni Wachache kuliko Wakulima wa Tumbaku watakaokufa Tabora kwa kukosa soko la zao lao la Tumbaku, kupanga ni kuchagua Serikali ichague inataka Raia gani wafe"- Mbunge wa Zamani wa Sikonge Mh.Said Mkumba

Watanzania zaidi ya 6,800 wafariki kila mwaka kwa utumiaji wa tumbaku. Wakulima wanaweza kulima mambo mengine. Laizma serikali iwasaidie hawa wakulima kulima mazao mengine kama mboga, matunda, korosho, mkonge na pia kuwapatia soko iliwasiathirike.
 
mbona hii imekuja baada ya kupigwa marufuku??? kwan mwanzo haikuwa na madhara???? mbona hawapigi marufuku sigara na kuku wa kisasa maana nao ni hatari?
 
Wangegusia na viroba kwa nguvu kama shisha ingekuwa poa!!
 
mbona hii imekuja baada ya kupigwa marufuku??? kwan mwanzo haikuwa na madhara???? mbona hawapigi marufuku sigara na kuku wa kisasa maana nao ni hatari?

La kwanza kuvuta sigara nje pia imepigwa marufuku. La pili, mimi nilikuwa nazingumiza Madhara ya shisha tangu mwezi wa nne kwenye Clouds Tv, Clouds FM, Choice FM na magazeti mbali mbali hata kabla yakupigwa marufuku. Na la mwisho, Naona wameikazania hiyo shisha kwasababu watu wengine wanaweka unga ndani yake. Ilikuwa njia moja yakutumia madawa yakulevya kwa baadhi ya watu.
 
Back
Top Bottom