Madhara ya Serikali ya Mseto

Dada Leti

JF-Expert Member
Oct 3, 2019
273
500
Nimeona wapinzani wetu wanamshangilia Rais Samia kuwaalika waingie Serikalini.

Bila shaka, Mama atawateua wale wapinzani wenye majina makubwa kwa malengo fulani ya kisiasa, pamoja na kuunda umoja wa kitaifa kama anavyodai.

Wasiwasi wangu ni kuwa, hawa wapinzani sijui kama wanajielewa.

Sijui kama wanaelewa madhara ya mfupa wanaotupiwa wautafune.

Wale wawindaji wanafahamu jinsi ya kumpoteza fisi anayekukimbiza. Unamtupia fupa ahangaike nalo wakati wewe unatokomea.

Wapinzani watakapojiloga kupokea hizo nafasi, kwanza watakuwa wameua vyama vyao kwa sababu hawawezi kufanya tena siasa za kipinzani wakiwa serikalini.

Pili, Mama Samia atakuwa amefanikiwa vizuri kutumia kanuni ya "divide and rule".

Wapinzani na wafuasi wao wataparaganyika huku na kule na hawatakua wanaelewa waunge mkono juhudi za serikali ya mseto ama waendeleza siasa zao za kipinzani.

Mama atakuwa amefanikiwa kuiua demokrasia kwa njia tulivu na ya kisayansi, tofauti na mtangulizi wake aliyewashugulikia wapinzani waziwazi.
 
Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,751
2,000
Nimeona wapinzani wetu wanamshangilia Rais Samia kuwaalika waingie Serikalini.

Bila shaka, mama atawateua wale wapinzani wenye majina makubwa kwa malengo fulani ya kisiasa, pamoja na kuunda umoja wa kitaifa kama anavyodai.

Wasiwasi wangu ni kuwa, hawa wapinzani sijui kama wanajielewa.

Sijui kama wanaelewa madhara ya mfupa wanaotupiwa wautafune.

Wale wawindaji wanafahamu jinsi ya kumpoteza fisi anayekukimbiza. Unamtupia fupa ahangaike nalo wakati wewe unatokomea.

Wapinzani watakapojiloga kupokea hizo nafasi, kwanza watakuwa wameua vyama vyao kwa sababu hawawezi kufanya tena siasa za kipinzani wakiwa serikalini.

Pili, mama samia atakuwa amefanikiwa vizuri kutumia kanuni ya "divide and rule".

Wapinzani na wafuasi wao wataparaganyika huku na kule na hawatakua wanaelewa waunge mkono juhudi za serikali ya mseto ama waendeleza siasa zao za kipinzani.

Mama atakuwa amefanikiwa kuiua demokrasia kwa njia tulivu na ya kisayansi, tofauti na mtangulizi wake aliyewashugulikia wapinzani waziwazi.
It is a polite and sound caution to the political snare. They have think hard, react to the strategy, and walk carefully. "Mama anataka kunasa ndege mjanja kwa kumtupia mtama".
 
Dada Leti

JF-Expert Member
Oct 3, 2019
273
500
Serikali ya mseto huwa inakuja pale vyama vinapopishana kidogo kama kule Zanzibar ccm na cuf ila kwa muungano ni ngumu kuwa na serikali ya mseto
Labda ni maneno tu ndio yanatofautiana maana lakini kitu ni kile kile.

Zanzibar wanaunda serikali ya mseto kwa mantiki ya kuwa, viongozi wa mihimili ya serikali wanatokana na vyama tofauti.

Lakini huu mseto wa samia, una lengo la kuwaleta watu wa vyama tofauti kuwa watendaji wa serikalini.

Kuna tofauti kati ya "viongozi" na "watendaji" katika serikali.

Mseto wa zanzibar ni viongozi, lakini mseto wa Tanzania ni watendaji.

Mfano mzuri ni Anna Mghwira RC wa Kilimanjaro.
 
Dada Leti

JF-Expert Member
Oct 3, 2019
273
500
Wapinzani si wanatka kuongoza ??? Wanapewa nafasi ili waongoze then lengo linakuwa limetimia.
Kuna tofauti kati ya kuwa Kiongozi na mtendaji wa serikali.

Hawa wapinzani watapewa vijikazi vidogo vidogo tu kwa lengo la kuwavuruga na kuwachota akili.

Mseto wa kweli ni ule wa kuongoza muhimili wa nchi.

Haya, tego hilo. Ngoja tuone.
 
Dada Leti

JF-Expert Member
Oct 3, 2019
273
500
It is a polite and sound caution to the political snare. They have think hard, react to the strategy, and walk carefully. "Mama anataka kunasa ndege mjanja kwa kumtupia mtama".
Hawa kwa jinsi ninavyowafahamu hawawezi kuchomoka kwenye huu mtego.

Mfano mzuri ni wabunge wa COVID.
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
17,719
2,000
Hahahaa.... yaaniii....

Mimi siku zote nina mashaka na hawa wanaoitwa wapinzani. Hawaelewi nini wanachotaka.
Ni wajinga flani hivi!

Ukiona wanavyoshangilia sasa hivi ni kama vile adui yao si ccm bali Magufuli
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,659
2,000
Nimeona wapinzani wetu wanamshangilia Rais Samia kuwaalika waingie Serikalini.

Bila shaka, mama atawateua wale wapinzani wenye majina makubwa kwa malengo fulani ya kisiasa, pamoja na kuunda umoja wa kitaifa kama anavyodai.

Wasiwasi wangu ni kuwa, hawa wapinzani sijui kama wanajielewa.

Sijui kama wanaelewa madhara ya mfupa wanaotupiwa wautafune.

Wale wawindaji wanafahamu jinsi ya kumpoteza fisi anayekukimbiza. Unamtupia fupa ahangaike nalo wakati wewe unatokomea.

Wapinzani watakapojiloga kupokea hizo nafasi, kwanza watakuwa wameua vyama vyao kwa sababu hawawezi kufanya tena siasa za kipinzani wakiwa serikalini.

Pili, mama samia atakuwa amefanikiwa vizuri kutumia kanuni ya "divide and rule".

Wapinzani na wafuasi wao wataparaganyika huku na kule na hawatakua wanaelewa waunge mkono juhudi za serikali ya mseto ama waendeleza siasa zao za kipinzani.

Mama atakuwa amefanikiwa kuiua demokrasia kwa njia tulivu na ya kisayansi, tofauti na mtangulizi wake aliyewashugulikia wapinzani waziwazi.

Naamini unazungumzia wale PRO CCM na sio CHADEMA
 
Dada Leti

JF-Expert Member
Oct 3, 2019
273
500
Ni wajinga flani hivi!

Ukiona wanavyoshangilia sasa hivi ni kama vile adui yao si ccm bali Magufuli
Hahahaaaaaa... lol.

Hawajui kuna mfumo ambao una mizizi zaidi ya magufuli.

Haya ngoja tuone nini kitatokea baada ya adui yao kufa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom