Madhara ya Marufuku Siasa kwa miaka 5 imesababisha CCM kukosa uvumilivu wa kisiasa

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,402
24,327
14 August 2020
Hai, Kilimanjaro
Tanzania

Madhara ya Marufuku ya Siasa kwa miaka 5 imesababisha CCM kukosa uvumilivu wa kisiasa na kutishia machafuko nchini
Kufuatia kupigwa marufuku shughuli
za kisiasa Tanzania sasa tunaona madhara yake katika maeneo fulani. Na athari zake zimekuwa kubwa kabisa kwa upande wa CCM kwa wanachama, makada, wafuasi na wapenzi wake kukosa kufuata sheria, jadi , kawaida ya waTanzania kushindanisha hoja kwa kutumia ushawishi na kubaki na ulemavu wa kifikra kuamua kutumia nguvu na mabavu.

Video : Tukio la wanaCCM jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro


Shughuli za kisiasa zilitumika kutoa elimu ya kiuraia kuwajenga Watanzania kuamini katika kupiga kura ndiyo njia sahihi ya kumkataa mwanasiasa fulani baada ya kusikiliza hoja zake.

Lakini sasa tunaona baada ya viongozi wa juu wa nchi mwaka 2016 kuamua kuachana na haki hiyo ya msingi kabisa ya kikatiba kwa kupiga marufuku shughuli za kisiasa sasa baadhi ya waTanzania nao wameonesha wamekosa uvumilivu na kupoteza ufahamu kuwa huwezi kumpiga marufuku mwanasiasa fulani kufika eneo lako kisa mnatofautiana ktk mitizamo ya kiitikadi na mpo chama tofauti.

Tuliyoyaona kule wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ni matunda ya serikali ya CCM Mpya kupiga marufuku viongozi wa vyama vya upinzani kufika maeneo fulani kwa miaka 5 sasa, sababu watawala wa CCM wanadai mbunge wa chama fulani siyo eneo lake la kibunge au kuwa uchaguzi umeisha hivyo hakuna kuendelea kufanya siasa za hoja kujenga ushawishi.

Katiba ya nchi iliona mbali kuwa ruhusa ya kufanya siasa ni afya kwa utulivu wa nchi ili ikifikia kipindi cha kampeni waTanzania wasiwe wabaguzi wa kisiasa au kimaeneo bali wawe na ufahamu wa kufanya maamuzi kupitia sanduku la kura.

Tumeona wanaojiita wanaomtetea Magufuli kuwa hawataki kuona watu wengine wanafika maeneo yao kwa kuwa hawajawaona kufika huko kwao, bila kufahamu kuwa wanasiasa hao wa upinzani walipigwa marufuku.

Na kuthibitisha wanaigiza tabia za viongozi wa juu wa serikali ya CCM Mpya wamejaribu na wao kufanya jaribio la mwendelezo haramu wa marufuku kwa kufunga barabara, kufanya vurugu na kupandisha mabango ya shutuma kuwa wanasiasa wa vyama vingine ni mabeberu, vibaraka wa wazungu n.k

Hii siyo afya nzuri kwa siasa za Tanzania kwa wananchi kuacha kutumia sanduku la kura kufanya uamuzi na kuamua kutumia njia zingine sisizotambulika kupeleka ujumbe hawataki uchaguzi, wagombea wa vyama vingine na kampeni za kisiasa.

Kama nilivyojaribu kufafanua haya ndiyo matunda na matokeo ya kuminya siasa kufanyika, kuzuia midahalo, kuzuia kutoa maoni ktk vyombo vya habari, asasi za kiraia NGO, kuwaumiza wapinzani na sasa vikundi vya watu huko Hai Kilimanjaro wameamua kuiga vitendo vya serikali na watawala wa CCM Mpya kujichukulia sheria mikononi, kupuuza haki za mtanzania na mwanasiasa kujumuika na waTanzania wa mikoa, wilaya na majimbo mengine kufanya shughuli za kisiasa.

Hali hii isipodhibitiwa na serikali ya CCM nchi itakuwa haifuati utawala wa sheria na katiba kuanzia ngazi za viongozi waliopo ktk nafasi za uongozi wa dola na mpaka mitaani kama tulivyoona kwa baadhi ya wananchi wa wilaya ya Hai.

Nadhani hili tukio la watu kukosa uelewa wa haki za kiuraia za kwao na za wengine kufanya shughuli za kisiasa, wasomi na wazoefu kama Mzee Pius Msekwa wataona walikosea kuunga mkono kuzuia shughuli za kisiasa na kuwa ni hatari kwa usalama wa nchi pia kinyume na vile walivyofikiria wakati walipounga mkono marufuku ya kufanya siasa baada ya uchaguzi kuisha 2015.

Published on 10 Jul 2018
Video hii ikimuonesha mmojawapo wa thinktank ya CCM Mpya ikimuunga mkono Magufuli kupiga marufuku shughuli za kisiasa
Pius Msekwa: Hauoni kwamba kuzuia mikutano ya hadhara ni kuuwa upinzani?, Sumaye alinihoji

 
24 June 2016

MAGUFULI : HAKUNA SIASA MPAKA 2020

Tanzania's President elect Magufuli addresses members of the ruling CCM at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam

Picha : Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli
* Wapinzani, wadau wampinga wadai anataka kuua demokrasia

RAIS Dk. John Magufuli amepiga marufuku vyama kufanya ushindani wa siasa mpaka baada ya miaka mitano ili wananchi wahoji wanasiasa kama wametekeleza yale waliyoyaahidi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Alitoa kauli hiyo Ikulu Dar es Salaam jana baada ya kukabidhiwa ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva.

“Niwaombe wanasiasa wenzangu wafanye siasa za ushindani kwa nguvu zote baada ya miaka mitano ili wananchi watuhoji tuliyoyaahidi kama tumeyatekeleza au hatujayetekeleza.

“Kila nchi hata zile zilizobobea kwenye demokrasia unapokwisha uchaguzi unakuwa ni wakati wa kazi.

“Haiwezekani mkawa kila siku ni siasa watu watalima saa ngapi? Kila siku ni siasa, ni vema tukatimiza wajibu wetu tuliopewa na wananchi na watatupima kwenye hilo.

“Ni matumaini yangu kuwa Watanzania tunaowaongoza wanataka maendeleo. Iwe kwa bahati nzuri au mbaya Serikali inayoongoza ni ya Chama Cha Mapinduzi.

“Yapo tuliyoyaahidi kuyatekeleza kwa wananchi katika kipindi cha miaka mitano, nisingependa kuona mtu yeyote ananichelewesha kutekeleza hayo niliyoahidi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema Rais Magufuli.

Alisema ushindani wa sasa ambao unatakiwa ufanywe kwa nguvu ni kwa wale wawakilishi waliopewa mamlaka na wananchi kupeleka hoja zao kwenye maeneo yao.

“Kama ni madiwani wakapeleke hoja kwa nguvu zote kwenye maeneo yao, kama ni wabunge wakazungumze kwa nguvu sana bungeni lakini hata kuziba midomo nayo ni demokrasia, hiyo ni demokrasia ya mwelekeo wa ya aina yake,”alisema.

Alisema ingawa watu mbalimbali walijitokeza kugombea katika uchaguzi wa mwaka jana, uchaguzi huo haukuwa na mshindi wala mshindwa na kwamba Watanzania wote ni washindi.

“Uchaguzi umekwisha, wakati wa uchaguzi watu mbalimbali walijitokeza kugombea wengine wakaibuka washindi lakini naomba niwaambie kwamba uchaguzi huu haukuwa na mshindi wala mshindwa, sisi Watanzania wote kwa umoja wetu ni washindi,”alisema.

Source : Magufuli: Hakuna siasa mpaka 2020 - Mtanzania
 
Katika video hii utaona jinsi wananchi walivyofedheheshwa kwa mkutano wa TL kuvurugwa.

Na wapo wananchi walikuwa wanawatuliza wenzao wasijibu vurugu walizofanyiwa.

 
Mkuu Bagamoyo

Sijawai ona wapumbavu kama CCM kwa kweli. Wao ndo wanaanzisha fujo wao ndo wanapanga watu wao kufanya fujo alafu wao ndo wanaleta propaganda kuwa Eti Tundu Lissu katumwa na wazungu kuja kuleta fujo!

Yaani fujo mfanye na kuongoza nyie alafu nyie wenyewe ndo mlete maneno kuwa Chadema mgombea wao katumwa kuleta fujo.

Kwa haya yote ninayoyaona nazidi kusisitiza kuwa hakuna namna CCM watashinda uchaguzi was mwaka huu. Nasema hakuna!!
 
Magufuli na timu ya washauri wake wanaojiita thinktank ya CCM Mpya kina Pius Msekwa, Job Ndugai n.k walikosea sana.

Sasa baadhi ya Watanzania hawana uelewa wa demokrasia, vyama vingi, katiba , kushawishi, kujenga hoja kilichobaki ni CCM Mpya wamejenga mazingira ya kuleta machafuko nchi Tanzania kwa makusudi au bila ya kujitambua.

Utawala wa CCM Mpya haujachelewa bado kuna muda wa kijisahihisha waombe Baraza la Usalama na Ulinzi la Tanzania lifanye kikao cha dharura kuthathmini, kuchambua, kujadili tishio hili jipya na kumshauri Rais na wasaidizi wake kurekebisha hali hii kabla ya mambo ya usalama wa nchi hii ya Tanzania kuharibika kabisa.

Kwani inaonesha upande wa CCM Mpya, watendaji wake na vyombo vyake vyote ndiyo wanaotaka "kuvunja madaraja" ya mafahamiano na umoja baina ya waTanzania wa kambi tofauti za vyama, itikadi na maeneo wanakotoka.
 
Magufuli na timu ya washauri wake wanaojiita thinktank ya CCM Mpya kina Pius Msekwa, Job Ndugai n.k walikosea sana.

Sasa baadhi ya waTanzania hawana uelewa wa demokrasia, vyama vingi, katiba , kushawishi, kujenga hoja kilichobaki ni CCM Mpya wamejenga mazingira ya kuleta machafuko nchi Tanzania kwa makusudi au bila ya kujitambua..
Unazani baraza la usalama watashauri nini??? Kikubwa wamuachie jiwe mwenyewe nchi impasukie.

There is no way CCM watakubali kuachia hii nchi kwa amani, sasa waache waanzishe fujo wenyewe alafu wananchi waje kuwajibu!!
 
Acha wavune wlichopanda tuliwashauri sana hawkutaka kusikia walidhani kumiliki dola ndio kumiliki akili zetu. Ukimchunga sana mtoto lazima akuletee mimba.

Tuliwambia acheni wapinzani waaongee ili ikifika wakati wa kuongea wasiwe na mapya,sasa ccm wameongea pekee yao 5 yrs hadi wamemaliza yote hawana mapya ambayo awajazaoea wananchi hata tayari tunajua kwenye kampeni zao hawana mapya zaidi ya sgr,

flyover, mabeberu, stiglers,ndege yatakuwa ni ya kurudiarudia si ajabu kuwaambia wananchi wa kasulu,tarime,pangani tumejenga flyover au sgr ambao kuwaelewesha hadi wajue sgr,flyover ni nini ni lzm uwe na dictionary.Leo wanawazuia wapinzani kuongea sababu wapinzani wanayo mengi
 
Mkuu Bagamoyo

Sijawai ona wapumbavu kama CCM kwa kweli. Wao ndo wanaanzisha fujo wao ndo wanapanga watu wao kufanya fujo alafu wao ndo wanaleta propaganda kuwa Eti Tundu Lissu katumwa na wazungu kuja kuleta fujo!...
Wala sio Ccm mkuu
Huyu ni mpumbavu mmoja mteule ambae ame jisahau na kuona yeye ni kila kitu hapo Hai.. Sasa nadhani ifike mwisho Mh Rais kama kweli jana akiona uwepo wa Mungu pale TAG amuondoe Sabaya wilaya ya Hai. Huyu sio mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama bali ni mhuni tuu.
 
Unazani baraza la usalama watashauri nini??? Kikubwa wamuachie jiwe mwenyewe nchi impasukie.

There is no way CCM watakubali kuachia hii nchi kwa amani, sasa waache waanzishe fujo wenyewe alafu wananchi waje kuwajibu!!

Ni ushauri kwa wenye mamlaka, wakitaka kurekebisha sawa, wakiamua kuwa wanaweza kuendelea na hali hii inayosababisha hali ya hatari kwa usalama wa nchi ni juu yao. Wao ndio wenye maamuzi.
 
Ni bahati mbaya sana, hata wenye akili CCM wameufyata,wametulia tuliii bariiiiiidi....!

Mrisho Mpoto,aliwahi kuimba(kabla ya 2015:))kuwa madhila yakizidi mioyo ya Binadamu huota kutu....kinachojengwa Sasa kwenye mioyo ya Watanzania kitakuja kuigharimu nchi!

Wala huu si utabiri , hii Ni Sheria ya kimaunbile !inaweza kuchelewa tu kulingana na aina ya Jamii!kwenye Jamii goigi(Tz!?)inaweza kuchukua muda mrefu lakini ukweli upo palepale!

NA HATUA ZISIPOCHUKULIWA UCHAGUZI WA 2025 UTAKUWA MGUMU SANA!
Mungu ibariki Tanzania!
Tuamshe tuache woga
Unafiki
Uzandiki
Kwa sababu hii Ni Mbolea ya anguko,
Machafuko
Chuki
Haki huinua Taifa!
 
13 Oct 2019
Mzee Msekwa amfananisha JPM na Nyerere.



Mzee Pius Msekwa alionesha matumaini makubwa kwa Magufuli. Sasa aombe miadi wakazungumze faragha hali hii mpya ambayo naamini hata kwa jinsi Nyerere alivyozungumzia kujenga umoja atakuwa anaweweseka kaburini kuiona Tanzania inakaribia kutumbukia katika machafuko kutokana na ukosefu wa kujali.
 
Mkutano na wastaafu : Jaji Mkuu Samatta hapepesi macho kuhusu utawala wa sheria

4 Jul 2018
Ni tarehe 2 Julai 2018 Ikulu Dar es Salaam katika kikao cha Rais John Magufuli na viongozi wastaafu. Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas ameeleza bila woga, kuhusu umuhimu wa rais na viongozi wengine kuzingatia utawala wa sheria, tena sheria nzuri.
 
Wala sio Ccm mkuu
Huyu ni mpumbavu mmoja mteule ambae ame jisahau na kuona yeye ni kila kitu hapo Hai.. Sasa nadhani ifike mwisho Mh Rais kama kweli jana akiona uwepo wa Mungu pale TAG amuondoe Sabaya wilaya ya Hai. Huyu sio mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama bali ni mhuni tuu.
Naona unamsahau Magu. Huyu bwana akiwa kanisani au kwenye mikutano ya watumishi wa Mungu ni malaika mkamilifu. Na akishatoka hapo anakuwa shetani aliyekamilika pia. Pale kwenye mkutano wa TAG lazima aone mkono wa Mungu, lakini nje ya mkutano anaona mkono wa shetani.
 
Naona unamsahau Magu. Huyu bwana akiwa kanisani au kwenye mikutano ya watumishi wa Mungu ni malaika mkamilifu. Na akishatoka hapo anakuwa shetani aliyekamilika pia. Pale kwenye mkutano wa TAG lazima aone mkono wa Mungu, lakini nje ya mkutano anaona mkono wa shetani.
Na hao wanao mwalika Ni Mawakala wa Nani!
 
Mkutano na wastaafu : Jaji Mkuu Samatta hapepesi macho kuhusu utawala wa sheria

4 Jul 2018
Ni tarehe 2 Julai 2018 Ikulu Dar es Salaam katika kikao cha Rais John Magufuli na viongozi wastaafu. Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas ameeleza bila woga, kuhusu umuhimu wa rais na viongozi wengine kuzingatia utawala wa sheria, tena sheria nzuri.

Hii clip mkuu Bagamoyo ndo huwa inamaliza kila kitu. Ukiangalia hii clip ndo utapata jibu kuwa sio kwamba Magufuli hakuwai kuambiwa before hapana aliambiwaga na hawa viongozi majaji wastaafu sema ni kiburi chake tu.

Yanayoendelea sasaivi ni matokeo ya siasa chafu za kidhalimu za magufuli na watu wake wachache Kama kina Sabaya!
 
Back
Top Bottom