Madhara ya machinga kwenye afya na uchumi

pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,465
6,109
Rais amepiga marufuku machinga kuzuiliwa kuingia mijini kati na biashara zao.
Wengine wanauza nguo,viatu ,matunda ,vyakula na kadhalika.
Je,haya maamuzi yana madhara kiuchumi na kiafya?

1.Kiuchumi,maduka yanakosa wateja maana machinga wapo barabarani.
Machinga hawalipi kodi.Mauzo madukani yatashuka na makusanyo ya kodi yatashuka sana.

2.Wenye maduka watatoa bidhaa zao barabarani,kwenye hifadhi za barabara.Hakutakuwa na parking za magari,hivyo makusanyo ya halmashauri yatashuka sana.

3.Kiafya,msimu wa masika unakaribia.Miji yetu ni michafu,sewage systems zinavuja.Magonjwa ya mlipuko yataweza kudhibitiwa? Hao wamachinga na ndugu zao watakwepa kufa na kipindupindu?

Magonjwa ya kuhara?
Wakurugenzi hawataweza tena kuzuia biashara za matunda,mama ntilie kwenye sehemu chafu.Wameng'olewa meno.

Rais wetu umeteleza,haijawahi kutokea serikali ikapendwa kama unavyotaka.Umekosea na unaenda kuua uchumi wa halmashauri na nchi.
Unaenda kusababisha vifo kutokana na kipindupindu n.k
 
Bavicha bana wakiondolewa machinga mnalalamika wakiruhusiwa mnakuja Na sababu za kitoto... MH rais kashatoa maelekezo watafutiwe sehemu maalum ambapo kila kitu kitazingatiwa
 
Back
Top Bottom