Shangazi yangu aliniambia ukimtilia mwanaume Libwata usha uua, yaani atakufa mapema, na kukuacha na watoto peke yako. Au ndio usha mlemaza akili, hawezi kuwa mwanaume kamili, na atashindwa kufanya majuku yake, na umasikini ndio usha ukaribisha hivo.
Washirikina wote kwenye koo yangu ni masikini sana, kuliko wote. Wengine kama wamelaanika hivi na watoto wao hawabarikiwi, wanaishi kwa maumivu maumivu. Magonjwa na maradhi ya ajabu ajabu.
Nilikuwa na rafiki wa kike kutoka Tabora, kuna siku aliniambia yeye anaenda kwa mganga wa kienyeji kuchukua chukua dawa ya mapenzi ili mumewe hasimuache, hasiwe na mchepuko, na awe anamuachia pesa nyingi.
Kuna siku yule mumewe akanifuata na kunitaka kimapenzi, nilishangaa na kujiuliza dawa zote zile hazifanyi kazi?Nilifikiri zile dawa ni majani ya mpapai tu ama kisamvu, kumbe ni sumu jamani.Miaka 7 baadae nikaletewa meseji na binamu yangu, yule mume wa rafiki yangu amefariki dunia. Nikakumbuka akiosema shangazi yangu limbwata sio zuri, kumbe ni kweli.
Nimekutana na marafiki wengi sana wananishawishi tuende kwa waganga, nawaambiaga namuamini mungu tu.Kama mtu hakupendi au anatabia mbovu mbovu bora kuachana nae kuliko kulazimisha akupende, kwa madawa.
Na wanaume mujue wanawake wa Dar hatari, wapo kimaslay yao tu. Musidandie dandie kila mwanamke, wengine hawamjui mungu, wanamjua shetani tu.
Babu yangu alikuwa Tabibu, mfuga majini, msoma albadili, na wengi walio kula dawa ya huyu mzee sio wazima kiakili, wasema ovyo. Hadi mama yangu walimtilia madawa alikuwa msema ovyo, mgonjwa na haeleweki.
Msile sile tu madawa ya waganga, mtaweuka akili. Jamaa mmoja alisema nitilie tu Limbwata nikikupenda sana ndio vizuri, utakufa.