Mkuu, mwili wa binadamu ni wa moto, unapokunywa maji au kinywaji chochote cha baridi, yanapofika ndani ya tumbo, yanasababisha mwili kufanya kazi ya ziada ya kuyabadili maji kuwa ya moto ndipo yaweze kutumiwa na mwili. Maji au kinywaji baridi kamwe hakiwezi kutumika na ubaridi wake, vinginevyo damu yako itakuwa baridi na madhara yake ni makubwa.
Unapotumia maji moto, mwili wako haupati kazi yeyote kubwa ya kusafisha na maji hutumika maramoja, na kwa sababu maji ni ya moto huyeyusha mafuta mafuta yanayoelea ndani ya tumbo.
Mfano chukua chupa mbili nyeupe zilizowekwa mafuta na yakaisha, chupa moja mimina maji baridi, utaona mafuta yaliyobaki kwenye kuta za chupa huganda na kuonekana. Chupa ya pili mimina maji ya moto, utaona kuta za chupa zinazidi kuwa nyeupe bila mafuta au uchafu wowote.
Ndiyo maana unapokunywa maji baridi, mafuta yaliyopo kwenye kuta za tumbo huganda na ndiyo mojawapo wa chanzo cha kitambi, ukinywa maji moto mafuta yaliyopo kwenye kuta za tumbo huyeyushwa na kitambi huanza kupotea.