Madhara ya kumtumikia Rais haya hapa

Madhara ya kumtumikia Rais haya hapa

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Viongoz wote wa Umma wanaapa kuwatumikia wananchi na siyo kumtumikia Mhe Rais.

Lakini viongozi wengi wa Umma wamejikita kumtumikia Mhe Rais kuliko wananchi.

Rais ni binadamu mwenye mapungufu yake, hajakamilika na hivyo taifa alipaswi kumtumikia au kutumika kwa ajili yake maana wanaotumika watatumikia mema na mabaya yake.

Viongoz wanaotumikia wananchi awapaswi kumtumikia Rais Bali wanapaswa kumheshim na kumshauri Rais ipasavyo kwa maslahi mapana ya nchi.

Marais wote waliopita Tanzania wamethibitika kufanya mambo ambayo kitaalam yanaitwa kushindwa kulinda rasilimali ipasavyo. Umetokea ubadhirifu na uhujumu wa Mali za umma kwa sababu waliopaswa kumshauri walijikita kuwatumikia.

Watu wale wale waliojikita kumtumikia Rais ndo hao hao anapoondoka wanabaini mapungufu yake. Kumbe wangejikita kuwatumikia wananchi wangemshauri Rais sawasawa na matakwa ya umma

Wasomi na watumishi wa Umma watumikieni wananchi acheni kumtumikia Rais maana anapita ila wananchi wapo siku zote. Tumshauri Rais ipasavyo bila kujali kupoteza nafasi zetu. Tumshauri kwa hekima na maarifa, tusimtumikie.
 
Wengine wanashindwa hata kuapa mbele yake kwa sababu ya ukali wake uliokithili
 
Sasa si ungemtaja jina tu. Japo wapo wengi Ila yule profesa wa.najalalani yupo kwenye first three.
 
Kwa nchi zetu hizi za kiafrika Rais ni Mungu mtu ambaye ana kauli kuliko mwananchi.
 
Back
Top Bottom