Madhara ya Kufutwa kwa CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madhara ya Kufutwa kwa CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LordJustice1, Mar 7, 2011.

 1. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikitafakari sana jinsi kejeli toka katika Serikali ya JK na chama chake cha CCM wakati wa uchaguzi kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pamoja na vyama vingine vya upinzani ni "vyama vya msimu-uchaguzi!" Pamoja na kejeli hizo CHADEMA kilitoa upinzani mkali sana kwa CCM na kuna uwezekano mkubwa wa uchakachuaji wa kura za urais na hatimaye kimekuwa ni Chama Kikuu cha Upinzani!

  CCM kwa kujua umahiri wa Wabunge wa CHADEMA hasa wawapo Bungeni (2005 - 2010) walijiandaa sana na hata kubadili Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007 ili kukidhoofisha Bungeni ambako umaarufu wake ulianzia.

  Kubaini hivyo CHADEMA kilifuata utaratibu wa "kuishtaki CCM/Serikali kwa wananchi" kama walivyofanya wakati wa kusoma "List of Shame" wakati walipobaini kuwa ufisadi wote ulioibuliwa (Meremeta, Tangold, Mwananchi Gold, EPA, Richmond, Deep Green Finance, etc) haukufuatiliwa kwa undani unaostahili na Serikali.

  CCM/Serikali wameshabaini kwamba CHADEMA si "chama cha msimu" kama walivyokuwa wamefikiria, lakini badala ya kujibu mapigo wamekimbilia msaada wa dola ili angalau kiendelee kulinda ka-umaarufu kaliobakia ili kasimalizwe kabisa na CHADEMA.

  Bila shaka hoja iliyoko mezani kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mh John Tendwa, ni kukifuta CHADEMA au la kwa madai eti kwamba wametoa kauli ambazo zinahatarisha amani na utulivu wa nchi, na wameenda mbali kwa kudai kwamba kauli hizo zinaashiria uhaini!

  Maswali ya kujiuliza ni kwamba: Hivi kwa nini wananchi wanaitikia maandamano yanayoitishwa na CHADEMA kwa wingi kiasi hicho? Ina maana wananchi hawawezi kufikiria kwamba CHADEMA ni chama cha namna gani mpaka CCM iwaambie? Hivi kauli za kukataa malipo haramu ya DOWANS na kupinga kupanda kwa bidhaa za vitu kwa mfumuko wa ajabu kunahatarisha amani na utulivu? Mbona wananchi wenyewe wameandamana kwa amnani na hakuna aliyesababisha vurugu yoyote? Hivi CCM inaogopa nini hasa mpaka Mwenyekiti wake Mh JK aliongea kwa unyonge wa ajabu wakati wa Hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari, 2011. Kumbuka kwamba JK kwenye Hotuba yake alidai eti kwamba "hivi karibuni wananchi wameingiwa na hofu!" Hivi ni wananchi wa mkoa upi walioingiwa na hofu? Na kama wangeingiwa na hofu kwa nini wajitokeze kwenye maandamano? Hivi ni wananchi walioingiwa na hofu au ni CCM ndiyo iliyoingiwa na hofu kwa kuogopa kivuli cha CHADEMA?

  Sasa nije kwenye title ya thread hii. Je, Msajili wa Vyama vya Siasa, Mh John Tendwa, akiamua kucheza shilingi chooni akakifuta CHADEMA kutoka kwenye daftari lake, nini kitatokea?
  1. Demokrasia ya nchi itakuwa imebakwa sana kwa kuwa nchi itaongozwa na Chama kimoja kikiwa katika matawi mbalimbali: CCM-A (CCM), CCM-B (CUF), CCM-C (TLP), CCM-D (UDP), CCM-E (NCCR-MAGEUZI), etc.
  2. Nchi itaingia tena kwenye chaguzi nyingine ndogo za wabunge na madiwani ambazo zitasababisha gharama kubwa zisizo za lazima. Kwa sasa nasikia nchi haina fedha za kutosha kwa sababu wafadhili waligoma kugharamia uchaguzi mkuu, 2010, kwa hiyo tulitumia fedha zetu wenyewe! Sasa kwa nini tuingie kwenye gharama za namna hiyo? Si afadhali tuilipe DOWANS kama hatuna uchungu na fedha kiasi hicho?
  3. Mafisadi watapumua kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu hakutakuwa na wa kuwabughudhi kwenye ufisadi wao watakaokuwa wanaufanya!
  4. Kuna uwezekano wa kutokea vurugu, maana wananchi wenye kuipenda nchi yetu hawatapendezwa na hatua ya kukifuta CHADEMA! Mungu apishe mbali kwenye hili!
  5. EX-CHADEMA members wataenda Mahakamani kupinga kufutwa kwa CHADEMA na kwa kuwa haki huwa haiwezi kuzuiwa, huwa inacheleweshwa tu, watashinda kesi na watakuwa na nguvu ya ajabu kuliko ilivyokuwa mwanzo.
  6............
  7...........
  Mh John Tendwa tafadhali usilewe madaraka, Maisha ni zaidi ya huo usajili wa vyama, zawadi ambayo umeikabidhiwa kwa muda na JK! Itakie mema nchi yetu ambayo demokrasia yake ndio kwanza imeanza kuchipua! Serikali inapokosolewa hailali usingizi, inafanya juu chini itekeleze ahadi zake kwa wananchi! Badala ya kutekeleza ahadi zenu mmekuwa busy kuangalia CHADEMA inafanya nini na kupoteza muda na resources za nchi kwa kuwafuatilia, shame on you! Historia itawahukumu kwa hili!


  Tujadili!
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Naona wakuu bado kuchangia mada hii, stay blessed anyway!
   
 3. J

  John10 JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chadema ni chama ni chama cha Wakatoliki, na Padre Slaa ndiye Padre Mkuu wa chama hicho. Mbinu za Padre Slaa ni kuleta Ukatoliki wake zaidi ndani ya Serikali. Chadema bora kifutwe kabla Counter-Attack kutoka haijaanza kazi yake.

  Angalia Somalia, Pakistan, au Iraq. Kama Chadema kitaendelea kuwepo basi ujue kabisa nchi itaingia ktk vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa sababu, Waislamu hakubali Padre Slaa awe Rais.
   
 4. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Umesoma Katiba ya CHADEMA ukakuta kuna mambo ya Kikatoliki humo? Na kwenye mikutano yao umesikia CHADEMA kikiongelea juu ya Ukatoliki au hata UDINI kwa ujumla wake? Si JK mwenyewe kwa kuishiwa hoja huwa anaamua kusema kuwa Tanzania kuna udini ili aonewe huruma? Mbona Dr Slaa alishaacha upadre akaoa, kwa nini kumbagua mtu kwa dini yake? Ni kama kusema ule usemi alioutoa Nyerere kwamba "Sifa zoooote za kuwa Rais anazo, ila 'TATIZO NI MKATOLIKI!'" Huko Somalia, Pakistan au Iraq kulikuwa na Chama gani cha wakatoliki na walifanya nini au kikatokea nini? Huoni kuwa propaganda za JK za kudai kwamba kuna chama chenye udini ndio zinazosambaza udini mpaka ameifanya nchi sio moja tena ili yeye aendelee kuwa madarakani?
   
 5. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Sheria ya vyama vya siasa iko wazi kwamba, chama cha siasa chenye misingi ya udini, ukabila, n.k. hakitasajiliwa, sasa unaposema CHADEMA ni chama cha wakatoliki haueleweki, jenga hoja za maana sio ushabiki usio na kichwa wala miguu, hatupo katika JF kucheza kiduku hapa, Toa mawazo kama mtu mwenye akili timamu, ni mwendawazimu peke yake ndio asiyeweza kuona hali ngumu ya maisha iliyopo. Tuwe wazalendo kwa kuwa wakweli, CCM nchi imewashinda, ila wanang'ang'ania madaraka kwa sababu kwao uongozi ni ajira na sio utumishi. Hata mkijikomba sana kuwatetea mwisho wake upo karibu. Labda wabadilike kabisa kivitendo, lakini kwa mtindo wanaokwenda nao, hawana maisha marefu mbele ya safari, hata wananchi wamechoka na hali ngumu, siku wakisema imetosha, hakuna nguvu za dola zitakazoweza kuwazuia. Mungu ibariki Tanzania.
   
 6. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siku ukisikia Tanzania kuna vita ni siku ambayo watakifuta CHADEMA. Hapo ndio utajua kwamba kuna watanzania wenye hasira.

  NI mangai CCM wanafanya lakini wao huwa wakifanya ni sawa? Wengine wakifanya ni makosa?
   
 7. J

  John10 JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi siyo propaganda za JK. Chadema na Padre Slaa agenda yao kubwa ni kuleta Ukatoliki serikalini. Waislamu wanajua huu mpango. Nyerere aliwaumiza na kuwatesa sana Waislamu kwa Ukatoliki wake. Safari hii, Waislamu hawatokubali kumuona Padre Slaa anakuwa Rais. No Way.
   
 8. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Usipotoa ushahidi maana yake unaeneza propaganda kama anavyofanya JK. Nimekuambia uoneshe kwenye Katiba ya CHADEMA au angalau kauli kwenye mikutano ya CHADEMA wanazungumzia UKATOLIKI, umeshindwa kutoa umeng'ang'ania kuwa "Waislamu hatukubali!" Huoni unafanya kile kile ambacho unadhani kwamba unakipinga?
   
 9. J

  John10 JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushahidi? angalia Uongozi wa Chadema, na Wabunge wa Chadema, majority ni kutoka Dini moja na Kabila moja. Naona huo ni ushahidi tosha.
   
 10. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kama ilivyo suala la uzazi,kwamba mchakato mzima wa upatikanaji wa mtoto,maandalizi ya awali na vipindi vya uchungu na kero ni mchakato binafsi wa watu wawili..ila mtoto akishazaliwa ni wa jamii..waliofanya mchakato mzima wa upatikanaji wa mtoto husika watabaki kuwa wazazi tu! Hawana haki ya kusitisha uhai wa mtoto hata km wao ndio wazazi wake! Km ilivyo kwa mtoto...Chadema kilifanyiwa mchakato,kikaandaliwa,kikasukwa,kikazaliwa na kukua..wamefanya kile wengine wasichothubutu kufanya...Si Tendwa wala Kikwete wenye mamlaka na uhai wa CHADEMA! Ni chama cha umma,kilichofika kilipo kwa kufuata kanuni na taratibu!
   
 11. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kwa kuwa JK ni mwislamu akifuatiwa na Makamu wa Rais basi CCM ni Chama cha Waislamu? CUF Je, kwa kuwa majority ni Waislamu kwa hiyo Chama hicho ni cha Waislamu? Je, Sheria ya Vyama vya Siasa inasema kwamba chama kikiwa na watu wengi wa kutoka kwenye dini fulani basi chama hicho ni cha watu wa dini hiyo? Je, Kuna Waislamu ambao wamekatazwa kujiunga na CHADEMA? Mbona kuna Waislamu ambao wamejiunga na CHADEMA?
  Je, kuna siku yoyote ambayo umewahi kusikia CHADEMA wanahubiri UKATOLIKI au UDINI kama anavyofanya JK na wapambe wake, wewe ukiwa mmojawao?
   
 12. J

  John10 JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nazungumzia Majority. Hata CCM, majority ni Wakatoliki. Lakini, Chadema kina agenda kabisa ya UDINI na UKABILA. Kwenye kampeni mwaka jana, Padre Slaa alikuwa anasema Waislamu "wanapendelewa" Huu ni ushahidi tosha kwamba agenda ya Padre Slaa ni kuona Waislamu wananyimwa haki zao zote kama akiwa Rais.
   
 13. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa alisema katika Mkutano upi wa Kampeni (taja tarehe na mahali husika plse) kwamba eti Waislamu "wanapendelewa?"
   
 14. J

  John10 JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Naona unaanza ubishi usio na msingi. Tafuta video ktk You tube utaona ktk mahojiano na ITV alisema kwamba JK "anapendelea" waislamu, zipo video nyingi tu zenye ushahidi huo wa kutosha.
   
 15. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sina ubishani, umejenga hoja mwenyewe, kwa hiyo wa kuitetea ni wewe mwenyewe! Haya nasubiri hayo mahojiano!
   
 16. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  @TM zile siasa za kutofungamana na upande wowote sasa hazipo.
   
 17. n

  nyangwe Senior Member

  #17
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kelele za vyura hazimzuii Tembo kunywa maji na mfa maji haachi kutapatapa,siku ya kufa nyani mti yote huteleza.the ends day of ccmfaka chama cha mafisadi aka chama cha kuchua chako mapema aka chama cha mazoea nk is at hand.
  nionavyo mimi wanajua nguvu ya chadema,imani ya wananchi kwa cdm wanaijua,wanataka kutishia nyau (cdm)wakati nyau hatishiki kwa panya (ccm) HON.Dr slaa na Mbowe wamesema wapo tayari kwa lolote.wakifute watakiona kama dr hatahamasisha wananchi waandamane kumungoa jk halafu hata akipigwa risasi damu yake haitapotea bure mpaka lengo la damu hiyo kumwagika litakapo timia ie kuingoa
  go dr.slaa go Mbowe, go cdm go all patriotists
  " Freedom has always been an expensive thing,history is a fit testimony to the fact that freedom is rarely gained without sacrifice and self denial"
   
 18. n

  nyangwe Senior Member

  #18
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kelele za vyura hazimzuii Tembo kunywa maji na mfa maji haachi kutapatapa,siku ya kufa nyani mti yote huteleza.the ends day of ccmfaka chama cha mafisadi aka chama cha kuchua chako mapema aka chama cha mazoea nk is at hand.
  nionavyo mimi wanajua nguvu ya chadema,imani ya wananchi kwa cdm wanaijua,wanataka kutishia nyau (cdm)wakati nyau hatishiki kwa panya (ccm) HON.Dr slaa na Mbowe wamesema wapo tayari kwa lolote.wakifute watakiona kama dr hatahamasisha wananchi waandamane kumungoa jk halafu hata akipigwa risasi damu yake haitapotea bure mpaka lengo la damu hiyo kumwagika litakapo timia ie kuingoa
  go dr.slaa go Mbowe, go cdm go all patriotists  " Freedom has always been an expensive thing,history is a fit testimony to the fact that freedom is rarely gained without sacrifice and self denial"
   
 19. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tunaokoelekea! MUNGU SAIDIA.mimi c mkatoliki wala mchaga,lakini niko cdm.simchukii Jk kwa sababu ya uislamu wake,bali kukosa maono kwake.nampenda dr Slaa c kwa ukatoliki wake,bali dhamira ya dhati aliyonayo kwa kumkomboa mTZ.
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  akili za kuangalizia hizi:

  Pakistani, Somalia, Iraq kuna wakatoliki?
   
Loading...