LordJustice1
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 2,263
- 533
Nimekuwa nikitafakari sana jinsi kejeli toka katika Serikali ya JK na chama chake cha CCM wakati wa uchaguzi kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pamoja na vyama vingine vya upinzani ni "vyama vya msimu-uchaguzi!" Pamoja na kejeli hizo CHADEMA kilitoa upinzani mkali sana kwa CCM na kuna uwezekano mkubwa wa uchakachuaji wa kura za urais na hatimaye kimekuwa ni Chama Kikuu cha Upinzani!
CCM kwa kujua umahiri wa Wabunge wa CHADEMA hasa wawapo Bungeni (2005 - 2010) walijiandaa sana na hata kubadili Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007 ili kukidhoofisha Bungeni ambako umaarufu wake ulianzia.
Kubaini hivyo CHADEMA kilifuata utaratibu wa "kuishtaki CCM/Serikali kwa wananchi" kama walivyofanya wakati wa kusoma "List of Shame" wakati walipobaini kuwa ufisadi wote ulioibuliwa (Meremeta, Tangold, Mwananchi Gold, EPA, Richmond, Deep Green Finance, etc) haukufuatiliwa kwa undani unaostahili na Serikali.
CCM/Serikali wameshabaini kwamba CHADEMA si "chama cha msimu" kama walivyokuwa wamefikiria, lakini badala ya kujibu mapigo wamekimbilia msaada wa dola ili angalau kiendelee kulinda ka-umaarufu kaliobakia ili kasimalizwe kabisa na CHADEMA.
Bila shaka hoja iliyoko mezani kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mh John Tendwa, ni kukifuta CHADEMA au la kwa madai eti kwamba wametoa kauli ambazo zinahatarisha amani na utulivu wa nchi, na wameenda mbali kwa kudai kwamba kauli hizo zinaashiria uhaini!
Maswali ya kujiuliza ni kwamba: Hivi kwa nini wananchi wanaitikia maandamano yanayoitishwa na CHADEMA kwa wingi kiasi hicho? Ina maana wananchi hawawezi kufikiria kwamba CHADEMA ni chama cha namna gani mpaka CCM iwaambie? Hivi kauli za kukataa malipo haramu ya DOWANS na kupinga kupanda kwa bidhaa za vitu kwa mfumuko wa ajabu kunahatarisha amani na utulivu? Mbona wananchi wenyewe wameandamana kwa amnani na hakuna aliyesababisha vurugu yoyote? Hivi CCM inaogopa nini hasa mpaka Mwenyekiti wake Mh JK aliongea kwa unyonge wa ajabu wakati wa Hotuba yake ya mwisho wa mwezi Februari, 2011. Kumbuka kwamba JK kwenye Hotuba yake alidai eti kwamba "hivi karibuni wananchi wameingiwa na hofu!" Hivi ni wananchi wa mkoa upi walioingiwa na hofu? Na kama wangeingiwa na hofu kwa nini wajitokeze kwenye maandamano? Hivi ni wananchi walioingiwa na hofu au ni CCM ndiyo iliyoingiwa na hofu kwa kuogopa kivuli cha CHADEMA?
Sasa nije kwenye title ya thread hii. Je, Msajili wa Vyama vya Siasa, Mh John Tendwa, akiamua kucheza shilingi chooni akakifuta CHADEMA kutoka kwenye daftari lake, nini kitatokea?
1. Demokrasia ya nchi itakuwa imebakwa sana kwa kuwa nchi itaongozwa na Chama kimoja kikiwa katika matawi mbalimbali: CCM-A (CCM), CCM-B (CUF), CCM-C (TLP), CCM-D (UDP), CCM-E (NCCR-MAGEUZI), etc.
2. Nchi itaingia tena kwenye chaguzi nyingine ndogo za wabunge na madiwani ambazo zitasababisha gharama kubwa zisizo za lazima. Kwa sasa nasikia nchi haina fedha za kutosha kwa sababu wafadhili waligoma kugharamia uchaguzi mkuu, 2010, kwa hiyo tulitumia fedha zetu wenyewe! Sasa kwa nini tuingie kwenye gharama za namna hiyo? Si afadhali tuilipe DOWANS kama hatuna uchungu na fedha kiasi hicho?
3. Mafisadi watapumua kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu hakutakuwa na wa kuwabughudhi kwenye ufisadi wao watakaokuwa wanaufanya!
4. Kuna uwezekano wa kutokea vurugu, maana wananchi wenye kuipenda nchi yetu hawatapendezwa na hatua ya kukifuta CHADEMA! Mungu apishe mbali kwenye hili!
5. EX-CHADEMA members wataenda Mahakamani kupinga kufutwa kwa CHADEMA na kwa kuwa haki huwa haiwezi kuzuiwa, huwa inacheleweshwa tu, watashinda kesi na watakuwa na nguvu ya ajabu kuliko ilivyokuwa mwanzo.
6............
7...........
Mh John Tendwa tafadhali usilewe madaraka, Maisha ni zaidi ya huo usajili wa vyama, zawadi ambayo umeikabidhiwa kwa muda na JK! Itakie mema nchi yetu ambayo demokrasia yake ndio kwanza imeanza kuchipua! Serikali inapokosolewa hailali usingizi, inafanya juu chini itekeleze ahadi zake kwa wananchi! Badala ya kutekeleza ahadi zenu mmekuwa busy kuangalia CHADEMA inafanya nini na kupoteza muda na resources za nchi kwa kuwafuatilia, shame on you! Historia itawahukumu kwa hili!
Tujadili!