Madhara ya dua la kuku kwa mwewe: Kuku na yeye ni kiumbe wa Mungu

Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
2,347
3,033
Ndugu zangu, mnakumbuka hadithi za MAZIMWI WALA WATU na kelele za AGANO JIPYA?

Hadithi hii nilihadithiwa na Baba. Katika hadithi hiyo alisikika mtu mmoja akisema

Enyi mateka wenzangu kwenye nchi ya MAZIMWI WALA WATU wenye uchu wa damu zetu, tusikate tamaa MUNGU anatuona na kutusikia tuzidi kumuomba atatujibu dua zetu na atatuokoa ni swala muda tu tuwe wavumilivu.

Je, mnakumbuka hali ilivyokua wakati wa AGANO LA KALE limeshamiri, Agano ambalo MAZIMWI WALA WATU wamekua wakilitegemea kwa KIBURI na MAJIGAMBO?

Je, mnakumbuka tulivyomuomba sana MUNGU kwa vilio vya uchungu kuhusu UDHALIMU wa MAZIMWI na MUNGU akatujibu kwa kuzima KIBURI na MAJIGAMBO yao?

kama maandiko yalivyosema na ikawa tofauti na ilivyotegemewa kama mmesahau basi nendeni mkasome KUMBUKUMBU LA TORATI: 17:3-21

Mateka wenzangu hata sasa tusichoke kuomba, kama wao kwa makusudi na kwa hila ya uchu na tamaa yao hawataki kuleta AGANO JIPYA basi MUNGU atalileta kwa kuwasambaratisha na dhoruba na wala wasitambuane tena

Midhali wamedhihirisha kwa kauli yao wenyewe kwamba hawana mpango na AGANO JIPYA kwa sasa basi hiyo ni kudhihirisha KIBURI na MAJIGAMBO mbele za MUNGU na huko ni kutangaza vita ya mojakwamoja na MUUMBA hivyo basi tuzidishe maombi na tutarajie majibu ya haraka sana kwenye vita hii kabla ya 2025.
 
Ni Aibu na ni hatari sana CCM kujiona wanaweza kuamua mambo yq kitaifa ambayo inatakiwa yaamuliwe na watu karibu 60M.
 
Back
Top Bottom