Madhara ya Bangi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madhara ya Bangi

Discussion in 'JF Doctor' started by Maasai_, Jul 5, 2012.

 1. M

  Maasai_ Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kufahamu madhara ya Bangi kwani wengine wanasema ni dawa na mi natumia
   
 2. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Tukupe? we nani mbaka upewe?? sema naomba kufahamu..nyama we
   
 3. paty

  paty JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,251
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  haina madhara .
   
 4. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,866
  Trophy Points: 280
  Bangi can cure cancer I heard.
   
 5. M

  Maasai_ Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiswahili kigumu mkuu huoni we mwenyewe badala ya kutype mpaka umetype mbaka
   
 6. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,943
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  bangi ni majani yaliyokaushwa ya mmea ujulikanao kitaalamu kama canabis sativa na mwingine ujulikanao kama canabis indica. bangi ina majina meeeengi kutokana na maeneo inakotumika, marijuana, hashish, na mengineyo

  kemikali iliyo ndani ya bangi hujulikana kama delta-9-tetrahydrocannabinol kwa kifupi (Δ9-THC). kiasi kidogo kabisa kinachoweza kusababisha effect mwilini mwako ni kuanzia microgram 10 kwa kila kilo ya uzito wako...


  baadhi ya matumizi ya bangi kiafya ni pamoja na;

  hutumika kwenye dawa za kutuliza kikohozi na kichefuchefu,

  pia inatumika kwenye dawa za glaucoma (presha kwenye macho)

  Marihuana pia hutumika kupunguza maumivu kwa wagonjwa wa kansa na ukimwi walio kwenye hatua ya mwisho


  madhara ya bangi ni: euforia(kujisikia haireee), midomo kukauka, heat sensation, mapigo ya moyo kuongezeka........ etc  ngoja nikomeee hapo kwa sasa
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Hasara ya Kuvuta Sigara kubwa ''Bangi''

  [TABLE="class: cms_table, width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"][TABLE="class: cms_table, width: 599"]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="class: cms_table, width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  BAADA ya kuwepo kwa baadhi ya tafiti zilizokuwa zikiruhusu uvutaji wa bangi kwa madai kwamba ilisaidia wagonjwa waliosumbuliwa na msongo wa mawazo, hali hiyo imesababisha baadhi ya nchi kuruhusu matumizi yake.

  Pamoja na mawazo ya wengi kufikiria kuwa kutokana na nchi ya Jamaica ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kwa watumiaji wengi ingekuwa ya kwanza kuruhusu bangi, lakini ukweli ni kwamba nchi ya Canada

  ndiyo ilikuwa ya kwanza kukubali bangi kutumiwa kama dawa ya maradhi.
  Baada ya utafiti huo wa awali hivi karibuni watafiti wengine wamegundua kuwa matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasababisha kujiongezea madhara badala ya kutibu kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.

  Watafiti hao wamekwenda kinyume na wale wa kwanza kwa kusema kuwa matumizi yake yana uwezekano mkubwa wa kumletea mtumiaji magonjwa ya kupungua uzito mara kwa mara, magonjwa ya figo, ini na ugonjwa wa akili.

  Watafiti waliogundua athari hizo ni wale wanaotokea nchini Australia ambao katika utafiti wao wamegundua kuwa zaidi ya vijana 3,100 walio katika umri wa miaka 20 ndio wamekuwa watumiaji wakubwa wa bangi.

  Utafiti wao umekwenda mbali na kubaini kwamba asilimia 18 ya vijana hao ni wale waliojiingiza katika matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa muda wa miaka miwili au mitatu.
  Asilimia nyingine 16 ya vijana wa umri huo wamebainika kutumia kwa muda wa kati ya miaka minne hadi mitano.

  65 kati ya watumiaji wamegundulika wameshaathirika na maradhi ya ugonjwa wa akili.
  Wakati hao wakisumbuliwa na tatizo hilo wengine 233 wamebainika kuathirika kwa figo na ini.

  Watafiti wamebaini vijana wengine kati yao wanasumbuliwa na tatizo la kupata uchizi (wehu).
  Baada ya kubaini hayo watafiti wametoa ushauri kwa vijana kutotumia dawa hizo za kulevya kwa vijana kwa zaidi ya miaka sita au zaidi tangu pale siku ya kwanza alipoanza kutumia.

  Wanasema kuwa kwa wale ambao sasa wamevuta kwa muda mrefu kati ya miaka 15 na zaidi wengi wao wamekumbwa na tatizo la kiakili.

  Kwa mujibu wa Dk. John McGrath, wa kituo cha uchunguzi wa afya ya wagonjwa wenye mtindio wa ubongo cha Queensland, nchini Marekani, anasema: “Wengi wa wagonjwa ambao wamekumbwa na matatizo hayo tumegundua ni wale waliowahi kutumia bangi kwa muda mrefu na hatimaye kujikuta wakipata tatizo la akili.”

  Daktari huyo anasema kuwa ni nadra sana kukutana na wagonjwa wa akili vijana halafu wakawa hawajawahi kutumia bangi, iwe mwaka mmoja au zaidi.
  Anasema kuwa iwapo matumizi ya bangi yatakomeshwa tatizo la vijana kupata matatizo ya utaahira yatapungua kwa kiasi kikubwa duniani.

  Bangi ni nini, inatumiwaje?

  Kwa hapa nchini na baadhi ya nchi, bangi imetambulika kama dawa ya kulevya ambayo imekuwa na majina mengi kutokana na kutumiwa na kundi la vijana zaidi kuliko watu wazima.
  Bangi imekuwa ikijulikana kwa majina mengi ikiwamo, dawa, ganja, hashish, kijiti, marijuana, kaya blunt na mengineyo, ilimradi kutegemeana na sehemu inapotoka.

  Watumiaji wengi wamekuwa wakiitumia kwa kuvuta kama sigara au wengine hutumia kwenye kiko kwa kuvuta.

  Bangi ni bidhaa iliyochanganyika na kemikali hatari ambazo ni sumu na huathiri afya.
  Wapo baadhi ya watumiaji wa bangi ambao wamekuwa wakiitumia kwa kuiweka katika maji wakiifanya kama majani ya chai na wengine huchanganya kwenye chakula.
  Bangi inaathiri vipi ubongo?

  Wanasayansi wamebaini kuwa matatizo makubwa yanaanza kupatikana kutokana na bangi kuingia kwenye ubongo wa mtumiaji na huathiri mfumo mzima wa akili.

  Tatizo kubwa linalomkumba mvuta bangi ni kunyemelewa na magonjwa ya ugonjwa wa shinikizo la damu (BP), kupoteza kumbukumbu, mawazo, anaridhika hata kama ana matatizo.

  Pia mtumiaji wa kila siku anakuwa akikumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika ubongo wake.
  Imebainika kuwa bangi inachangia kuongeza mapigo ya moyo kutoka asilimia 20 hadi 100, muda mfupi tu wa saa tatu baada ya kuvuta.
  Bangi huaribu mapafu, kwani ina zaidi ya asilimia 50–70 ya kemikali aina ya carcinogenic hydrocarbons kuliko mvutaji wa tumbaku.

  Mtumiaji wa bangi hupumua kwa tabu sana kuliko yule anayevuta tumbaku ingawa wote wanaharibu mapafu, pamoja na kuwa na uwezekano mkubwa wa kukaribisha ugonjwa wa kansa.

  Imebainika kuwa watu wanaovuta bangi wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na matatizo mengi ya kiafya.
  Watafiti wamegundua kuwa wavutaji wengi wa bangi wamekuwa hawana mahusiano mema na watu walionao karibu kwani wamekuwa chanzo cha matatizo kutokana na wao kuona kila wanachofanya ndiyo sahihi na cha wenzao si sahihi.@
  Maasai_
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  ATHARI ZA BANGI


  BANGI


  Bangi ni mmea wenye rangi ya kijani,ambao hutoa majani na maua ambayo hutumika kama kilevi.Bangi hustawi karibu maeneo yote hapa nchini na hutumika zaidi kuliko dawa zingine za kulevya.


  Bangi hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Mara,Iringa,Arusha,Kilimanjaro,Shinyanga,Tabora,Tanga,Kagera,Mbeya.Morogoro.n.k


  Madhara ya Bangi


  Matumizi ya bangi husababisha madhara mbali mbali ikiwa ni pamoja na:


  · Kuchanganyikiwa,ukatili,ukorofi,uhalifu,n.k.


  · Kuona,kusikia na kuhisi vitu visivyokuwepo.


  · Kupoteza kumbukumbu


  · Utegemezi na usugu


  · Moshi wa bangi unapoingia kwenye mapafu hutengeneza kitu kama lami ambayo huganda na kuathiri utendaji kazi wa mapafu.


  · Bangi ni kemikali (sumu) inayosababisha (saratani) zaidi ya tumbaku (sigara).


  · Kupunguza kinga ya mwili


  · Mtumiaji kuridhika na hali duni aliyonayo hivyo kukosa mwamko wa maendeleo huku akijihisi ni mwenye mafanikio makubwa.


  · Kuumwa koo,kupata kikohozi na saratani ya mapafu.


  · Kuathirika kwa mfumo wa uzazi ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na mabadiliko ya hedhi kwa wanawake.


  · Kuharibika mimba


  · Kuzaa mtoto njiti


  Imani na hisia potofu kuhusu uvutaji wa bangi


  Je ni kweli bangi huongeza uwezo wa kusoma na kuelewa zaidi?Hapan.Bangi hufanya mishipa ya damu na ubongo kusinyaa,kunakosababisha kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kukumbuka.Utafiti umebainisha kuwa wanafunzi waliovuta bangi kwa matarajio hayo wameshindwa kufaulu.


  Utajiepushaje na utumiaji wa bangi?


  · Jiepushe na makundi ya watumia bangi


  · Shiriki kwenye michezo


  · Jifunze na kuzingatia stadi za maisha


  Sheria inasemaje kuhusu bangi?


  Kutumia,kuhamasisha matumizi,kuuza,kusafirisha,kuhifadhi au kujihusisha kwa namna yoyote ile na bangi ni kosa la jinai.Adhabu kwa makosa haya hufikia hadi kifungo cha maisha
   
 9. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Canabis,jani, ndumu,kijiti,cha arusha,herb,hemp....
   
 10. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  tangu nimeanza kutumia sijapata MADHARA.!
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Subiri mkuu Madhara yake utayaona baadae sio sasa wakati utakapoumwa au kushauriwa na Daktari uache ndio hapo Madhara yatakuwa yameshakuingia BAGAH
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
 13. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
 14. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
 15. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwa maana hiyo basi wengi wetu tumeshakula sana bangi kwakutokujua eeeeeeeeeee
   
 16. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
Loading...