Madhambi na makosa ya Serikali ya CCM hayaondoi na kuhalalisha udhaifu wa CHADEMA kushika Dola,Tujipange kwa Umakini....

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Mara utasikia Kidumu chama Tawala, wanahitikia KIDUMUU, Pembezoni utasikia Ngangari Jino kwa jino,

Mwishoni kabisa utasikia Peoples' wanaitikia power. Katika kuvichunguza vyama vya siasa tulivyonavyo nimeona vyote vina mfumo na madhaifu yale yale tofauti ni alama za vidole wanavyonyoosha na sare zao.

Bila kupepesa macho vyama vyote vya upinzani vimeingia mtego wa ku copy baadhi ya mambo yafanyikayo CCM na kuya paste ndani ya mifumo yao , hii ni kutokana na kwamba ndio chama kikuu kianzilishi hapa nchini.

Kwa uchunguzi wa kina tumeyagundua haya yafuatayo
1.Rushwa

Ndani ya vyama vyetu vyote vina abudu katika rushwa kabisa, tuhuma kadhaa zimewaendea viongozi wa vyama vyote kiongozi akiwa CCM kikifuatiwa CHADEMA, tukumbuke kwamba uchache wa rushwa ndani ya CHADEMA si kwamba kuna waadilifu wengi , hapana ni kwakuwa hata mali za kula hawana wanaiba hicho hicho kidogo , kuanzia ruzuku, mpaka mali za vyama na manunuzi.

CHADEMA imetuhumiwa sana kwenye Rushwa ya ngono na undugu katika teuzi ama za viti maalumu na kugombea nafasi mbali mbali kushika madaraka ndani ya chama kwenye ngazi za juu,

2.Wanao hoji kupotea
kila chama kinajua yanayoendelea, na saa nyingine umekuwa ni mchezo wa kiurushiana mpira, CHADEMA wakimpoteza mtu wao wanajificha katika wanaopotea kisa ubavu wa serikali hasa ya awamu ya tano kumbe kuna baadhi ya mambo wanakuwa wamehoji na kutofautiana na wakubwa.

nina mifano michache juu ay suala hili
A.Mwita Waitara amewahi kuweka bayana mipongo mibovu ya mwenyekiti Mbowe dhidi yake na pia kuweka hadharani mipango yao dhidi ya wengine.

B. Zitto kabwe kwenye ziara za Arusha akiwa bado ndani ya Chadema na tuhuma juu ya Lema na mipango michafu juu yake.

c. Benson Mramba amekuwa anaeleza hapa kila mara kuhusu masuala yanayoendelea ndani ya CHADEMA,

Kwa upande wa CCM ndo kinara wa kuteka na kupoteza watu wanaotuhumiwa kuyapinga ya wakubwa na saa nyingine kujeruiwa kabisa, nikisema nitoe mifano ya CCM tutakesha hapa,

3.Ukanda na Ukabila,
CCM imeanza kunyemelewa sana na suala ambalo ndo lipo kabisa ndani ya CHADEMA ambalo wachache ndani ya CHADEMA wamelipigania sanaa nadhani limeanza kupungua, ukitaka kuthibitisha ilo hata watakao comment kupinga hoja hii ni watu wa ukanda huo,

4.Udikteta wa wenyeviti wa vyama hivi viwili hasa CCM na CHADEMA, unafanana kabisa , tofauti ya Mbowe na Magufuli ni kwamba mmoja ana Phd na mwingine ni bachelor degree, mwingine wa kanda ya ziwa mwingine ni wa Kaskazini, Mmoja ni Rais mwingine ni mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni, ila kwa suala la udikteta wote wanafanana, siyo hao tu hata wa vyama vingine vipo katika mfumo huo,

5.Hakuna chama chenye ajenda ya kitaifa kukwamua umaskini, wote wana ubinafsi na umimi, hasa CDM wana kujiona kama kikundi special ndani ya nchi kum be nao ni watanzania kama walivyo CUF, NCCR na TLP, ajenda nyingi za vyama vyetu vimejikita kujenga vyama zaid badala yua Taifa,


Kwa maoni yangu muamko ukiwapo wa ama kuvisafisha vyama hivi au kuanzisha vyama vingine ningependa visiingie mtego wa kuyafuata yaliyokuwa ama madhaify ya CCM na CHADEMA ndo tupate siasa safi ya ushindani bila kushikiana mitutut na risasi,
CHADEMA BADO NAO WANA MADHAIFU MAKUBWA MNO, PAMOJA NA KWAMBA CCM NI WABOVU ILA HATA MBADALA WAO HAWAKO VEMA

Britanicca
 
Kama ni hivyo bora tubadili tu.

Walau tutaridhika kuwa tumebadili.

Na pia tutajenga utamaduni wa kubadili.
usemalo kweli ila je tutakuwa tumetatua tatizo ama tumebadiri wa kutusababishia matatizo yale yale
 
Sababu kuu ya kubadilisha ni kuwaonyesha wanaopewa nafasi ya kuongoza ni wafanyakazi wa taifa hili na sio mabosi wenye uwezo wa kutumia Kodi za wananchi Kama wapendavyo
 
Tanzania haijawahi kupata vyama vya upinzani vya hovyo kama tulivyo navyo, uimara wa vyama vya upinzani huonekana pale tu inapotokea CCM ikiongozwa na kiongozi dhaifu, na uimara wake hukoma mara tu CCM inapopata kiongozi bora.
 
CHADEMA wakishika dola hata kwa miaka mitano tu wanaweza wasifanye chochote cha tofauti lakini watakua wamefungua kitu kipya kwa nchi yetu, UWAJIBIKAJI wa vyama vya siasa, CCM na vyama vingine vyote watakua wanajua wazi kuwa ukivurunda basi wananchi wanakuadhibu kwa sanduku la kura, kwa hali ilivyo sasa CCM itaendelea tu kujivua magamba lakini inabaki kuwa ileile, chama kinachokumbatia mfumo na watu DHAIFU, wazee wa ndiyooo!
 
Mimi nitakua tayari kuchagua hata jiwe iwapo tu nitahakikishiwa ccm kutoka madarakani kwa hiyari baada ya kushindwa kwenye uchaguzi huru na wa haki utakaoitishwa siku za usoni.
Kwani mkuu jiwe litakuwakilisha vip
 
CHADEMA wakishika dola hata kwa mika mitano tu wanaweza wasifanye chochote cha tofauti lakini watakua wamefungua kitu kipya kwa nchi yetu, UWAJIBIKAJI wa vyama vya siasa, CCM na vyama vingine vyote watakua wanajua wazi kuwa ukifurunda basi wananchi wanakuadhibu kwa sanduku la kura, kwa hali ilivyo sasa CCM itaendelea tu kujivua magamba lakini inabaki kuwa ileile, chama kinachokumbatia mfumo na watu DHAIFU, wazee wa ndiyooo!
Hii ni Point
 
Ila katika yote chadema pekee wameonesha mini maana ya upinzani

Toka 2000 kuwa chama cha upinzani bila kutetereka sio mchezo waongeze juhudi watafika mbali
 
Tanzania haijawahi kupata vyama vya upinzani vya hovyo kama tulivyo navyo, uimara wa vyama vya upinzani huonekana pale tu inapotokea CCM ikiongozwa na kiongozi dhaifu, na uimara wake hukoma mara tu CCM inapopata kiongozi bora.

Unaposema kiongozi bora unatumia vigezo gani?

Hatujawahi kuwa na kiongozi bora nchi hii.

Na ndiyo maana uchumi wetu umekwama na umasikini unaota mizizi.

Tangu JPM aingie madarakani umasikini umepungua kwa 2%. Sasa huyo utamuita kiongozi bora kweli?
 
Unaposema kiongozi bora unatumia vigezo gani?

Hatujawahi kuwa na kiongozi bora nchi hii.

Na ndiyo maana uchumi wetu umekwama na umasikini unaota mizizi.

Tangu JPM aingie madarakani umasikini umepungua kwa 2%. Sasa huyo utamuita kiongozi bora kweli?
Kaka Umaskni umepungua kivipi
 
CHADEMA wakishika dola hata kwa mika mitano tu wanaweza wasifanye chochote cha tofauti lakini watakua wamefungua kitu kipya kwa nchi yetu, UWAJIBIKAJI wa vyama vya siasa, CCM na vyama vingine vyote watakua wanajua wazi kuwa ukivurunda basi wananchi wanakuadhibu kwa sanduku la kura, kwa hali ilivyo sasa CCM itaendelea tu kujivua magamba lakini inabaki kuwa ileile, chama kinachokumbatia mfumo na watu DHAIFU, wazee wa ndiyooo!
Waanze kwanza kumtoa mbowe kama wanaweza, maana inaweza isha miaka mitano wakang'ang'ania kama mbowe anavyofanya kwenye uenyekiti
 
Back
Top Bottom