ALEX_ANDER
JF-Expert Member
- Jul 8, 2014
- 570
- 812
Sawa kabisa, tena waoshe na maiti, na wawasaidie madaktari wakati wa postmortem ili wajue madhara ya vitendo vyaoMamlaka ya Usalama wa Uchukuzi nchini Kenya NTSA imependekeza adhabu mpya miongoni mwa madereva walevi.
Madereva walevi sasa watalazimika kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti ili kupunguza idadi kuu ya ajali za barabarani.
”Hatuwezi kuwa na madereva wengi walevi wanaofanya ajali na wanapofikishwa mahakamani wanapewa adhabu hafifu.Tutakapokamilisha kutengeza sera hiyo mpya tutahakikisha kuwa inakuwa sheria”, alisema mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis Meja.
Na Wakenya wengi katika mitandao ya kijamii waliunga mkono mpango huo na kusema kuwa utawafanya madereva kuwa makini.
Je una hisi sheria hii ikija Tanzania itasaidia kupambana na madereva walevi?.
Hata ukiambiwa kafagie shuleni ni adhabu kubwa sana kwa sababu unaacha shughuli zakoKumbe kufanaya kazi mochwari ni adhabu!!!.
Balimi Bia za mwalimu na maaskariAisee hiyo sheria ikifika huku naacha balimi
Jamaniwalazwe mochwari kabisa au wawekwe kwenye majeneza kwa masaa mawili tena usiku
Hailingani na makosa wanayofanya. Madereva hao walevi wanaweza kusababisha ajali, watu wakapoteza maisha, wiungo vya mwili, uharibifu wa mali nk, kwa makusudi.Hata ukiambiwa kafagie shuleni ni adhabu kubwa sana kwa sababu unaacha shughuli zako
Alafu eti wanaita ni adhabu.Upuuzi huu...Yaani mwili wa marehemu ukapatiwe huduma na mlevi?
Si bora ndugu yangu nimuandae mwenyewe nyumbani na nikamzike kwa ustaarabu na heshima anazostahili.
Upuuzi huu...Yaani mwili wa marehemu ukapatiwe huduma na mlevi?
Si bora ndugu yangu nimuandae mwenyewe nyumbani na nikamzike kwa ustaarabu na heshima anazostahili.
Hivi mnajua wanaofanya kazi mochwari ndo walevi kuzidia? Hao jamaa huwa wanachapia mkate kwenye vodka chee ili macho yao yarudi focus na magoti yao mawili yaache mnato.Alafu eti wanaita ni adhabu.