Madereva walevi kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti Kenya?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
_98847990_210c8af1-63da-4a93-b090-e33f67987434.jpg


Mamlaka ya usalama wa uchukuzi nchini Kenya NTSA imependekeza adhabu mpya miongoni mwa madereva walevi.

Madereva walevi sasa watalazimika kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti ili kupunguza idadi kuu ya ajali za barabarani.

''Hatuwezi kuwa na madereva wengi walevi wanaofanya ajali na wanapofikishwa mahakamani wanapewa adhabu hafifu.Tutakapokamilisha kutengeza sera hiyo mpya tutahakikisha kuwa inakuwa sheria'', alisema mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis Meja.

Na Wakenya wengi katika mitandao ya kijamii waliunga mkono mpango huo na kusema kuwa utawafanya madereva kuwa makini.


BBC
 
Back
Top Bottom