BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,533
- 3,839
Wakuu,
Nakubali kabisa sisi madereva wa serikali tukiwa barabarani huwa tunaona barabara kama zetu na huwa tunaona waendeshaji wengine wa magari hawana lolote wala hawana chochote. Hiyo ni chanzo cha ajali huko barabarani
Lakini mi naomba niwaambie ukweli, madereva tunarogana sana. Tunarogana ili kuzipata safari za na maboss lengo ni kupata posho, hivyo ukiona kila safari mwenzio ndio anapangiwa basi lazima utatafuta namna ya kufanya ili safari ijayo asipate yeye upate wewe na hapo ndio tunaangukia kwenye ushirikina.
Kwenye riziki hapakosi chuki, dereva yupo tayari kwenda kwa mganga kumtengenezea ajali dereva mwezie ikibidi afe ili yeye awe anapata safari na maboss.
Madereva wenzangu, tusipokuwa makini tutaisha kwa ushirikina.