Madereva wa magari makubwa na mabasi ni kuanzia miaka 45

Pyepyepye

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
1,940
3,825
Serikali inakusudia kupeleka mswaada bungeni wa madereva wanaoendesha magari makubwa ya mizigo pamoja na abiria, wawe ni wenye umri wa kuanzia miaka 45

Hayo yameswemwa na waziri wa ujenzi na uchukuzi mhandisi Kamwelwe alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa barabara jijini mbeya.

Chanzo ITV
 
Na watawapeleka wapi all employed personnel not qualified under the amendment?
 
Nimemsikia Waziri but sikupata kwanini aseme 45+ je ndio kusema walio between 30-44 hawawezi kuendesha basi?
Vijana walio wengi waendeshe Nini?
 
Kuna wakati hawa jamaa wanajisahau kwenye nafasi zao huwezi niambia kwa sasa mfano nina miaka 35 niache kazi nisubirie mpaka nifikishe miaka 45 Hapo katikati familia yangu nitaipeleka kwake ailishe mpaka hapo nitakafikisha hiyo miaka nitaenda kuwachukua yeye anaongea hivyo kwa kuwa ana uhakika wa kuuza maneno jukwaani akaishi sisi wengine tunaishi kwa kutegemea Huo Udereva Darasa la 7 hamtutaki serikalini tumeokolewa na ajira za mitaani bado napo mnataka kuja kutusumbua mnataka tufanye kazi gani? Tuishi na familia zetu.
 
Back
Top Bottom