Madereva kuweni makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madereva kuweni makini

Discussion in 'Jamii Photos' started by GM7, Sep 8, 2009.

 1. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hili ni eneo la tukio la ajali ya magari mawili kama yanavyoonekana baada ya gari iliyoumia kuingia barabarani ghafla na kugonga na kukata nguo ya umeme. Nguzo hiyo inaonekana nzima lakini chini imekatika kabisa na kusogezwa mbele kama mita moja hivi baada ya kugonga na gari hilo.

  Gari nyeusi ilikuwa inatokea upande wa kushoto mwa picha hii na hiyo teksi iliyobonyea iliingia ghafla barabarani bila kuchukua taadhari na hatimaye kusababisha ajali hiyo

  Kwa mujibu wa walioshuhudia ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa na mashuhuda wa ajali hiyo wanasema dereva huyo wa teksi alikuwa amelewa. Ajali hii ilitokea leo saa 9:30 hivi kama ilivyonaswa na kamera yangu.

  Hii ni ajali ya tatu kutokea eneo hili la IYUNGA JIJINI MBEYA kwa kipindi cha takribani wiki mbili hivi katika eneo hili ambapo kabla ya ajali hii gari moja aina ya Hiace iligonga nguzo inayofuata upande wa kulia (kwenye picha haionekani) na kumjeruhi dereva. Na nyingine ilitokea kama wiki mbili zilizopita baada ya Hiace kugongana na Landrover katika eneo hili hili la Iyunga Mbeya.
  [​IMG]
   

  Attached Files:

Loading...