Madeni Shamte Kipande Akaimu Ukurugenzi mkuu TPA

Jumanho

Member
Sep 14, 2010
37
5
Hongera sana Eng. Madeni Shamte Kipande kwa kuteuliwa kuchukuwa nafasi hiyo nyeti na juu kabisa katika taasisi za umma nchini. Kwa ninavyomfahamu mimi ninauhakika mamlaka ya bandari imepata kiongozi shupavu, jasiri, makini mwenye kuthubutu pia mwenye upeo wa hali juu. Tunatumai utaiongoza mamlaka hiyo kupiga hatua kubwa sana.
 
Ukiwa mkurugenzi wa mamlaka ya bandari hakuna cha ufanya kazi bora wala uadilifu atakula hela kama wenziwe atajijazia mali na fedha ka waliomtangulia mi nampa hongera kwa kupata cheo cha ulaji kwa kua hata wangeniweka mimi ningekula vibaya mno....
 
Ingekuwa ni busara kama unaweka na CV yake wengine hatumfahamu, najaribu kugoogle wap/ hebu weka CV kama vp tumpongeze amala!
 
Mgawe ametolewa nafasi yake imechukuliwa na Eng. Kipande.....

Walikuwa wanamtaka mtu wao sasa wamempata ili waweze kutuibia vizuri na wamepanga akiondoka Kitilya TRA, wampeleke mtu wa sampuli ya Ramadhani Dau ingawa fani yake ni marketing.

Endeleeni tu kuigawa hii nchi kwani matunda ya sera zenu chafu mmeishaanza kuyaona kwenye sensa.
 
This Day Magazine: Just In: Dkt. Mwakyembe amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bandari
ust In: Dkt. Mwakyembe amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bandari




Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.

Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wwadao wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na inami na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.

Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.
16511139-3627462532208271623
 
Huyu kipanda siyo yule aliyekuwa tanroads? Alianza kama rural road engineer-mbeya, regional engineer-kilimnjaro, baadaye mkurugenzi wa mizani -tanroads. Si-comment chochote, lakini nyie mnafahamu yaliyojiri huko mizani
 
Huyu kipanda siyo yule aliyekuwa tanroads? Alianza kama rural road engineer-mbeya, regional engineer-kilimnjaro, baadaye mkurugenzi wa mizani -tanroads. Si-comment chochote, lakini nyie mnafahamu yaliyojiri huko mizani

Kama ni huyu 'kichaa' bandarini habaki mtu.Aliwahi kumtupia mwarabu dola zake laki 1 usoni na kumfukuza kama mbwa...kisa mwarabu kapigwa faini milioni 400 kwa kuzidisha uzito.

Pia Azim dewji na boti zake 2 zilizidi upana na uzito zilikua ziende ziwa victoria kwa malori kisha zitoswe majini...jamaa alitia ngumu hadi waziri mwandosya kaja lakini wapi...kila ajaye anamfunulia vifungu vya sheria.ilibidi muhindi apele boti mombasa kwa bahari
 
Huyu kipanda siyo yule aliyekuwa tanroads? Alianza kama rural road engineer-mbeya, regional engineer-kilimnjaro, baadaye mkurugenzi wa mizani -tanroads. Si-comment chochote, lakini nyie mnafahamu yaliyojiri huko mizani

Kwenye red hapo ni Kipande, Hapo kwenye red ya pili hajawahi kuwa mkurugenzi wa mizani tanroads, bali ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Ujenzi nafasi ambayo alikuwa anaishikilia mpaka anateuliwa kuchukua nafasi hii ya sasa. Ila haswaa ni huyo unaemfahamu
 
mnh. Tanroad nayo inaweza ikatoa mtu makini na malosoloso yote haya nnayo yafahamu mimi??
 
Hapo ndipo huwa naiona vita dhidi ya ufisadi inayoendeshwa na hawa magamba ni usanii mtupu. Kwanza Hosea alikuwa wapi siku zote? Hakuzijua tuhuma hizi na kuwakamata mara moja akina Mgawe na kuwapeleka mahakamani?

Pili hao wachunguzi aliyowateua Mwakyembe, jee wamepewa hadidu za rejea za kuchunguza akaunti za benki na mali za watuhumiwa na kuzikamata mara moja?

Mie naona ni usanii mtupu!!!!
 
Back
Top Bottom