The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,778
- 8,209
Kila Binadamu katika safari ya maisha hukutana na hali ya madeni iwe ni madeni ya pesa, ahadi, au hata madeni ya kihisia.
Mara nyingi, deni huanza kama msaada wa haraka, ahueni ya muda mfupi, au njia ya kujinusuru. Lakini kwa undani zaidi, deni linaweza kuwa mnyororo unao ifunga roho yako kimya kimya, mnyororou naojificha kwenye sura ya matumaini lakini taratibu ukifungwa bila kujitambua
Madeni mengi huanza kwa hisia ya matumaini. Unapokuwa katika hali ya changamoto, deni huonekana kama taa ya mwanga katika giza. Huamini kwamba
Ukikopa kidogo, biashara itafufuka.
Ukilipa hili deni haraka, mambo yatanyooka.
Ukijikwamua mara moja, hutahitaji tena kukopa.
Lakini mara nyingi, haya ni matumaini ya bandia yanayotokana na haja ya haraka, si hekima ya ndani. Hapo ndipo unapo anza kujifunga mnyororo huu taratibu tena kwa upole shingoni – bila wewe kutambua.
Baada ya kupata deni la kwanza, wengi huanza kuamini kuwa njia ya kutoka ni kukopa tena. Unataka kulipa – lakini hauna. Unahitaji kuendelea – lakini mtaji haupo. Ndipo unakopa kulipa deni jingine.
unapojaribu kutaka kujinasua kwa kukopa tena,n ndipo upo anza najifunga zaidi. Unakuwa kama mtu anayezama kwenye mchanga kadri unavyojaribu kutoka kwa nguvu zako mwenyewe, ndivyo unavyo zidi unavyozama zaidi.
Katika hali ya kupoteza, kuna hamu ya kulazimisha mambo yaende kwa nguvu kuzuia biashara isife, kuzuia duka kufungwa, au kazi isiharibike. Ndipo mtu huchukua mikopo zaidi, au hufanya maamuzi ya haraka kwa hofu ya kupoteza kila kitu.
Unapolazimisha jambo kwa hofu, unalikuza badala ya kulitatua.
Unapotumia nguvu kuzuia jambo linaloondoka, unalipa gharama kubwa – kiakili, kiroho na kimwili. Tatizo linapanuka kadri unavyolipinga kwa nguvu zisizo na mizani.
deni si tatizo la kiuchumi pekee. Ni ishara ya ndani kwamba mtu hajajifunza kutulia kwenye wakati alio nao sasa, hajajua kusubiri mzunguko wa maisha, ama huja kwa kuto ruhusu sauti yako ya ndani kukuongoza.
Mara nyingi mtu mwenye deni ni ishara ya aliyekata tamaa kwa ndani.
Anayetafuta suluhisho kwa njia ya muda mfupi badala ya kuruhusu sauti yake ya ndani iongee
anayepingana na mabadiliko badala ya kuyakubali kama sehemu ya safari yake.
Deni ni kielelezo cha mtazamo ulioharibika, siyo tu hali ya kukosa pesa.
Usijidanganye wala kujisingizia. Hali uliyo nayo ikubali wa uhalisia – hii ndiyo hatua ya kwanza ya ukombozi.
Badala ya kutafuta mkopo mwingine, tafuta njia ya kurudi ndani yako tafakari, omba hekima, punguza matumizi, acha kuficha hali yako.
Ukimya unakupa mwanga. Katika ukimya ndipo majibu huzaliwa na si katika makelele ya mawazo ya haraka au presha ya watu.
Labda biashara ilifeli kwa sababu ilikuwa nje ya msimu wako wa kiroho. Labda ulikopa kwa sababu hukujua zaidi. Samehe nafsi yako. Sasa jifunze, tulia, na jenga upya kwa msingi bora.
Kujinasua kutoka kwenye madeni kunahitaji zaidi ya pesa kunahitaji mwamko wa ndani, uelewa wa kiroho, na ujasiri wa kukubali hali. Ukishakuwa huru ndani yako, hautafungwa tena na deni lolote la nje. Utaishi kwa imani, kwa hekima, na kwa utulivu.
Mtu aliye huru ndani yake hawezi kufungwa na mnyororo wa nje.