mademu wa kizungu hawapigi mizinga kama wakibongo?

mademu wa kizungu hawapigi mizinga kama wakibongo?

Me nna girlfriend kutoka usa, mara ya 1 kutoka out nikataka kulipa akakataa hvyo akalipa nusu nami nusu. Licha ya kulazimisha nilipe yote alikataa. Nikamwambia huku bongo wanaume ndo tunalipa, akanambia yexe si mbongo. Kwa hyo tumeshazoea kila tukitoka out wakat wa kulipa me namtania kwa kumuuliza "Bongo style or american style" anachagua american style. Hivyo ndo walivyo wenzetu.
 
Kwani haki sawa inayoimbwa kila kukicha na wanawake ni magumashi?.

Hakuna kitu kinachoudhii kama kuwa na mwanamke ambaye anafikili kukupa penzi ni favor na akifanya hivyo basi lazima liambatane na malipo.

Kwa nchi za magharibi, mizinga mara nyingi inakuwa kwa watu weusi na wazungu wachache.
 
Nimeangalia muvi nyingi za
hollywood za mapenzi sijawahi kuona demu akimpiga mzinga bf wake.
Atapigwa mti na kusepa bila kuomba nauli wala hela yya matumizi sijui
hela ya saluni. Au watatoka out kula kila moja atalipa.
Hii tabia ya kuombaomba mademu wa bongo wameiiga wapi? Maana ukilala
naye lazima akupige mzinga kama kakuuzia. Mbona wabongo mnalaana hv kila
ubaya mnao nyie. Bora mtu uchukue wanaojiuza rasmi kona baa ujue
moja.

Wapo mkuu wanaopiga mizinga,we unazungumzia movie....! njoo hapa A town kuna kijiwe kimoja ni balaa. mademu wa kitasha wanapiga mizinga balaa
 
nahisi wafafanua mada wakuu bado wamefungiwa fungate ya weekend...!!tufanye subira..
 
Watakuwa wamefundishwa na wanaume wa kibongo. Wakaka wa kibongo kwa mizinga wameshindikana! Anakufukuzia huku anapiga mizinga. Nahisi wakaka wa kizungu hawapigi mizinga.
 
Nacho kiona ni utamaduni tu na hali ya uchumi kwa jumla nimeshashuhudia siyo mwanamke tu hata wakikutana wazungu wanaume labda ktk lunch baada ya mlo kila mtu anatoa kiasi kuchangia malipo na hiyo ni utamaduni wa kuwajibika walio nao na hili lipo ktk maisha yao kwa ujumla iwe ofcn, biashara n.k tatizo kwetu dhana ya kuwajibika bado mtihan ktk nyanja zote ukiunganisha na mambo ya mapenzi

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom