Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria kupitia ACT Wazalendo, Peter Madeleka, amesema kuwa serikali iliyoko madarakani sasa itafikia kikomo cha uhalali wake mwezi Oktoba mwaka huu, na hivyo Watanzania wana jukumu la kuunda serikali mpya kupitia uchaguzi.
Julai 4, 2025 akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Busega, mkoani Simiyu, Madeleka alisisitiza umuhimu wa kushiriki uchaguzi kama njia ya kidemokrasia ya kuleta mabadiliko ya kweli.
"Serikali tuliyonayo leo hii itamaliza uhalali wake mwezi wa kumi. Tunao wajibu wa kutafuta Serikali nyingine. Serikali hiyo tutaipata kwa njia ya uchaguzi. Uchaguzi ni haki ya kidemokrasia. Anayekwambia usishiriki uchaguzi hakutakii mema," alisema Madeleka mbele ya umati wa wananchi waliojitokeza.
Ameonya kuwa wito wa kususia uchaguzi una manufaa kwa chama tawala pekee na unadhoofisha juhudi za kidemokrasia za wananchi.
Hotuba hiyo imekuja wakati ambapo mjadala kuhusu ushiriki wa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu ukiendelea kushika kasi. ACT Wazalendo wamesisitiza dhamira yao ya kushiriki kikamilifu ili kuzuia kile wanachokiita "utawala wa mabavu bila ridhaa ya wananchi."
Viongozi wa ACT Wazalendo wanaendelea na Operesheni yao waliyoiita Majimaji katika mikoa mbalimbali kueleza msimamo wa chama chao na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi.