Madee mwanamuziki wa midundo ya bongo flavor amekufuru kwenye wimbo wake anaosema amepata mateso makali kuliko ya Yesu.
Wakristo wanaamini kuwa hamna mtu amewahi kuteswa kama yesu. Madee akiwa ni muislamu, hakupaswa kulinganisha taabu zake na mateso ya yesu.
Madee amekufuru.
nyie vipi kwani yesu nani? hebu nipisheni hapa.....yesu si alikuwa binadamu kama sisi tu au
Watu wa aina hii ingepaswa wawe na wahariri wa mashairi yao maana hawajui impact ya matamshi yao,wanachoangalia ni ku-balance vina vya mashairi ya wimbo tu.
Kila kinavyoimba na wasanii,au kuandikwa na wana fasihi ukikichukulia kwa juu mm naamini usengekuwa unasoma au kuckiliza nyimbo zao,kazi ya fasihi iache ichukue nafasi yake,kwangu mm madee hana maana ya mtoa mada kijana unapoaelezeea mateso makali kuliko yote ni ya yesu kristo so jamaa anajalibu kuelezee mateso kwa maana ya mateso,na anajaribu kufikisha ujumbe tu na wala hana maana ya kikanisa au kimsikiti,na unaposema yy muislam mm sikuelewe cos hata waislamu wanamjua masii kama nabii wao.so usijali kutoa tasfiri ya juu juu ya kazi ya sanaa
Mkubwa kila music unawatu wake na una maana yake na mtu sahihi wa kutoa tafsiri nzuri wa alichokiimba ni madee mwenyewe,bado dogo ana haki kuckilizwa na sio kuhukumiwa tu,hata ng'ogi wa thiongi anasema unaposoma kitabu chake mwanzo mwisho na uelewi dhima ya kitabu chake acha cos ww sio hadhira wake.so even music ukickiliza uelewi tafuta music mwingine unaweza elewa zaidi,sory ni maoni tuUsitake kutetea kisichostahili kutetewa. Mbona unataka kuhalalisha visivohalalishika?
kama kawaida; hawa vijana wanaovaa suruali zipo chini ya ****** na hereni kama mashoga halafu wanajiita wasanii wa bongo fleva asilimia kubwa huwa hawafikirii kabla ya kutunga nyimbo zao! Huo wimbo umelengwa kwa jamii, lazima ajue Tanzania ni nchi ya wakristo wengi, na zaidi wimbo wake unategemea kwenda nje ya mipaka ya nchi; YESU kwa wakristo ni zaidi ya nabii, ni MUNGU! Kwa wakristo hakuna mtu wa kumfananisha na YESU na hakuna mwanadamu katika dunia hii atakayeweza kustahimili mateso aliyoyapata yesu!! Huyu Madee yeye lishawahi kuchapwa mijeledi na Wayahudi? (si ajabu hata viboko vya shule ya msingi hajawahi kuvionja) Amewahi kuchomwa mkuki huyu? (zaidi ya sindano za chanjo na alipokuwa anaumwa malaria tu)...na je, ALISULUBIWA WAPI Madee?? (kama kweli mateso yake ni zaidi ya Yesu)...Asichezee imani za watu wengine
Kila kinavyoimba na wasanii,au kuandikwa na wana fasihi ukikichukulia kwa juu mm naamini usengekuwa unasoma au kuckiliza nyimbo zao,kazi ya fasihi iache ichukue nafasi yake,kwangu mm madee hana maana ya mtoa mada kijana unapoaelezeea mateso makali kuliko yote ni ya yesu kristo so jamaa anajalibu kuelezee mateso kwa maana ya mateso,na anajaribu kufikisha ujumbe tu na wala hana maana ya kikanisa au kimsikiti,na unaposema yy muislam mm sikuelewe cos hata waislamu wanamjua masii kama nabii wao.so usijali kutoa tasfiri ya juu juu ya kazi ya sanaa
Nabii Issa ''masii" wa waislamu ni tofauti na Yesu Kristo wa wakristo. Kwa hiyo epuka kuandika maneno ya kusikika, katafute msaafu wa waislamu na biblia ya wakristo soma watu hawa wawili. Aliyepo wa waislamu ni upotofu kwa yule anaye elezewa wa wakristo.
Nafikiri ndo zake, hapimi uzito wa mistari yake. si ndo yeye kaimba Yote Maisha wakiwa na Majani - kuna mstari unasema;
"asante Mola napumua bila ushuru, ila sishukuru si bora ungeniumba tu kunguru" Huo wimbo naupenda sana ila nikifika hapo naboreka kabisa.
Misanii mingine inaimba ili mradi ipate vina.
Mf. kuna kundi flani waliimba.."MUNGU SI ATHUMANI WALA DEFAOO....BABA JENI ALIPOPATA MAFAOO...
Yani ilimradi tu.
Nimesikia eti amekulia Manzese,
amesoma primary school manzese, na hupendelea kushinda Manzese.
Hata hivyo Manzese wapo wastaarabu wengi tu ila yeye kampani yake ni
wavutaji wa ile sigara inatoa moshi mzitoo, mkalii.