Madawa ya Kulevya: Kumbe Makonda Alizuiwa Kutaja Majina!. Anaamini Uwazi, Atunge By-Law Ataje Majina

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,650
119,257
Wanabodi,
Kiongozi yoyote akilitenda jambo analoliamini, litafanikiwa sana kwa sababu utekelezaji wake utakuwa unahusisha the powers of will, kulifanikisha na kutekeleza jambo usiloliamini ni failure before the start.

Hivyo ndivyo alivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anaamini katika ukweli na uwazi kwa kutaja majina ya washukiwa wa madawa ya kulevya, kuwa expose jamii iwajue, lakini inaonyeshwa amelazimishwa kwa kunyamazishwa na kutakiwa kukabidhi majina ya wahusika bila kuwataja.

Hili ni bandiko la ushauri kwakwe kwamba he must do what he believes. Kama serikali kitaifa imemzuia, yeye kama Mkuu wa Mkoa ni rais wa Dar es Salaam, anayo serikali yake ya mkoa yenye bunge lake, lenye mamlaka kamili ya kutunga sheria ndogo, by-laws, ili kumruhusu kuendelea kutaja majina ya watuhumiwa wa mkoa wake only if hizo by-laws hazitakinzana na sheria mama.

Kumbe ile siku anakabidhi yale majina ya watuhumiwa wa awamu ya tatu, alikabidhi kwa shingo upande, alipanga awataje kama mwanzo lakini alipigwa stop, hivyo kulazimika kukabidhi fail bila kuwataja majina na ingekuwa Kamishna yuko chini ya amri yake, angemuamuru ayataje hayo majina kwa sababu yeye Paul Makonda anaamini katika kupigana vita vya wazi na kwa kelele ili kila mtu asikie ni more effective kuliko silent war!.

Hayo yamethibitishwa leo asubuhi na Paul Makonda mwenyewe, baada ya kumpigia simu mtangazaji wa Clouds TV, Baby Kabae wa kipindi cha 360 Degree, na kumjulisha leo ni siku yake ya kuzaliwa hivyo kuomba apaishwe hewani kuna jambo anataka kulisema.

Muda muafaka ulipofika Baby Kabae akampandia kwa simu na kumuweka hewani mubashashara, kwanza kwa kumuwish happy birthday na kisha kumuuliza ni jambo alitaka kulisema kuhusu vita hii ya madawa?.

Ndipo Makonda akafunguka kwa kusema wazi kuwa yeye ni muumini wa ukweli na uwazi na sio katika usiri, hivyo anaamini katika vita vya wazi, na kuuliza kwa miaka 40, vita hii imekuwa ikipiganwa kimya kimya kwa usiri, jee imeleta manufaa gani kulinganisha na vita ya wazi? .

Hii inamaanisha hata yale majina ameyatoa shingo upande. Alitaka kuyatangaza.

Ushauri kwa Makonda, yeye kama mkuu wa serikali ya mkoa, ana mamlaka kamili ya kutunga sheria ndogo, by laws, kupitia mabaraza ya madiwani kuwa washukiwa wote wa madawa ya kulevya jiji Dar es Salaam, watangazwe wazi kwa majina only if kama sheria mama haijazuia kutaja majina.

Kwenye serikali za wenzetu, if you don't believe in something, you just say so, there and then na kuwabwagia barua yao, na sio kukabidhi majina kimya kimya huku you don't believe in silence and confidential kisha kwenda Clouds TV na kusema you don't believe!.

Happy Birthday Paul Makonda.

Paskali.
 
By-laws hazitakiwi kuzi violate sheria mama......kama sheria mama inasema hawatakiwi kutangazwa basi by-laws zinatakiwa ziulinde msingi huo......by the way Jiji lipo chini ya madiwani na meya wa ukawa ambao Mwenyekiti wao Mbowe ni victim wa huu upuuzi wa Makonda unategemea watakubali????
 
Kuwataja proved very effective.Hii ya kimya kimya ni mkakati mahsusi wa kurudisha nyuma juhudi za Makonda. Nimechukia sana.
Vita vya kimya huwa ni loop hole ya kukwepea mkono wa sheria. Tutajuta kuua hata hiki kidogo alichoanzisha Makonda. Sasa tunarudi kwenye business as usual na huyoe"man of principles! "
 
Sasa kimetokea nini mpaka kufikia kutokutaja majina mubashara kama tulivyomzoea Hali hiyo imekuja ghafla kunani hapo au michango mbalimbali ya wachangiaji imemfanya au imemshtua atambue kuwa sheria inamkataza kufanya hivyo au nini kimetokea? Na wale aliokwisha waanika matokeo yake ni nini?
 
Kama makonda anaona ametendewa ndivyo sivyo kwa kuzuiwa kusoma majina ya watuhumiwa wa mihadarati hadharani amkabidhi tu aliyemteua barua ya kuachia ngazi. Kulalamika kwenye vyombo vya habari siyo hatua stahiki.

Yeye anaamini katika uwazi wakubwa wamemziba mdomo...cha kufanya awaonyeshe wakubwa kuwa hakubaliani nao kwa kujiuzulu. Akifanya hvyo wafuasi wake watamuheshimu sana na historia itamkumbuka.
 
mkuu, Paskali. ufisadi ni twin brother/sister wa unga business.

kwa hiyo kuwe na level play field kwenye vita vyote viwili. yeye anataja wenziwe kwa unga, wanawekwa sentro. yeye anatajwa kwa ufisadi, ajiweke ndani pia.

all square!
 
Kama makonda anaona ametendewa ndivyo sivyo kwa kuzuiwa kusoma majina ya watuhumiwa wa mihadarati hadharani amkabidhi tu akiyemteua barua ya kuachia ngazi. Kulalamika kwenye vyombo vya habari siyo hatua stahiki.

Yeye anaamini katika uwazi wakubwa wamemziba mdomo...cha kufanya awaonyeshe wakubwa kuwa hakubaliani naona kwa kujiuzulu. Akifanya hvyo wafuasi wake watamuheshimu sana na historia itamkumbuka.
Well said
 
Back
Top Bottom