Madaraka ya spika wa bunge

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,358
6,422
Watanzania tumeona jinsi spika Anna Makinda ambavyo amekuwa akizima hoja zenye umuhimu katika taifa letu. Tumejifunza mengi kuhusu madaraka ya spika kipindi hiki cha Anna Makinda. Definitely waliokuwa wanatoa hoja za kulinusuru taifa hili ni wapinzani particularly CDM.
MAONI YANGU: KUNA HAJA YA KUAINISHA MADARAKA YA SPIKA-
1. mfano, ikiundwa kamati, isiwe discretion ya Spika kutoa taarifa hiyo kwa umma/wabunge wenzake, bali iwe mandatory kuiweka wazi.
2. Spika asiwe Spika Mfalme !!! Kwa sasa ilivyo, ndani ya Bunge spika ni Mfalme!
3.Amekataa miongozo mingi toka kwa wapinzani-bunge la vyama vingi lina haja ya kuangaliwa kanuni za uendeshaji wake
4. etc, etc, etc, etc
 
Mkuu nakuunga mkono asilimia mia moja.Madaraka ya spika ni makubwa mno,mfano kutangaza matokeo ya uchunguzi wa kamati inategemea ridhaa ya spika au hata kuamua kama taarifa ya kamati ijadiliwe au isijadiliwe bungeni.Huu ni upuuzi wa hali ya juu na tukumbuke ni kodi zetu ndio zinatumika kugharamia kamati hizo alafu mtu anaachwa aamue jinsi anavyotaka bila kuwa na sheria ya kumbana.Cha ajabu wabunge nao wameridhika na upuuzi huu.Inakera sana na kuuzi.Sijui ni wasomi wa ain gani tulionao bungeni.

Mapungufu ya katiba wanayaona ila yanayohusu kanuni,taratibu na sheria za kuendesha bunge hawayaoni!

Swali: sheria na kanuni za kuendesha bunge ni sawa na msaafu au biblia?
.
 
Sidhani kam tatizokubwa ni kanuni. Nafikiria kubwa ni kuwa bunge letu bado ni la Chama kimoja. Tutakapokuwa na iwakilishi wa kutosha kutoka zaidi ya Chama kimoja Spika hatakuwa na cha kufanya bali kutoa haki na kufuata matakwa ya Wabunge na wananchi. Kwa sasa Kanuni zinatafasiriwa apendavyo au Chama/ serikali yake inavyotaka - kulinda maslahi Yao.
 
Back
Top Bottom