Madaraka: Taifa limeshindwa kumuenzi Nyerere

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
MTOTO wa Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere amesema taifa linayumba kutokana na viongozi wengi kutumia nafasi zao kujilimbikiza mali kutokana na kukiuka miiko ya uongozi iliyoasisi na Mwalimu Julius Nyerere. Hali hiyo imesababisha uchumi kuhodhiwa na watu wachache huku umaskini ukiongezeka kwa Watanzania.

Kauli ya Madaraka inakuja wakati Watanzania wakiungana kukumbuka kifo cha Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 13 iliyopita mjini London Uingereza. Katika andiko lake alilotuma kwa Mwananchi Jumapili, Madaraka alisema kuachwa kwa sera ya Ujamaa na Kujitegemea na uchumi kuwa mikononi mwa wachache kumeifanya Tanzania ishindwe kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo.

“Zamani kulikuwa na miiko ya viongozi ambayo iliwataka wasijihusishe na biashara, lakini sasa ni tofauti. Nawaomba Watanzania katika mchakato wa Katiba Mpya wachangie mawazo ambayo yataleta faida kwa umma kama Mwalimu Nyerere alivyopigania wakati wa uongozi wake,” anasema.

Madaraka alisema anasikitishwa na baadhi ya viongozi wanaotamba hadharani kwa utajiri walionao huku wakibeza familia ya mwasisi wa Taifa, Mwalimu Nyerere kutokana na umaskini wao.

Madaraka: Taifa limeshindwa kumuenzi Nyerere
 
Me naona utabiri na laana ya baba wa taifa nyerere imetimia maana nakumbuka mwaka 1995 nyerere alimkatalia Vasco Da gama kugombea urais na kumwambia hawezi kuongoza nchi kwa sababu kazi ya kuongoza nchi ni ngumu,nadhani Vasco Da gama anaona jinsi kazi ya kuongoza nchi ilivyo ngumu,nchi inataka kugawanyika kwenye udini mikononi mwake.
 
Mimi ninacho kumbuka Mwl alisema yeye "Yai bovu analitambua" mwisho wa kunukuu, na jingine alilosema ni mtoto akililia wembe mpe, ukisha mkata ndio ataelewa, machungu na matamu ya wembe
 
Back
Top Bottom