Madaraka kwa wananchi

Kikusya

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
266
365
Hili ni wazo jipya la kuishauri serikali, kwa sababu hii nchi ni kubwa, kuwe na dawati la kero mtandaoni kwa kila wilaya. Hii itasaidia viongozi wa juu kuona live kupitia mtandao kero za wananchi mojamoja bila kupitia kwa wakurugenzi au kwa viongozi wa wilaya.

Hii ni dawati huru la wananchi kutoa kero zao. Kiongozi anaweza kupitia dawati hili hata kabla ya kwenda eneo husika.

Ni vigumu kwa Raisi au waziri kujua kero za wananchi kila wilaya. Mara nyingi viongozi wanategemea kupewa maelezo toka kwa viongozi wa wilaya pale wanapokuwa ziarani, kwa hiyo kwa kutumia dawati hili huru kiongozi anakuwa na uelewa wa changamoto zinazowakumba wananchi.

Kwa mfano, unafungua hilo dawati wilaya ya Rungwe, humo utakuta kero za Rushwa, uzembe, uwajibikaji na uwizi , ufujaji wa mali za umma.

Itasaidia kupunguza wale viongozi wenye uchu na mali ya umma, udokozi kila kukicha.
Miaka nenda miaka rudi hatupigi hatua za maendeleo kwa kasi kwa sababu ya hizi tabia.

Kwa kifupi wakati umefika kwa sisi wananchi kuweze kuwasilisha kero zetu, ambazo zitasomwa na Raisi, waziri mkuu moja kwa moja.

Ahsante nawakirisha wananchi wanyonge.
 
Shida sio uwasilishaji wa kero bali shida kubwa ipo kwenye Utekelezaji wake na Vipaumbele vya mahali husika.

Ukiishi Oysterbay unaweza kujua kero za tandale na Mabibo sokoni lakini huwezi kufanya chochote chenye tija na mabadiliko.
 
Back
Top Bottom