Odense
JF-Expert Member
- Nov 3, 2020
- 2,661
- 3,455
StressDuuh! Mbona jamaa kauliza swali simple tu lakini watu mnatoa kashfa badala ya majibu
StressDuuh! Mbona jamaa kauliza swali simple tu lakini watu mnatoa kashfa badala ya majibu
Hii ndio Afrika mkuu na watu wameridhika kabisa. Umasikini tumeufanya ni sifa. Ukiwa huna kazi hiyo pesa ni nyingi sana inakuwa ndogo ukiwa na kibarua kwa hapa bongo.Hii nchi bado ni maskini sana aiseeh basi tu. Mtu anahangaika miaka yote shule na university anatoka na degree yake then anakuja kulipwa 765,000/- kwa mwezi mzima?! This is equivalent to 293 USD. Binadamu anawezaje kuishi kwa USD 293 kwa siku 30?! Na huyu ndo anasemakana kasoma adi degree, ambao hawajasoma wako mtaani wanaishije?! Walioko vijijini je?! Kuna nchi nilikua naprocess visa ya kwenda huko kiwango cha chini cha pesa unayotakiwa kua nayo kwa mwezi kijikimu kimaisha ni 800 EUR hii ni kama 2.4M hivi kwa pesa za Tz. Kuna nchi Africa tu hapa kila raia ambae hafanyi kazi analipwa kima cha chini cha wafanyakazi wa kawaida serikalini ama sekta binafsi, bima ya afya kwa wote na elimu bure adi chuo kikuu. Watumishi wanalipwa minimum salary kulingana na hali ya uchumi. Calculations zote zinafanyika kitaalamu kiasi ambacho pesa anayolipwa mtu itatosha kikidhi mahitaji halisi ya kibinadamu.
Ajira mpya atakaa mwaka 1 wa KUTHIBITISHWA. Kisha miaka 3 ya kutumikia cheo. JUMLA 4, atapanda kutoka TGS D1 kwenda TGS E1.Wakuu naomba kuuliza swali. Rafiki yangu amebahatika kupata ajira za utumishi katika wizara ya kilimo baada ya kuhangaika sana na usaili kila mwaka.
Ameajiriwa katika ngazi ya bachelor's degree, na daraja la mshahara aliloanza nalo ni TGS D.1, yaani atakuwa anapokea 765,000 TZS kama gross salary. Swali ni kwamba, je inachukua muda gani kupanda daraja kwenda mfano TGS D.2-D.12 au kupanda kabisa kwenda TGS E ?
Je ni vigezo gani huhitajika katika kupandishwa daraja la mshahara? Je atahitaji kwanza kwenda kusoma masters degree ili kupanda au ni huangaliwa muda wake katika utumishi? Na ni nani anayeamua mpandisha mtumishi daraja la mshahara?
Hii tabia ya kila mtu akileta uzi humu kusema rafiki yangu, mtu wangu wa karibu, jamaa yangu inatokana na nini, kwani ukisema niwewe kuna shida ganiWakuu naomba kuuliza swali. Rafiki yangu amebahatika kupata ajira za utumishi katika wizara ya kilimo baada ya kuhangaika sana na usaili kila mwaka.
Ameajiriwa katika ngazi ya bachelor's degree, na daraja la mshahara aliloanza nalo ni TGS D.1, yaani atakuwa anapokea 765,000 TZS kama gross salary. Swali ni kwamba, je inachukua muda gani kupanda daraja kwenda mfano TGS D.2-D.12 au kupanda kabisa kwenda TGS E ?
Je ni vigezo gani huhitajika katika kupandishwa daraja la mshahara? Je atahitaji kwanza kwenda kusoma masters degree ili kupanda au ni huangaliwa muda wake katika utumishi? Na ni nani anayeamua mpandisha mtumishi daraja la mshahara?
Tulishadanganya kwenye forum X kwamba tunauza magari, sasa huku tukija front ile CV fake inaweza ku shake.Hii tabia ya kila mtu akileta uzi humu kusema rafiki yangu, mtu wangu wa karibu, jamaa yangu inatokana na nini, kwani ukisema niwewe kuna shida gani
Mtumishi wa umma unaupiga mwingiNimerudi tena.
Ipo hivi mkuu, suala la kupanda madaraja kwenye utumishi wa umma ni haki ya kila mtumishi baada ya kutimiza wajibu wake. Mfano ukiajiriwa na daraja TGS D.1 hapo unatakiwa usubiri baada ya miaka minne kwenda TGS E. Kwa maana ya mwaka mmoja wa matazamio (probation) kisha miaka mitatu ya utendaji kazi, ila katika kipindi hicho cha miaka mitatu unatakiwa kuhakikisha unafanyiwa tathimini na kupata alama nzuri na supervisor wako, kwa mfumo wa zamani ni OPRAS ila mfumo mpya wa kidijitali unaitwa PEPMIS.
Madaraja kama D.2, D.3, D.4 ..... D.12 hayo yanatokana na increments za kila mwaka kulingana na sera za utumishi, pia unatakiwa kuhakikisha unatekeleza majukumu yako vema kwenye tathmini za PEPMIS au OPRAS ili uweze kupata hizo increments kila mwaka. Hivyo utaenda D.2 kisha D.3. Ikifika mwaka wa kupanda daraja, ambapo ni kila baada ya miaka mitatu utaenda TGS E baada ya miaka mitatu mingine utaenda TGS F.
Kwa watumishi wenye elimu ndogo au vyeo ambavyo daraja la mwisho ni TGS D hao wamefika ukomo wa madaraja yao wataendelea na increments D.4, D.5, D.6 mpaka D.12 kisha watakomea hapo. Kuna madaraja ili kuyafikia unatakiwa kuwa na kiwango fulani cha elimu. Mfano kufika TGS H hadi TGS I unapaswa uwe na elimu fulani (maybe master).
Ndio maana kuna walimu wapo shule ya msingi wana mishahara hadi Tsh. milioni 3 (TGS I) kwa mwezi.