Madalali wa nyumba,viwanja wasajiliwe

moma2k

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
1,091
1,404
Biashara ya udalali wa kuuza/kununua nyumba,viwanja nk inafanyika kienyeji na kiholela na watu wasio na usajili wowote.

Serikali haiwafahamu. Hivyo hawalipi kodi. Biashara hii ya hovyo haiwapi usalama wa kisheria wananchi(legal protection).

Aidha, hao madalali wasiojulikana kisheria wamekuwa wakipandisha bei ya nyumba, viwanja n.k. kadiri wanavyojisikia, na hivyo kuwaumiza wananchi(bona fide citizens). Hali hii inachangia maisha magumu kwa wananchi.

Hivyo basi:
1. Itungwe sheria ya ku-regulate biashara hii ya madalali.
2. Madalali wote wasajiliwe.
3. Madalali hao walipe kodi
4. Zitengenezwe Code of Conduct kwaajili ya madalali hao
5. Asimilia ya pato lao iwekwe kisheria.
 
Mkuu kuna sheria mpya inaandaliwa, muda wowote muswada wake utapelekwa bungeni kusomwa,...itawalazimisha madalali kusajiliwa kwa level ya mtaa/kata/wilaya/mkoa na taifa. Na pia watatakiwa wawe na taaluma husika kutoka vyuo vinavyotambulika.
Ubabaishaji ulizidi na serikali inakosa mapato huku wananchi wakiumia.
 
ni kweli hawa madalali wanaweza hata kutuletea maagaidi kirahisi maana wao wanaamini tu kupata mtu mwenye pesa nyingi pia wanaongeza ghaarama ya vyumba
 
Nakubaliana na mtoa mada. Madalali wakisajiliwa watakuwa wanatambulika kisheria hivyo kutakuwa na faida zifuatazo
1. Itapunguza utapeli na ubabaishaji.
2. Itasaidia kuzuia mfumuko wa bei na kodi za pango.
3. Watalipa kodi kwa serikali. Kama serikali ikitaka kufanya hivyo maana wanapata kipato kikubwa kupita kima cha chini cha mshahara wa mtumishi wa umma.
4. Itawasaidia kuunda taasisi zao ambazo zinaweza kuwasaidia kupata mikopo, kuweka akiba nk......
5. Itawarahisishia wanaohitaji huduma yao kupatikana kwa urahisi.
6. Itapunguza migogoro kati ya mpangaji na mwenye nyumba hususani kwenye pango (kodi ya nyumba)
7. Itaisadia serikali kujua kiwango cha fedha mwenye nyumba anachopokea kutoka kwa mpangaji wake. Hii itasaidia serikali kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato (tax base) kwa kumtaka mwenye nyumba alipe kodi kwa kuwa anapokea kipato. Japo ni ngumu kiutekelezaji lakini tax base yetu bado ipo chini sana na kuna vyanzo vingi havitumiwi kama hivi baadhi wabapokea kipato kinachostahili kukatwa kodi lakini hakikatwi. Kwa mfumo huo Mpangaji anaweza ku-withheld asilimia fulani ya fedha kutoka kwa kodi ya pango kabla hajampa mwenye nyumba na kupeleka TRA kama final withholding tax.

kwa kuwasajili madalali inawezesha serikali ijue kiwango cha kodi ya pango kwa kuwa wanawekeana mikataba ambayo itakuwa inatambulika kisheria.

Mwisho kabisa tutambue kuwa madalali ni watu muhimu sana katika kukuza sekta ya huduma nchini, hivyo ni lazima watambulike kisheria na kuwe na sheria zinazowaongoza kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.
 
Back
Top Bottom