Madalali wa Majembe wasimamishwa kukamata daladala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madalali wa Majembe wasimamishwa kukamata daladala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Dec 9, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  12/9/2009
  Na Mwandishi Wetu


  KAMPUNI ya Udalali ya Majembe imesimamishwa kwa muda kuendelea na kazi ya kukamata daladala zinazokiuka sheria ya usafirishaji jijini Dar es Salaam.

  Hatua hiyo imechukuliwa wakati ambapo kampuni hiyo imeleta mvutano mkali na madereva wa daladala jambo ambalo liliwafanya kugoma Jumatatu wiki hii na kusababisha adha kubwa ya usafiri jijini.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi alinukuliwa jana na Redio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC-Taifa) akisema kwamba hatua hiyo ni ya muda tu.

  Alieleza kwamba, lengo la kusimamisha kwa muda operesheni za Majembe ni kutoa fursa kwa wamiliki wa daladala kusahihisha kasoro zao na pengine kupata ufafanuzi zaidi juu ya mkakati huo.

  Madereva wa daladala waliitisha mgomo kupinga kitendo cha Majembe kukamata mabasi yao na kuwatoza faini kati ya Sh100,000 hadi 300,000, kiwango wanachodai kuwa ni kikubwa ikilinganishwa na makosa wanayokamatwa nayo.

  Majembe walikabidhiwa kazi hiyo baada ya kushinda zabuni iliyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

  Majembe wanafanya kazi hiyo chini ya usimamazi wa Sumatra ambao ndio wanaosimamia leseni za usafirishaji jijini.

  Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alipoulizwa na gazeti hili kuhusu hatua hiyo alisema ofisi yake haina taarifa za uamuzi huo.

  Hata hivyo, alisema inawezekana yamefanywa kati ya Sumatra ofisi za kanda ya Mashariki na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kuona adha inayowapata wakazi jijini.

  Juhudi za Mwananchi za kumpata Ofisa Mkuu wa Sumatra kanda ya Mashariki, Walukan Lihamba ziligonga ukuta baada ya kuwa nje ya ofisi yake na alipopigiwa simu yake ya mkononi hakupokea.

  Hata hivyo, mmoja wa maofisa kwenye ofisi hizo alilithibitishia gazeti hili kwamba Majembe wamesimamishwa kwa muda lakini hakueleza wamesimamishwa kwa muda gani.

  "Kinachoonekana ni kwamba hawa mabwana wakubwa wamekutana huko, wala sijui ni wapi, wakakubaliana. Hata maofisa wa Majembe waliofika hapa tumekubaliana wasiendelee kufanya kazi kwa sababu Mkuu wa Mkoa ameagiza." alisema ofisa huyo kwa sharti la kutotaja jina lake gazetini.

  Mwananchi lilipowasiliana na Afisa Uhusiano wa Majembe, George Kyatika, alisema: "Hata sisi tumesikia taarifa hiyo redioni, lakini hatuna maelezo yoyote ya maandishi yanayotuamuru tusiendelee na kazi. Kama mpaka kesho hakutakuwa na taarifa ya maandishi, sisi tutaendelea na kazi".

  Katika hatua nyingine, Kyatika alifafanua kuhusu utozaji wa faini ambazo wamiliki wengi wa daladala wanazilalamikia kuwa ni kubwa ikilinganishwa na makosa wanayokutwa nayo.

  "Katika operesheni hii wajibu wa Majembe ni kusimamia zoezi, kupitia muongozo uliotolewa na Sumatra kwa lengo la kuhakikisha sheria za leseni na taratibu zilizowekwa kwa usafirishaji abiria nchini zinafuatwa kwa umakini".

  Alitaja miongoni mwa faini zilizoorodheshwa kwenye kanuni za leseni za usafirishaji abiria za mwaka 2007, makosa ambayo yanatakiwa kutozwa faini ya Sh100,000 ni pamoja na kutumia lugha ya uhasama au matusi kwa abiria, kuwaziba au kuwazuia kwa makusudi wahudumiaji wengine wa usafiri na kuendesha gari zaidi ya vikomo vya spidi kwa kushindania abiria.

  Alisema makosa ambayo yanatakiwa kutozwa Sh250,000, ni kufanya biashara ya kubeba abiria bila leseni au kibali maalumu.

  Tangu Majembe ilipoanza operesheni hiyo Desemba Mosi, Kyatika alisema tayari imekamata magari zaidi ya 700 kwa makosa mbalimbali na kuyaagiza yalipe faini ofisi za Sumatra.

  Alisema wameajiri vijana 200 ili kuboresha ufanisi wa operesheni hiyo, lakini wamebanwa kutokana na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo.

  Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ufinyu wa barabara na wingi wa foleni unaosababisha askari kusimamia uongozaji wa magari muda mrefu kuliko kufanya ukaguzi.
   
 2. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huu unakuwaje mradi wa CCM?!!!!!!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  uliza sumatra wanajua pesa zinapelekwa wapi ndugu mjini hapa....,
   
 4. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wanatafuta hela za kampeni mwakani
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  ...
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Kwa kifupi serikali imebinafsisha kazi ya polisi! Kweli nchi imeuzwa hii.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hii ni kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa jeshi la polisi, traffic inabinafsishwa kwa sumatra. Ulinzi wa kawaida kwa security companies na sungusungu etc na ulinzi jamii etc wao ( polisi ) wamebakia na press statements tu.
   
 8. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hafadhali maana ni wasumbufu sna watu hawa.
   
 9. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Duh...Majembe...100,000 hadi 300,000...!!!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Dec 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hawa sasa wapuuzi.. kama hadi kazi za Polisi zinabinafsishwa kwanini kazi za Ikulu zisibinafsishwe vile vile?
   
 11. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  I wholeheartedly agree with your assertion. It seems like our government is keen in outsourcing its duties. Let me put it bluntly, Majembe Auction doesn't have neither the expertise nor the constitutional right to enforce our traffic laws. There is a reason the government built a police college in Moshi.


  It is also unconstitutional to allow Majembe to do the police's job. We need prudent attorneys of the likes of ACLU to take these people, who for so long have abused our constitution, to court.
   
 12. bona

  bona JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  nakubaliana na suala la kusimamwisha kwa ii kampuni inayoitwa eti majembe, kutoka kupiga mnada mhadi kua askari wa usalama barabarani, jamani wapi tunaenda? kazi za askari wa usalama barabarani zimrbinasfsishwa? je wanatraining ya kutosha kwa kazi iyo? kwa nini awa majembe wako powerful sana power ii kisheria inatambulika? kitendo cha usalama barabarani ktk jeshi l polisi kinafanya kazi gani kwa sasa? wapunguzwe ili kodi za walalahoi zitumike ktk sekta nyingine!
   
Loading...