Madalali na wapiga debe wapigwe marufuku nchi Tanzania

Madalali na wapiga debe wapigwe marufuku nchi Tanzania

Siku Mungu akikufungulia milango ukaanza kusafiri nchi zilizo endelea utakuta kuna madalali hadi wa madada poa na ukirudi bongo ndo utaelewa kumbe afya pia ni mtaji
 
Umesahau MAWINGA wa Kariakoo. Hao nao ni janga. Wanapandisha bei dukani tena mbele ya mwenye duka. Kile anachozidisha anachukuwa winga. Siwapendi hawa jamaa basi tu.
nimewahi kufanya kazi katika duka la spare za pikipiki kahama mkabala na AC BANK,winga hana anachoiba ndugu zangu. mteja anaandika oda ktk duka letu let say clutch cables 10,wiring10 nk jumla 2m, ktk kufunga mzigo clutch cables na wiring zikakosekana na mteja tumemwandikia bei labda cable elfu moja miambili,wayaring 9000 ikabidi nichukue hela kulingana na bei tuliomwandikia tukahemee duka jirani, duka jirani unakuta bei punguzo ....nimechoka kuandika
 
Sasa wewe hapo haukuwa winga.
Mawinga wanapiga cha juu!
 
Hao watu wamekuwa wasumbufu sana, wezi na wapigaji sana, wamekuwa wakiongeze bei ya vitu hali inayosababisha ugumu wa maisha.

Mfano mpiga debe analipwa kila kichwa anachopeleka kwenye gari hizi pesa zinakuwa za huyo msafiri mfano nauli ingeweza kuwa 10000 inapanda mpaka 12000 ili mpiga debe apate posho yake.

Hivi mtu ambae anasafiri anashindwa kujua kuwa anasafiri kwenda wapi na gari gani mpaka awepo mpiga debe, wengi wa Hawa wapiga ni wezi maana ukikaa vibaya wanakuibia hasa wanapokuwa wanakuzonga zonga pale stendi.

Kundi lingine ni madalali, hawa nao wamesababisha bei ya vitu kupanda sana kwa sababu ya kutaka cha juu kikubwa, mwenye uwanja au gari anaweza kuwa anauza 5M ila dalali akaanzia akataka 9M na akakomaa kweli.

Serikali iwapige marufuku hawa watu maana wanaendekeza uzembe na ni wapigaji.
Ngoja waje upondwe na kukulaani kua unawaonea wivu
 
Unachoongea ni kweli kabisa, mpiga debe au mtu yeyote anayempeleka mteja kwenye booking office huwa anapokea asilimia fulani kutoka kwenye fedha husika ya anayesafiri. Kwa mfano nauli ikiwa ni shilingi 27,000/= mpiga debe yake ni shilingi 2,000/= na office inabaki n shilingi 25.000/=.
Tiketi ya efd wanakukatia ya 27,000 ama 25,000?

Kwamba nauli zilizowekwa za latra zinajumuisha malipo ya dalali ama?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom