Madaktari zaidi ya 80 waliopo MoHSW Centre wahamishiwe wilayani hakuna wanachokifanya pale

shykwanza

Senior Member
Nov 28, 2011
156
30
Inasikitisha kuona Makao makuu ya Wizara inakuwa na Madaktari zaidi ya 80 ambao wanafanya kazi za kisiasa wakati sisi katika wilaya yetu hatuna Daktari( MD) hata mmoja kwani hata DMO aliepo ni AMO inasikitisha sana. Nchi hii haina chembe kabisa ya equity na fairness. Tukijaribu kufikiria kwa kina kama wachambuzi wa mambo inakuwaje Wilayani hakupelekwi Madktari na badala yake wanalundikwa Makao makuu ya wizara ya Afya hii ni aibu. Au kazi yao hao nikusubiri Madaktari Madaktari wenzao wagome na wao wakazibe pengo.

Naimba serikali baada ya kutatua mgogoro wa Madaktari na kuboresha Maslahi ya Watumishi wote wa sekta ya Afya iwapange kazi Madaktari waliopo makao makuu ya Wizara kwenda katika Wilayani kuokao maisha ya ndugu zetu.
 
wapo zaidi ya 80 nimemsikia Dr Mponda Waziri Wa afya akisema kuwa leo amewaagiza kwenda Muhimbili kutoa tiba. Then najiuliza kwanini wao hawagomi? Je wanamishara mikubwa kuliko wenzao wanao toa tiba mahospitali na kama mishahara yao ipo sawa wameridhika nini?
 
Katika kufuatilia mgomo wa Madaktari nimekuja kukugundua kuwa kuna kundi kubwa la Madaktari ambao hawajajihusisha kabisa na mgomo na wengine wamekuwa wanaumpinga vikali mgomo wa Madaktari wenzao. Kundi hilo linaongozwa na Madaktari zaidi ya 80 waliopo makao makuu ya Wizara ya Afya, Waganga Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Hospitali. Naomba kuuliza hivi Madaktari wanaoajiriwa Makao makuu ya Wizara wanalipwa mishahara mikubwa kuliko ya wenzao wanaofanya kazi mahospitalini? na kama mishahara ipo sawa kwanini wao hawagomi? Je wananjia nyingine ya kujiongezea kipato?

Mwisho naitaka Serikali iwahamishe Madaktari hao 80 kutoka Wizara ya Afya makao makuu na kuwapeleka katika wilaya ambazo zina upungufu mkubwa wa madaktari ilikufanikisha equity
 
Inasikitisha kuona Makao makuu ya Wizara inakuwa na Madaktari zaidi ya 80 ambao wanafanya kazi za kisiasa wakati sisi katika wilaya yetu hatuna Daktari( MD) hata mmoja kwani hata DMO aliepo ni AMO inasikitisha sana. Nchi hii haina chembe kabisa ya equity na fairness. Tukijaribu kufikiria kwa kina kama wachambuzi wa mambo inakuwaje Wilayani hakupelekwi Madktari na badala yake wanalundikwa Makao makuu ya wizara ya Afya hii ni aibu. Au kazi yao hao nikusubiri Madaktari Madaktari wenzao wagome na wao wakazibe pengo.

Naimba serikali baada ya kutatua mgogoro wa Madaktari na kuboresha Maslahi ya Watumishi wote wa sekta ya Afya iwapange kazi Madaktari waliopo makao makuu ya Wizara kwenda katika Wilayani kuokao maisha ya ndugu zetu.

Walichokifanya madaktari ni zaidi ya siasa ndugu yangu. Mwanasiasa kidogo anajali utu wa binadamu mwenzake. Uanjua mimi nimejiuliza maswali mengi sana eti moja ya madai ya Madaktari ni kutaka wenzao waliopelekwa mikoani warudishwe Dar. Una taarifa kwamba kuna walimu wanapangiwa vituo ambavyo baada ya kushuka toka kwenye basi wanachukua usafiri wa baiskeli na mwisho kabisa humalizia kwa miguu kwa vile baiskeli inakuwa haiwezi tena kufika aendako? Jamani kweli kama kuna siasa ziko nyuma ya mgomo huu basi sioni umuhimu wa kufanya siasa. Nilisikia mheshimiwa John Mnyika anatamka bila hata uoga kwamba anunga mkono wagonjwa wafe. Ilibidi nisikilize vizuri kama nilikosea kusikia lakini ukweli ukabaki kuwa ni yeye aliyekuwa akiongea. Wanyonge ambao kila siku wanapigia kelele kuwa wanawatetea ni wapi kama Madaktari wamepelekwa mikoani naye anaungana nao kuwa warudishwe Dar es salaam au wanyonge wako mjini tu? Serikali iwapeleke Madaktari mikoani na wilayani. Mimi ningeomba uchaguzi ufanyike pale Muhimbili kuwa wanaounga mkono mgomo wa madaktari wasimame nyuma yao na wanapinga mgomo nao wasimame nyuma ya Mgonjwa mmoja atakayeonekana kuwa na hali mbaya zaidi ili tuwaone hao wendawazimu watakaounga mkono Madaktari hao ambao wamechanganyikiwa kiasi hicho. Hawa ni kunyang'anya hata vyeti vyao vya taaluma ya utabibu kwa sababu ni wazi kwamba hawajui kwa nini walitunukiwa hivyo vyeti.
 
Kwa mfumo wa utendaji kazi serikalini mganga mkuu wa mkoa,wilaya,hospitali au mganga mkuu wa serikali hawawezi kugoma kwani wao wanawakilisha taasisi na taasisi ya serikali haiwezi gomea serikali! Hata migomo ya walimu hutasikia hata siku moja eti mwalimu mkuu wa shule ya serikali amegoma. Watagoma wengine ote ila yeye hatagoma
 
Back
Top Bottom