Ushauri: Maofisa Utumishi wa Wizara ya Afya wahamishiwe kwenye hospitali zilizo chini yake

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,240
4,466
Kufuatia uamuzi wa Amiri Jeshi Mkuu, kwamba hospitali zote za mkoa kuhamishiwa WIZARA YA AFYA, kumekuwa na sintofahamu nyingi miongoni mwa watumishi wanaohamia Wizara ya Afya.

Wakati Watumishi hawa wakiwa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa, RAS; mambo yao mengi walikuwa wakiyamalizia kwa RAS, na pale yalipohitaji msaada wa juu, basi ofisa utumishi wa RAS alikuwa anayapeleka moja kwa moja UTUMISHI (na sio TAMISEMI).

Kwa upande wa Wizara ya Afya, watumishi wake walioko Mirembe, Kibong'oto, Rufaa Mbeya wakiwa na matatizo ya kiutumishi, inabidi waombe ruhusa waende Makao Makuu ya Wizara ya Afya. Huko watatumia hadi wiki kufuatilia kitu ambacho kingemalizwa na ofisa utumishi kituoni kwake. Akishahudumiwa hapo file lake linakalishwa na ofisa utumishi kwa sababu ya wingi wa mafaili na itatumia muda kulifikisha UTUMISHI. Bahati mbaya sana maofisa utumishi wizara ya afya wana nyodo sana. Wameweka hadi vibao vya muda wanaotoa huduma. Wewe ukifika umetoka zako Arusha, lakini hujatokea ndani ya muda waliopanga wao; inabidi urudi guest na uje tena kesho ujaribu bahati yako.

Ukiangalia, watumishi wengi walioko hospitali za wizara ya Afya wana malalamiko mengi ya kutopandishwa vyeo au kutotambuliwa kada yao baada ya kutoka shule ukilinganisha na wale walioko chini ya hospitali za mikoa. Wana matatizo kibao ya kiutumishi.

Kuna madaktari waliokwenda kusomea udaktari bingwa na kurudi kazini, na kisha kukaa kwenye vituo vilivyoko chini ya Wizara ya Afya kwa miaka mitatu hadi mitano bila vyeo vyao kutambuliwa!!!! Hii imesababisha kuwe na huzuni miongoni mwa watumishi; lakini wale wenzao walioko chini ya RAS (wamehamishiwa Wizara ya Afya sasa), wamekuwa wakipata utambulisho mara baada ya kurudi masomoni.

Kuna umuhimu wa MoH kufanywa decentralization ya ofisi za Utumishi kwa kuhamisha watumishi wote walioko makao makuu na kuwapeleka kwenye Hospitali zilizoko chini ya Wizara. Na hata kama hawatoshi, basi kuna umuhimu wa kuajiri wapya. Na maofisa hawa wawe na mandate ya kuwasiliana moja kwa moja na UTUMISHI (sio MoH), na hivyo kuepuka mlolongo uliopo. Pia Wizara ianze kutumia mfumo wa electronics wenye taarifa zote za watumishi. Lakini pia kuna umuhimu mkubwa wa kufanya maboresho ya Ofisi ya Utumishi pale Wizara ya Afya; kwani hata DAP wa sasa anaonesha hatauweza mzigo huu aliopewa. Ikiwezekana DAP wa sasa ahamishwe, na aletwe damu changa toka nje ya Wizara.

Yote kwa yote inasikitisha kuona mtumishi anaingia gharama kibao, kwa ajili tu ya kwenda Wizara ya Afya akapitishiwe form yake ya mkopo, wakati mambo hayo yanaweza fanywa kituo chake cha kazi na huku anaendelea kuhudumia wananchi.

Sasa kumi, hawa maofisa Utumishi sasa wanashinda kuwasiliana na Waganga Wafawidhi na Makatibu Afya wa Hospitali za mikoa ili kujua idadi ya watumishi na mahitaji. Naamini hizi kazi zilipaswa kufanywa na ofisa utumishi aliyepo kwenye kituo husika.

KM hamisha hao Maofisa Utumishi waende Mikoani. Wanafanya nini huko? Wameajiriwa kuhudumia watumishi walioko mikoani sasa, wanafanya nini Makao Makuu?
 
Naamini kutakuwa na series ya maelekezo kufuatia mabadiliko haya...
 
Hakuna Wizara ya hovyo Kwa upande wa utumishi Kama Wizara ya afya.
Maafisa utumishi wa hii Wizara nahisi huwa wanapenda Sana watu mnapoacha kazi mikoani na kwenda ofisini kwao kupanga foleni.
Sasa wameongezewa mzigo itakuwa balaa kabisa.
Wizara ya afya mtu anafanya kazi miaka mitatu hata sita hana barua ya kuthibitishwa kazini.
Madaraja watu Wana miaka zaidi ya kumi hawajawahi kupanda.
 
Back
Top Bottom