Madaktari wauaji Mt. Meru Hospital arusha

anashangaza sana mtu huyu!pale hosp kuna sehemu ya kutoa malalamiko,anaweza kwenda polisi kureport mauaji au afike kwa mbunge wake ampe malalamiko na sio kubwatuka kama waandishi wa habari za udaku.

Mh. Hakuna mtu anabwatuka kama imekuuma sana na wewe ni miongoni mwao kwani unachokifanya ni kumtetea mtu ambaye unamjua kwa nje na hutembei naye na hujui moyoni anafikiria nini. Bado tunaendelea na uchunguzi na within very few days tutaweka sauti na picha na wahusika wengine humu kwani gadgets za hiyo kazi tunazo.

Kama wewe ni Dk. Na imekuuma sana cha kufanya siyo kutetea uovu kwani sikutokea from no where nikaanza kuandika rumours bali ninaandika nilicho experience sasa wewe unakana kwa ushaidi upi?. Inawezekana kabisa ukawa mmojawapo. sasa next time utakaposikia sauti za maneno machafu manesi na madokta wanayowajibu wagonjwa ninaamini you will re-think standing for murderers.
 
toka lini daktari akakupa karatasi ya discharge?kwa kawaida karatasi hii hutolewa na attendant!


If that is the case then how long it take to prepare? two hours, three hours or?

Nafikiri wewe una pepo mchafu yuleyule wa mauti kama ni Dokta na unatakiwa utubu au uache hiyo kazi kwani haikufai.
Kama Dr. hatoi karatasi ya discharge basi alipogundua ndugu wa mgonjwa na mgonjwa walikuwa wameshaisubiri more than two hours basi alipomaliza kuandika angemwita attendant azigawe na siyo kufunga file na kuondoka tena akaacha siyo ndani ya wodi bali nje ya kiofisi kidogo wakati attendant yuko wodini akigawa dawa. Attendant angepiga ramli ajue sasa karatasi imeshaandikwa au Dr. angemshtua?

Your arguments are simply baseless better stay untuned instead of distorting JF members
 
amekuwa discharged akiwa anaongea na alitembea mwenyewe bila kusaidiwa na kwa spidi kubwa tu mpaka nje ya geti tulimokuwa tume paki gari na akaingia mwenyewe.
sasa huyu mgonjwa anayeweza kutembea kwa kasi kubwa mpaka kwenye gari bado alihitaji drip ya glucose?ya nini tena wakati alikua vizuri!yaani wewe badala ya kumshukuru daktari wake eti unasema ni muuaji.kweli binadamu hatuna shukrani.
 

wewe ni mbwatukaji kwa sababu matendo ya dr mmoja ambayo huwezi kuyathibitisha yamekupelekea kuwachafua watumishi wote wa mt meru 'eti wauaji' tumia busara na ufute usemi wako!ushahidi ulionao peleka mahakamani au baraza la madaktari Tanzania utapata haki yako au na huko utasema ni wala rushwa?
 

mkuu naweza kusema dr huyu alishamaliza kazi yake kwani kama ameshaijaza karatasi ya discharge hapo inatosha,kinachobakia ni attendant ku-collect discharge forms za wale wote walioruhusiwa na kuziregister na kuhakikisha maelekezo yaliyoandikwa kwa ajili mgonjwa yanatekelezwa mfano kumtoa canula,kumpa karatasi za kuchukulia dawa,kumpa elimu ya afya,kumuelekeza dalili za hatari n.k
sasa usitegemee kwa mazingira ya hospitali yenye wagonjwa wengi kama mt meru mambo haya yatatekelezwa kwa mda wa sekunde au dakika.wewe mwenyewe ulimshuhudia attendant akigawa dawa sasa ulitaka aache kuwahudumia wanaoendelea kuwapo wodini(wenye hali mbaya sana) halafu amuhudumie aliyepona na kupata ruhusa kisa ni ndugu yako!usiwe selfish mkuu!
Kuhusu dr kuondoka yawezekana alielekea clinic kwenda kuona lundo la wagonjwa wengine lenye mahitaji pengine makubwa kuliko huyo wa kwako.
Nasisitiza:umekosa utu!unapenda kuropoka na sio mstaarabu,hutaki kuuliza kwa upole hatimaye unaelekea kuhukumu wanaohusika na wasiohusika!!!
 

hahahahaaa hahahaa umeniua mbavu zangu kwa kweli, kwa hiyo alisubiri ukachojoa kwanza ndio akakwambia sindano zimeisha? hehehe
 


Lengo langu siyo kubishana na wewe bali kufikisha hii message in the strongest term katika clarity yake kama shahidi wa mambo niliyosema awali. Suala la kuwa au kukosa utu halipo kwani hapa natetea utu wa mgonjwa na huo ndio ustaarabu na ubinadamu. Chama cha madaktari hakinihusu mimi kwani kazi yake kubwa ni kutetea haki na maslahi ya madaktari na siyo kutetea wagonjwa wala ndugu zao kwa hiyo usinitege.

Narudia kusema : Hata baada ya daktari kumaliza kuangalia wagonjwa wote wodini tulisubiri karatasi ya discharge kwa more than one hour wakati wengine wakiwa wamepewa long time.Kisha ikaandikwa na kufichwa ndani ya file mpaka attendant alipotuonea huruma akaenda kuitafuta.

Sina lengo la kumwaribia mtu hapa kwani Dr. Israeli Kassago sina kisasi naye wala simfahamu ila kutokana na hiyo drama aliyofanya na huyu Nurse mweupe wa kimachame ndo nilibidi nitafute jina lake
 
Kuna uwezekano Dr. I. Kassago alimaliza kazi ila hakutimiza wajibu wake.
 

Kauli ya kuwaita madaktari na manesi wauaji si kauli nzuri nakubaliana na wewe kabisa. Maana kuna doctors and nurses who are so dedicated to their work. Wanawasaidia wagonjwa kupita kiasi bila kujali how much they are getting at the end of the month. They work for patients and God and not for money and I have met so many of this kind. But, ukweli utabaki palepale kuna manesi wana roho mbaya jamani, tuache kubisha. Yaani unatamani kumzaba vibao kwa jinsi wanavyokera. The way they talk to patients, its like they are talking to rubbish, ni kama wagonjwa ndio wana shida na mimi kama nurse siwezi kuumwa so watajua wenyewe. Wanawagombeza wagonjwa mpaka unawaza sasa kama hataki hii kazi si aache kuliko kumfokea mgonjwa ambaye anahitaji ukarimu wa hali ya juu? Huko labor word unakosemea ndio usiseme, manesi wanawafokea wamama hasa ambao ndio wanaface labor pain, kuna rafiki yangu alijifungulia chooni kisa mtoto wake alifia tumboni (siyo Mt. Meru Hospital lakini) so doctor akaona ni bora asimfanyie C/S maana tayari mtoto amekufa na inauma sana kuuguza kidonda kisicho na mtoto, hivyo wakamuwekea maji ya uchungu, wakati rafiki yangu uchungu ndio umepamba moto anataka kwenda kujisaidia akamuomba nurse msaada, badala ya nurse kumletea chombo akamwambia (tena kwa kufoka) nenda chooni na wakati yeye kama nurse anajua yule anaweza kuwa mtoto anataka kutoka, matokeo yake mtoto akatokea chooni, sasa hebu niambie ni kwa kuwa mwanae alikuwa kashafia tumboni ndio akaona hana thamani tena?
 

Nadhani MVUMBUZI unahitaji kusoma upya post yako hasa hizo sehemu nyekundu...nadhani hata wewe mwenyewe utajishtukia kuwa hayo yapo mbali kidogo na ukweli. Si kitaaluma tu, hata kibinadamu. Na hujatenda haki kwa madaktari na wahudumu wa afya wanaohangaika kutwa kuchwa kuokoa maisha ya watu kwa ujira wa kutupa wakati wewe ukikoroma katika 6 x 6 yako! Maumivu ya kupoteza ndugu/rafiki au mtu wa karibu ni makubwa na kila mtu ana jinsi yake ya kujiliwaza, labda kwako wewe kukasirika, kulaumu na kushutumu watu wengine ndio jinsi yako ya kujiliwaza lakini...its not fair!
 

Its true, kwa jinsi alivyoandika ame-generalize. Wafanyakazi wa afya wanateseka sana, si kifedha tu hata mazingira wanayofanyia kazi ni magumu sana, hospitali nyingi hazina hata vifaa ambavyo vitamfanya nurse/doctor kufanya kazi vizuri, mambo mengi ni ya kuunganisha sana. But at least what we should all do is appreciating those who are trying so hard to help patients no matter how bad their lives, working environment are.
 

hata mimi sina lengo la kubishana na wewe.we unaona tunabishana?lengo langu ni kukusihi utumie kauli nzuri(ya kiungwana) wakati unaelezea matatizo ya liyokupata hospitali ya mt meru,you are calling them murderers!bila kujali aliyekukosea ni mmoja au wawili.
Kuhusu wapi upeleke malalamiko yako ni vyema ukaelewa utaratibu(acha jazba na upunguze hasira)
kwanza ongea na incharge wa hospital dr.mlai,au R.M.O dr Toure,au Baraza la madaktari Tanganyika(medical council of Tanganyika)
ukiona huku hakuna haki nenda mahakamani au mwambie mbunge wako.huu ndio utaratibu wa kiungwana na sio matusi kama unayoyatoa.

Najua huna kisasi na huyu daktari na nesi lakini inashangaza kwa nini unamchukulia dr.israel ana kisasi na mgonjwa wako to the extent anataka kumuua.walikuwa wanajuana kabla?huyu dr ni muuaji kiasi hiki?tsh 2000 ??NOO!! NAAMINI UMEKURUPUKA.WATAKE RADHI MADAKTARI NA MANESI WA MT MERU.
 

I think you understand me. Kwanza lazima ujue sijawaita madaktari wote wauaji kwani tangu mwanzo nimesema ni baadhi. Nashukuru kama wewe ni nurse lazima una hofu ya Mungu kwani umeongea ukweli tofauti na madaktari wenzako hapa JF wanapambana na ukweli kama huu. Na mimi nimetoa niliyoyashuhudia na nitaendelea kutetea ukweli huu kwani sielewi kwa nini sisi wasomi tunaojua baya na jema kuamua kufanya lililobaya na kuacha lililo zuri. Reward ya mtenda mabaya ni ubaya na ndo maana huu mjadala umetokana na ubaya aliofanyiwa mtu na katu nisingeweza kumsifia kwa aliyotenda dokta mhusika.
 


Niliyoandika ni ukweli na sijaambiwa na mtu, this is my personal experience man. Mkuu mimi nami pia silali na wakati mwingine nakuwa mbali na familia kwa ajili ya kuwatumikia watanzania kwa moyo wa dhati na upendo huku nikijua kazi niliyo nayo pamoja na kusoma si haki bali dhamana niliyopewa na Mungu kusimama katika nafasi yangu kuwasaidia watanzania in my capacity. Pale panapotokea problem kuna feedback mechanisms highly efficient kuhakikisha tuna review utendaji wetu to satisifaction of beneficiaries na siyo kwa lengo la kuwa prove walalamikaji wrong. Siogopi kukosolewa na pale ambapo kuna tatizo kama gentleman tuna chukua hatua haraka na siyo kubisha. Huyu Dk angekuwa amefanya sehemu yake nisingetu,mia muda wangu mwingi kujibu hizo hoja za kujisafisha. Hatua lazima zichukuliwe na siyo kutaka kujisafisha kwani cha kufanya hapa ni kuprove kwa kuchange- mindset za madaktari ili tuone kwa vitendo wanachosema.
 
mfumo huu unaosema sio unique kwa taasisi unayofanyia kazi bali ni universal hata mt meru upo,sasa wewe kwa makusudi umeamua ku-ignore kwa kisingizio madaktari eti wanateteana!kwa taarifa hakuna proffesionals wasioteteana but mtu hutetewa iwapo hajakiuka maadili na miiko ya proffession husika.nenda katoe feedback ya huduma aliyopewa mgonjwa wako hapo hospital, utaonekana jasiri,muungwana na mpenda maendeleo but kuja hapa jf na ku-smear mtu au taasisi inaonyesha usivyokuwa mstaarabu na mstahimilivu.
 


I'm very sorry man, mimi siko hivyo, najua haki yangu na HATAOMBWA RADHI DAKTARI YOYOTE NILIYEMTAJA HAPA. Sina tabia ya kuwa please binadamu na mara zote nina tabia ya kukiongelea kitu in ITS TRUE COLOUR . Kama utaona ni metoa MATUSI it's as per level of your perception ila mimi najua nilichoongea siyo matusi na mimi sina kumbukumbu za lini mara ya mwisho kumtukana mtu. My mouth is clean from dirty words, alcohol and cigarette kwa hiyo najua sikukurupuka na nilikuwa kwenye sense zangu zote na hata sasa bado nasema niliyoandika ni sahihi na I WON'T CHANGE ANYTHING.
 

Ningetaka kurefusha mambo ndo ningekwenda kulalamika mkuu ila ninavyojua taasisi nyingi za serikali including yours wana STATUS QUO ambayo wana operate tangu nchi ilipopata uhuru kwa hiyo kutoa malalamiko kama hayo wangenishangaa kwani hiyo ndiyo organisational culture yao. Hii pia ni sawa na kesi ya nyani kupeleka kwa ngedere kwani lazima mlalamikaji apoteze kesi.
 
mkuu edit hiyo title ya thread ili tukuelewe unasimamia wapi?


Hiyo ndiyo perception yangu na ni ngumu kuelewa vinginevyo kwa yaliyotokea na the thread will stay so long it's valid and relevant.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…