Madaktari watibuana; Baada ya wenzao kuomba radhi, wengine wasema hawahusiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari watibuana; Baada ya wenzao kuomba radhi, wengine wasema hawahusiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMATANO, SEPTEMBA 19, 2012 08:49 NA ELIZABETH MJATTA, DAR ES SALAAM


  *Baada ya wenzao kuomba radhi, wengine wasema hawahusiki
  *Wasema walioomba msamaha wanatumiwa kwa masilahi yao

  Jana Mwakilishi wa Madaktari kwa Vitendo, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Frank Kagoro, alisema tamko la kuomba radhi lililotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari walioathirika na mgomo, Paul Swakala, haliwahusu madaktari wote.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk. Kagoro, alisema tamko lililotolewa na Swakala linakihusu kikundi cha watu wachache ambao nia yao haijafahamika sawasawa.

  Katika mkutano huo uliowajumuisha viongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Kagoro alisema kwa sasa siyo wakati wa madaktari hao kuomba msamaha, kwa sababu suala lao lipo kisheria na kinachosubiriwa ni Baraza la Madaktari Tanzania (MCT) kuwaita kwa ajili ya kuwahoji.

  "Lile tamko siyo tamko letu wote, lile ni tamko la kikundi cha watu wachache ambao hatujui wana lengo gani na nia gani, lakini mkituuliza sisi tutawaambia tunasubiri tuitwe na MCT ili kuhojiwa.

  "Mahali suala letu lilipofikia, halina lugha ya msamaha, ninachofahamu ni kwamba, sisi suala letu tunalishughulikia kwa kushirikiana na Jumuiya, kwani tumefikia katika hatua ya kusubiri kuitwa na MCT.

  "Katika hili tulikubaliana kwamba, jumuiya itabeba gharama za kutafuta wanasheria, kwa hiyo, wale madaktari waliotoa lile tamko hatujui wana nia gani," alisema Dk. Kagoro.

  Akizungumzia suala hilo, Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Nchini, Dk. Godbless Charles, alisema kipindi hiki ni kipindi chao kutumia hekima na busara, kwani ni kipindi kigumu kwao.

  Kutokana na hali hiyo, alisema kuna kila sababu yeye na madaktari wenzake kuepuka tabia ya kutumiwa na kikundi cha watu wachache wanaofanya hivyo kwa masilahi yao binafsi.

  "Tunapenda ieleweke kwamba, mgomo wa madaktari si tukio, bali ni mchakato ambao utaendelea kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ndiyo maana tumeshuhudia migomo katika nyakati tofauti pamoja na kujitokeza kikundi au mtu kutumiwa kuomba msamaha kwa lengo la kudhalilisha taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha hali ya afya nchini na maslahi ya watumishi kwa ujumla.

  "Unajua, hata sisi tunawashangaa wale ambao wameomba msamaha, sasa waliomba msamaha kwa kosa gani?

  "Nasema hivyo kwa sababu sisi madaktari tulio chini ya usimamizi wa madaktari bingwa (interns), hatuwezi kufanya kazi bila usimamizi wa madaktari bingwa ambao wako katika mgomo.

  "Kuhusu suala hili la interns ikumbukwe kwamba, Julai 10, mwaka huu, Baraza la Madaktari (MCT) lilitoa taarifa kwa umma, kwamba, limesitisha leseni za muda kwa madaktari walio chini ya mafunzo kwa vitendo.

  "Pia MCT waliahidi kutuita mmoja mmoja kwa ajili ya kutuhoji hadi taratibu zote zitakapokamilika, lakini cha kushangaza hadi sasa ni miezi miwili imepita hakuna kinachoendelea.

  "Katika vikao mbalimbali ambavyo tumefanya na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na idara zake, tumekuwa tukisisitiza kuwa, suala hilo lipo kisheria na Interns wasubiri kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa, hivyo tunaitaka MCT iharakishe kuwaita ili kuharakisha upatikanaji wa haki.

  "Sisi tumejiandaa vya kutosha na taratibu za kisheria na tutahakikisha tunaweka mawakili pale interns watakapoanza kuhojiwa, kwa kuwa sheria inayounda MCT inatoa nafasi hiyo.

  "Lakini hata ukiangalia hoja za hao walioomba msamaha hazina uzito wowote, huwezi kusema ulilazimishwa kugoma wakati mgomo umekwenda kwa vipindi vitatu mfululizo na ulishiriki, hizi ni sababu ambazo zinatupa wasiwasi kwamba kikundi hiki kina sababu zake zilizojificha," alisema Dk. Charles.

  Naye Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Dk. Edwin Chitage, alisema huenda tamko lile la madaktari lina misukumo ya nje.

  "Katika mazingira kama haya, kila mtu ana uwezo wake wa kupokea jambo, kuna ambao wanaweza kuhimili mikikimikiki na wengine hawawezi, kwa hiyo wale sisi hatusemi kwamba tunawakana. Tunasema hatukubaliani nao na naamini siyo makubaliano ya interns wote," alisema Dk. Chitage.

   
 2. Piere. Fm

  Piere. Fm JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,194
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mambo ya Divide and rule.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Pesa sabuni ya roho! Kama Ulimboka aliahidi atazungumza, mpaka kesho kanyamaza kimya! Pamoja na kutesa na kudhalilishwa kote! Sembuse vijana hao! That is a leadership style! At least someone had the courage kukanusha! Msamaha my foot in high heel!
   
 4. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanini wanahangaika sana hawa jamaa maana kama mngekuwa mnamadai ya msingi na mnataka umma uwaelewe mngemleta ulimboka atueleze jinsi Ccm walivyompiga na usalama wa taifa walivyomtoa meno na plaizi ila amekaa kimya na ninyi hamtoi tamko hapo ndo mlipokosea sanaaaaa na itakula kwenu vibaya
   
 5. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  The arising of Ulimboka from the dead on early October
   
 6. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu King'asti, Just because he's quiet doesnt mean he was bribed.. we(citizens) have had evidence(his confession..from media-news papers, youtube etc) but bado tuko kimyaaaaaaaaa...KWANI SNA SISI(MERE CITIZENS) TUMEPEWA SABUNI YA ROHO mkuu? i dont think so.

  May be if we should do a little something with information in plate before we reach for another dish..!!
   
 7. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kama wenzake wanatumiwa ina mana na yeye anatumiwa pia.wenye akili wameona madhara ya kuwatesa watanzania kwa kuwanyima huduma,yeye anang'ang'ania ujinga wa nn
   
 8. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Huyu nae ni mcharuko mwingine tena,inaezekana ye ana kaduka chake cha kuuza madawa ndio mana haoni uchungu wa ugumu wa maisha wanaokutana nao wenzake.msaliti of this karne
   
 9. b

  bagwell Senior Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Agh wote munajuana mna sijui tumsikilize nani.
   
Loading...