Watu Kama wewe inatakiwa uundwe Mkoa mpya(Lalaland)kwa ajili yenu.Pole sana mtambuzi,lakini tatizo letu wabongo tunapenda kudanganywa mgonjwa akiambiwa ukweli hatupendi.Pili muhimbili ni hospitali ya kufundishia,kwahiyo huwezi kwepa mgonjwa wako kutumika kama kitabu.
mkuu umejibu vyema sana ila naomba nikwambie matatizo yanayozaa haya yote hapo juu.kwa kufuata maswali ambayo nimeyaibua kwenye hoja zako.Kama ndio hivyo basi yamefanyika makosa makubwa haya:
1. Kutokumpa mgonjwa opportunity ya kuopt out kutumika katika kufundisha wanafunzi. Hii ni haki ya mgonjwa kuamua kama yuko tayari kutumiwa kimasomo au la.
2. Mgonjwa kutojulishwa taarifa ya hali yake mapema. Majibu ya mgonjwa yakipatikana tu ni wajibu wa daktari kumjulihsa mgonjwa juu ya majibu hayo mapema iwezekanavyo.
3. Kupita round na wanafunzi mbele ya ndugu za mgonjwa. Kunaweza kuwa na mambo ambayo mgonjwa hataki ndugu zake wajue. Kuzungumza kuhusu afya ya mgonjwa mbele ya watu ambao si wahudumu wa afya wanaomhudumia ni kosa la kimaadili unless mgonjwa mwenyewe atoe ruhusu.
4.Kutoa taarifa mpya kwa watu wengine (wanafunzi) mbele ya mgonjwa bila kumshirikisha mgonjwa.
Watanzania huwa tunapenda sana kukesha tukiwalaumu wanasiasa, lakini inatakiwa ifike mahali tujiangalie kila mmoja katika kazi yake, je anaifanya kwa ufanisi???
Mtambuzi pole sana, wanaacha kumkomoa Kikwete na CCM yake, wanatukomoa sisi ambao hatuna uwezo hata wa kulipia hospitali kama ya Aga Khan.
Waganga wa kienyeji nao feki ile mbaya,
waombeaji nao wamekuwa magumashi ile mbaya.
Sijui tukimbilie wapi ili tupone.
Na wakati huohuo kila tunachokula na tunywacho tunaambiwa eti ni sumu.
Duhh
Pole sana mtambuzi,lakini tatizo letu wabongo tunapenda kudanganywa mgonjwa akiambiwa ukweli hatupendi.Pili muhimbili ni hospitali ya kufundishia,kwahiyo huwezi kwepa mgonjwa wako kutumika kama kitabu.
Tatizo sio kuwashtaki mkuu. Tatizo ni unawashtakia kwa nani???? Kuna sekta nyingi sana Tanzania zinatakiwa kuvunjwa na kuundwa upya ikiwepo hii ya Afya. Hao Madaktari kutokuwa weledi ni tatizo kubwa sana. Nilishawahi kumpeleka Wife kwa Daktari mmoja wa wanawake(Gyno) kwa check up ya kawaida kwa akina mama. Baada ya kuingia kwa Dr. Akaanza kueleza matatizo ya mgonjwa aliyetoka kumuona,yaani aliyekuwa mbele kwenye foleni kabla ya Wife. Alikuwa anaeleza vitu personal sana mpaka Wife aliponielezea nilichanganyikiwa. Halafu cha kushangaza Huyo Dr. Alikuwa ni mwanamke. Kwa hiyo Ina maana hata Issue za Mke wangu alimuelezea huyo anayefuata. Ethics Zero kabisa.
Pole sana Mtambuzi na familia kwa kuuguliwa na Mama.
Pole sana mkuu.
Ni kweli kabisa kitendo kilichofanywa na hao madaktari siyo cha kiungwana lakini na wewe haukupaswa kususa.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
ZeMarcopolo hii ndio thread unayopashwa kuchangia sio kulamba matapishi ya wanasiasa unadharirisha ilimu yako. Nimekupa like ukiendelea kulamba matapishi ya wanasiasa na kukubali malipo ya nape kukaa online 24hrs kuandika ujinga na hii like nitaitoaKama ndio hivyo basi yamefanyika makosa makubwa haya:
1. Kutokumpa mgonjwa opportunity ya kuopt out kutumika katika kufundisha wanafunzi. Hii ni haki ya mgonjwa kuamua kama yuko tayari kutumiwa kimasomo au la.
2. Mgonjwa kutojulishwa taarifa ya hali yake mapema. Majibu ya mgonjwa yakipatikana tu ni wajibu wa daktari kumjulihsa mgonjwa juu ya majibu hayo mapema iwezekanavyo.
3. Kupita round na wanafunzi mbele ya ndugu za mgonjwa. Kunaweza kuwa na mambo ambayo mgonjwa hataki ndugu zake wajue. Kuzungumza kuhusu afya ya mgonjwa mbele ya watu ambao si wahudumu wa afya wanaomhudumia ni kosa la kimaadili unless mgonjwa mwenyewe atoe ruhusu.
4.Kutoa taarifa mpya kwa watu wengine (wanafunzi) mbele ya mgonjwa bila kumshirikisha mgonjwa.
Watanzania huwa tunapenda sana kukesha tukiwalaumu wanasiasa, lakini inatakiwa ifike mahali tujiangalie kila mmoja katika kazi yake, je anaifanya kwa ufanisi???
watu mnavituko! hahhahaha yaani husahau ya jukwaa la siasa.ZeMarcopolo hii ndio thread unayopashwa kuchangia sio kulamba matapishi ya wanasiasa unadharirisha ilimu yako. Nimekupa like ukiendelea kulamba matapishi ya wanasiasa na kukubali malipo ya nape kukaa online 24hrs kuandika ujinga na hii like nitaitoa
Mtambuzi pole sana, wanaacha kumkomoa Kikwete na CCM yake, wanatukomoa sisi ambao hatuna uwezo hata wa kulipia hospitali kama ya Aga Khan.
Waganga wa kienyeji nao feki ile mbaya,
waombeaji nao wamekuwa magumashi ile mbaya.
Sijui tukimbilie wapi ili tupone.
Na wakati huohuo kila tunachokula na tunywacho tunaambiwa eti ni sumu.
Duhh
Mie ningewashtaki.....haiwezekani wamfanyie hivyo mama wa watu.
Poleni sana mkuu.
Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.
Duuh, madaktari wengine bwana, where is the so called privacy ya mgonjwa? Ikifika jioni si watu wote tunajua matatizo ya wagonjwa walioenda kumuona huyo daktari?
Niliwahi kupeleka mtoto hospitali moja DSM, of course mtoto alikuwa na matatizo ambayo hata mie mama mzazi nilikuwa nalia kila siku. Huyo daktari aliitaje madaktari wote wa watoto hapo hospitalini? Chumba kilijaaje hao madaktari na mishangao ya oooh, we are very sorry...aah poor kid...and the blaah blaah... Sijui nilitoa ujasiri wapi wa kutulia na kuendelea kuwasikiliza, manake kilichokua kichwani ni kunyakua mtoto wangu na kutoka nje.....