Madaktari - tutakutana na waziri mkuu jumatatu

I think si kwamba Drs wanachodai ni kuwa superclass. infact watumishi wa kada zote wanatakiwa kuungana na madoctors ili mfumo mzima wa mapato kwa wafanyakazi uwe fair. Unajua kwa nini serikali inagoma wito wa CDM kuondoa posho zisizo za lazima? huko ndiko wanakoponea na kuchakachulia mabilioni ya pesa yanayowafanya waishi kama superclass.
Mishahara yao ni kama yetu tu. And I am sure ukiwauliza mishahara yao ghafla hawawezi kukumbuka kwa kuwa wanaishi kwa posho tu. Si umesikia juzi ikulu ikikanusha kutumia mil 300 msafara wa rais lakini ikapotezea kusema ni Sh ngapi?
Hebu niambie sitting allowance ya 200,000 kwa KUKAA "mchana" kwenye mjengo na 10,000 kwa kukesha unazalisha akina mama?
Madaktari wetu msilegeze kamba madai yenu ni ya msingi kabisa.
 
Dr. Klinton asante kwa hili, niliuliza sasa mwito wa leo mtaitikia?, au mtashikilia ku dictate terms kwamba siku na mahali mlipopanga nyinyi?.
Haihitaji akili ya ziada kutambua Pasco ni mtumishi wa nani!
 
madaktari huo siyo uzalendo,watu wanakufa mahospitalini kwa kutojali utu kwanza. Kwa nini hamtaki kuonana na Waziri Mkuu mkazungumza naye mpate mwafaka.Je ,ni lazima madaktari wote wahudhurie au wawakilishi wenu hawana hoja za msingi? Si dhani kama kila daktaria ataongea kwenye hicho kikao.

Ushauri wangu kwenu Madaktari(MAT),kusanyeni kero zote kutoka mikoani ili muweze kuzijumisha katika mazungumzo yenu.
Kama hakuna hoja za msingi basi huo ni uhaini na ugaida wa hali ya juu.

Kwako JK(RAIS),vunja ziara yako huko DAVOS uje uokoe jahazi hili.Nchi inazama taratibu,wasomi hawana uzalendo tena na nchi yetu.

Kila sekta ikigoma,ndipo mtaona kila kada ni muhimu wala siyo madaktari pekee.acheni dharau kwa POLISI,WALIMU nk.

Mungu iokoe Tanzania inazama kama meli ya SPICE ISLANDERS!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Naomba idadi ya wagonjwa waliofariki kwa kukosa huduma ya madaktari..
Na waliokufa kwa magonjwa ya njaa nyumbani kwao idadi yao mbona huombi? Mbona unawataka madaktari wawe wazalendo na wabunge, mawaziri na makatibu wakuu wanaoiuza nchi hii mbona hutoi ushauri? Kama ni wagonjwa kufa kwa kukosa huduma haikuanza kwa madaktari kugoma imekuwepo daima kwa kukosa dawa au kupewa dawa feki zilizoagizwa na haohao unaowatetea.
 
Back
Top Bottom